kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
MKUU wa Shule ya Sekondari ya Ismila katika wilaya ya Iringa Vijijini, Pangras Msasamela, amekufa papo hapo na watu wengine zaidi ya 40 kunusurika kifo baada ya basi la Hekima lenye namba za usajili T 399AVU linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mbeya kugongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba T 746 AKU Toyota Mark II.
Watu wengine watatu walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo iliyotokea jana majira ya saa 4 usiku katika eneo la Kibwabwa Manispaa ya Iringa, wakati basi hilo likiwa safarini kuelekea mkoani Mbeya.
Abiria walionusurika walimweleza mwandishi wa habari hizi aliyefika eneo la tukio kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari hiyo ndogo kulihamishia gari upande wake na kutaka kukatisha upande wa kulia bila kulitazama basi hilo lililokuwa mbele.
"Kweli dereva wa basi amefanya jitihada kubwa sana za kuokoa maisha ya sisi abiria tuliokuwemo ndani ya basi hili ...kwani kama dereva angelikuwa mzembe katika basi hili letu hakuna mtu ambaye angetoka mzima ....ujue basi lilikuwa likielekea kupinduka kabisa," alisema Kevin Mwakasumile mmoja wa abiria aliyenusurika katika ajali hiyo.
Abiria wengi walionusurika katika ajali hiyo walipata michubuko midogo midogo baada ya kukanyagana ndani ya basi hilo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa mtu mmoja ndiye aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
http://4.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TRIQKteVgiI/AAAAAAAAOxY/2n-8hajCgCo/s1600/IMG_8787.JPG
http://1.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TRIQKfPvD4I/AAAAAAAAOxQ/uzj0XgrgceA/s1600/IMG_8795.JPG
http://4.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TRIQKAHjWcI/AAAAAAAAOxI/zk69b4W5KUw/s1600/IMG_8799.JPG
http://2.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TRIPVAgFWTI/AAAAAAAAOwY/FDKc0dpxSOQ/s1600/IMG_8780.JPG
http://1.bp.blogspot.com/_YaKHJFAZ_oc/TRIPVnpShKI/AAAAAAAAOww/m3X-SA85Bc4/s1600/IMG_8802.JPG