Basi la kampuni ya AM lapata ajali, watatu wajeruhiwa

Basi la kampuni ya AM lapata ajali, watatu wajeruhiwa

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
Serengeti. Basi la Kampuni ya AM lililokuwa linatoka Mugumu Serengeti kwenda Mwanza limepata ajali katika Kijiji cha Bokore wilayani hapa na kujeruhi watu watatu.

Basi hilo lilikuwa na abiria zaidi ya kumi.

Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana Alhamisi alfajiri ya saa 12.35 na kwamba wanamshikilia dereva kwa mahojiano.

Mganga mkuu wa Hospitali teule ya wilaya, Emiliana Donald amethibitisha kumpokea majeruhi mmoja aliyemtaja kwa jina la Sosoni Philipo mkazi wa wilayani Serengeti.

Amesema majeruhi huyo alikuwa analalamika kupata maumivu sehemu ya mgongo na kuwa wanaendelea na tiba.

Hata hivyo, majeruhi wengine wametibiwa katika zahanati za watu binafsi na kuendelea na safari zao.

Chanzo: Mwananchi
 
Poleni sana wana mugumu serengeti....ila kinachonishangaza ni basi kuwa na abiria kumi.Au ilikuwa hiace??
 
Poleni sana wana mugumu serengeti....ila kinachonishangaza ni basi kuwa na abiria kumi.Au ilikuwa hiace??
JPM kakaza kila mahali, kila mtu, kila kampuni wanaisoma taraaaaaaaaaaaatibu! hii inaonyesha hata zile safari za bila ulazima siku hizi hazipo tena! hahahahah. Good afternoon Perfecttz
 
JPM kakaza kila mahali, kila mtu, kila kampuni wanaisoma taraaaaaaaaaaaatibu! hii inaonyesha hata zile safari za bila ulazima siku hizi hazipo tena! hahahahah. Good afternoon Perfecttz
Hakika mkuu hata mimi nimeona hvy asee.Manake basi kuwa na watu kumi ndani halafu basi kubwa la mkoa hadi mkoa hii ni hatar sana
 
Hakika mkuu hata mimi nimeona hvy asee.Manake basi kuwa na watu kumi ndani halafu basi kubwa la mkoa hadi mkoa hii ni hatar sana
Si ajabu hadi kupata ajali alikuwa anafukuzana na wenzake ili kuwahi abiria wa sehemu za mbele ya safari yake
 
Back
Top Bottom