Bastola ‘yamvuruga’ Malisa wa UVCCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mwandishi Wetu - Raia Mwema


malisa219.jpg



MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Mali


Ahojiwa polisi, risasi zajeruhi mwanafunzi wa CBE


MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Benno Malisa, amehojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa madai ya kutodhibiti bastola yake ambayo ilitumika kumjeruhi tumboni mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) Dodoma, Raia Mwema imethibitisha.

Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti kuwapo kwa tukio la kumfyatulia risasi mwanafunzi huyo, Emmanuel James Nyakiomo (30), eneo la Sinza, Mugabe, Dar es Salaam karibu na Hoteli ya City Style.

Uchunguzi zaidi wa gazeti hili sasa umebaini kuwa kesi kuhusu tukio hilo lililotokea Novemba 30, mwaka huu, ilifunguliwa kwa mara ya kwanza katika Kituo cha Polisi cha Urafiki, kwa taarifa UPR/RB/100664/11.


Hata hivyo, licha ya jalada kuhusu tukio hilo kufunguliwa kwa takriban mwezi mmoja sasa, kutokana na sababu zisizo wazi kesi hatua zaidi za mbele kuhusu tukio hilo zilisuasua kuchukuliwa na baadhi ya polisi.


Taarifa kuhusu jalada hilo la kesi zinaeleza kuwa gari iliyohusika katika tukio hilo ni aina ya Landcruiser, yenye rangi nyeupe ikiwa na namba za usajili T439BAW, linalodaiwa kutumiwa na Malisa.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, wakati wa tukio hilo Benno Malisa hakuwapo kwenye gari ambalo aliacha bastola yake na dereva aliitumia kuwafyatulia risasi vijana waliomhoji sababu ya kuwamwagia maji machafu.


Katika toleo lililopita la gazeti hili, yaliripotiwa maelezo ya mmoja wa watoa habari wetu akisema; "Baada ya vijana hao kupiga kelele za kwa nini wamemwagiwa maji machafu, dereva huyo ‘alipaki' gari na kuanza kuwafokea vijana hao na walipojibizana naye alifyatua risasi mbili hewani na baadaye moja kumlenga tumboni Emmanuel."


Tukio hilo ambalo lilitokea saa saba usiku wa Novemba 30, 2011, limetajwa kuibua maswali mengi, ikielezwa kuwa kulikuwa na juhudi za kuzuia wahusika kuchukuliwa hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria.












 
Yaani Kila kiongozi CCM na Risasi baada ya Nyerere kufariki?
 
Yana mwisho! Ipo siku sheria itaongoza nchi hii na kila mtu atawajibika pasi kuangalia ni nani
 
huyu malisa nae ajaacha umalaya saa saba na nusu usiku anatafuta nini
,miaka yote alikesha na mizigo ya sinza akiwa chukokikuu sasa nini jipya anafwata kuacha kulala usiku jamani
acheni kujizalilisha alafu si ndio huyu anadai uongozi wapewe vijana kamweeeeeee wakajaza cd sinza usiku gari za mawaziri hata sikumoja baab jk jaza wazee mpaka watakapobadilika hawa
 
Huyu dogo alienda kupiga show pale karibu na City Styles. huku nyuma dereva kajiongeza kwenye bastola. Nchi yetu bwana. Kila mtu yuko juu ya sheria kisa eti ni kiongozi kwenye magamba. Ipo siku tuu
 
Kama ni kweli huyo dereva anastahili adhabu kali kwa ubabe aliouonesha, Malisa anastahili kupokonywa hiyo bastola kwa kutokuwa makini..!
 
Back
Top Bottom