Basi la Kampuni ya Vitu Line lapata ajali Iringa

yingamale

JF-Expert Member
Jan 5, 2017
223
222
Basi hili linafanya safari kutoka Wilaya ya Kilolo vijijini huko Lulanzi kuja Iringa mjini kila siku na kurudi.

Yani basi limetoka huko masafa marefu tena katika njia mbaya sana zenye utelezi na mvua isiyokwisha,lkn ajabu linakuja kudondoka linapoingia mjin!! Vifo na majeruhi ni wengi.

Eeeh Mwenyezi Mungu zilaze Roho za marehem pema peponi na uwajaalie majeruhi wote kupona haraka,Amen
16298799_761011010714591_7151088975798540929_n.jpg



16265427_761011177381241_1124033004025617737_n.jpg


16143107_761011364047889_6320000915001986829_n.jpg


=====

MTU mmoja amefariki dunia katika ajali ya basi la kampuni ya Vitu Line lenye namba za usajili T910 linalofanya safari zake kati ya Lulanzi Kilolo na Iringa Mjini baada ya kuligonga lori lenye namba T724 AVV scania lililokuwa limebeba Mbao.

Ajali hiyo imetokea asubuhi leo hii eneo la Tagamenda Mjini Iringa wakati basi hilo likitokea Kilolo kwenda Iringa mjini na kuelekea mwelekeo wa Lori hilo.

Chanzo kimeelezwa ni mwendo kasi wa basi hilo. Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amefika eneo La tukio pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama.
 
ajali zilisimama kwa muda,
naomba uhakiki uendelee ajali zitaisha, maana kipindi cha uhakiki sikusikia ajali kama hizi mara iringa mara mikese lol!!
 
Huku mikoani kwetu kuna changamoto kubwa sana ya usafiri. Ubora wa miundombinu pamoja na vyombo vyenyewe vya usafiri ni jambo la kuangaliwa kwa jicho la tatu na kuchukuliwa hatua na mamlaka husika. RIP wapendwa waliopoteza uhai kwenye ajali hii na majeruhi waugue pole!
 
Majina ya haya mabasi mengine yanashangaza, kama vile ni lazima watumie ili wafaidike kivileeee. Yaani yale yale masharti wanayopewa

R.I.P
 
umri wa basi unazidi wa dereva! sijui vipuri vinapatikana wapi? au wanakazia kamba bora injini izunguke. poleni sana wafiwa. majeruhi nawatakia uponyaji wa haraka.
 
Hili basi lilipigwa karantini kuingia mjini Iringa. Alichokifanya akaenda kubadilisha board, wanaliangalia tu, linadunda, vyombo husika vijitatmini kama vinatosha kuwatumikia wananchi wa Tanzania
 
Back
Top Bottom