Hivi punde, kumetokea ajali ya Basi la Princes munaa lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, katika kijiji cha Mtanana Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma.
Good decomm,wimbi la ajali sasa naona limekuwa sio geni machoni kwetu. Najitahidi sana kuripoti habari za ajali lakini naona kuna watu hawapendi mpaka wameanza kuniita majina ya ajabu ajabu kitu ambacho sipendi.
Kila siku tunawazika wapendwa wetu kwa uzembe wa madereva na mamlaka husika...kila siku mayatima wanaongezeka kutokana ongezeko la ajali hizi kila kukicha.....tumekuwa tukipiga makelele na mamlaka husika kulitafutia ufumbuzi wa kudumu suala hili..lakini mamlaka husika zimeweka pamba masikioni....
Kumbe nawe umeiona hiyo kitu, nilipoona picha nikaona kitu hicho, nikajiuliza maswali kadhaa halafu nikakosa majibu. Hebu wajuzi wa mambo watupe majibu kama yapo, hicho ni kitu gani, ni moto gani huo wapendwa?