mende 2014
JF-Expert Member
- Apr 13, 2014
- 763
- 131
Kwa habari ambazo hazijathibitishwa ni kwamba kuna taarifa kuwa basi la Mwanza Coach limetumbukia katika mto Simiyu mchana baada ya mvua ikitokea Musoma kwenda Mwanza.
Mwenye taarifa hizi atujuze tafadhali.
Siyo mto Simiyu; ila ni mbele sana ya mto Simiyu ila kuna daraja na korongo; kweli gari nimeiona ipo kwenye korongo lenye maji ilikuwa imezama level ya seat. Sikuweza kupiga picha ni sehemu yenye kona magari yanaporomoka hovyo
hivi hii kampuni ilisharuhusiwa kurudi barabarani?
Hayo mabasi yatatumaliza watanzania. Yafungiwe tena. Kwani aliyeyaruhusu ni nani? Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.