Basi la Dar-Songea ILYANA: Konda na Dereva wamshusha abiria njiani kwa nguvu

herikipaji

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
1,198
1,345
Abiria aliyepanda Ilyana Bus no. T202 B.. kutoka Dar es salaam kuelekea Songea leo tarehe 9 Oct. 2016 ambaye konda na dereva wa basi hili mmemshusha njiani kwa nguvu usiku huu amepotea. Abiria alipokata ticket Ubungo tarehe 8 Oct. 2016 alielekeza kituo anachoteremka na mkamkubalia kwani kituo halali na kinafahamika lakini Basi lilipofika mkakataa kusimama na mkamshusha porini mmefanya jinai kinyume na kanuni na sheria za Sumatra.

Abiria wa Dar to Songea kuweni makini hili basi la ILYANA lina huduma mbovu sana na halifai kwa usafiri.
Dereva na konda mna kesi ya kujibu.
 
Amepoteaje wakati uko naye.
Umpoteze wewe kwa malengo yako binafsi.
Kama wenzio wana kesi ya kujibu basi wewe umejipalilia mkaa kichwani.
Ni bahati njema nimemuona na nalazimika kumsaidia kwa usalama wake kwani sasa usiku na ni hatari sana. Yuko kwenye mikono salama sasa. Lakini hilo basi inaonekana ni mazoea yao kufanya unyama kama huo je angekutana na watu wenye nia ovu unafikiri ingekuaje?
 
Abiria aliyepanda Ilyana Bus no. T202 B.. kutoka Dar es salaam kuelekea Songea leo tarehe 9 Oct. 2016 ambaye konda na dereva wa basi hili mmemshusha njiani kwa nguvu usiku huu amepotea. Abiria alipokata ticket Ubungo tarehe 8 Oct. 2016 alielekeza kituo anachoteremka na mkamkubalia kwani kituo halali na kinafahamika lakini Basi lilipofika mkakataa kusimama na mkamshusha porini mmefanya jinai kinyume na kanuni na sheria za Sumatra.

Abiria wa Dar to Songea kuweni makini hili basi la ILYANA lina huduma mbovu sana na halifai kwa usafiri.
Dereva na konda mna kesi ya kujibu.

Na hapo aliposhishiwa kuna ' Simba ' na akina ' Scorpion ' wengi tumwombee tu kwa Mwenyezi Mungu.
 
Tatizo la Jf watu hufanya masihara hata kwa mambo ambayo yana gusa na kuumiza kama haya.
Kwanza nikupe pongezi kwa moyo wa ukarimu na wema ulio mtendea abiria huyo (alie potea).
Pili nasema asante kwa kutoa taarifa na tahadhari ili abiria wengine waweze chukua tahadhari kwa watajwa hao.
Tatu naomba kabla ya kumpa hifadhi huyo abiria, nivema ukatoa taarifa kituo cha polisi kilichopo karibu na ikiwezekana wenye bus waweze chukuliwa hatua kwa kosa la jinai.
 
Kwahiyo walivyogoma kukushusha pale kwenye kituo cha daladala ukaamua kuja kuanzisha uzi huku...
Mie nimemuona huyo abiria aliposhushwa hapajui na anahangaika kituo walichokataa kumshusha ni halali na kikubwa kinafahamika na alipokata tiketi aliwaeleza na wakakubali kama ni kituo cha daladala kwanini hawakumkatalia alipokata tiketi?
 
Tatizo la Jf watu hufanya masihara hata kwa mambo ambayo yana gusa na kuumiza kama haya.
Kwanza nikupe pongezi kwa moyo wa ukarimu na wema ulio mtendea abiria huyo (alie potea).
Pili nasema asante kwa kutoa taarifa na tahadhari ili abiria wengine waweze chukua tahadhari kwa watajwa hao.
Tatu naomba kabla ya kumpa hifadhi huyo abiria, nivema ukatoa taarifa kituo cha polisi kilichopo karibu na ikiwezekana wenye bus waweze chukuliwa hatua kwa kosa la jinai.
Asante ndugu na ushauri wako tumeupokea.
 
Ni bahati njema nimemuona na nalazimika kumsaidia kwa usalama wake kwani sasa usiku na ni hatari sana. Yuko kwenye mikono salama sasa. Lakini hilo basi inaonekana ni mazoea yao kufanya unyama kama huo je angekutana na watu wenye nia ovu unafikiri ingekuaje?
Bosi kwa ulichoandika hapa inabidi edit post yako ya kwanza kwa kujazilia nyama kutoka kwenye ujumbe wako huu nilio quote

Kwamba jamaa hajapotea ila kashushwa sehemu asioijua na ni usiku sana na ni hatari na maisha yake

Halafu waombe Mods wakufanyie mabadiliko kwenye heading ya mada yako... kuwa jamaa hajapotea
 
  • Thanks
Reactions: y-n

Mada imejitosholeza unataka ni edit ili iweje? Hivi ungekuwa umefanyiwa wewe hivyo ungeiskiaje? Unaona walichofanya ni utu kweli mkuu?
 
Back
Top Bottom