Basi la Lucky Star pulizeni dawa ili kuua Kunguni

Basi la Lucky Star pulizeni dawa ili kuua Kunguni

Domhome

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2010
Posts
3,198
Reaction score
3,975
Jumatano ya 17 Januari 2018, nilisafiri na basi la Lucky Star toka Mwanza kwenda Dodoma, pale Mwanza tuliondoka saa 7:30 mchana na tulifika Dom saa 7 usiku.

Basi lile japo kwa muonekano liko vizuri lakini ilikuwa ni mateso kwa abiria tulosafiri nalo siku ile kwani Kunguni walitushambulia mno. Binafsi mwanzo sikutambua kuwa ni Kunguni ila Mara tu tulipofika Bahi, majira ya saa Sita usiku ndo abiria ndani ya basi lile tukagundua kumbe muwasho tuupatao ni mng'ato wa Kunguni na hii ni baada ya basi kusimama Princes Hotel, kwaajili ya chakula na uchimbaji dawa ndipo Kunguni walionekana "mubashara" na abiria wote.

Ewe mmiliki wa gari hili hurumia abiria wako kwa kufanya fumigation ili uuwe Kunguni na Mende waliomo ndani ya gari yako, yawezekana wafanyakazi wako wana sahau au kupuuzia kukujulisha hili....

Kumbuka, biashara ni ushindani !!
 
MABASI MENGI SANA HASA YA SAFAR NDEFU YANA KUNGUNI,M NILIPANDA CITY BOY YA KARAGWE KWENDA BUKOBA BAC LINA KUNGUNI WAKUTOSHA.
 
Kweli kabisa hizo gari zina kunguni. Tuliwapouliza muhudumu akasema wanapuliza dawa kila wiki ila wanarudi. Kuna kaka mwingine alijibu kijeuri akasema gari hainununiliwi na kunguni bali mnakuja nao nyie abiria
 
MABASI MENGI SANA HASA YA SAFAR NDEFU YANA KUNGUNI,M NILIPANDA CITY BOY YA KARAGWE KWENDA BUKOBA BAC LINA KUNGUNI WAKUTOSHA.
TABOA inabidi waliangalie na hili..
 
Kweli kabisa hizo gari zina kunguni. Tuliwapouliza muhudumu akasema wanapuliza dawa kila wiki ila wanarudi. Kuna kaka mwingine alijibu kijeuri akasema gari hainununiliwi na kunguni bali mnakuja nao nyie abiria
Wafanyakazi wengine jeuri utadhani "bwana yule" yaani wana lugha chafu hata Tajiri yao hayuko hivyo !!
 
Back
Top Bottom