Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,034
- 63,184
Ndugu Bashiru;
Wewe ni katibu mkuu wa chama cha mapinduzi.Wewe ni Muislamu uliyelelewa kiislamu katika familia yenye maadili ya kiislamu.Unalo jukumu kama Katibu Mkuu kuunganisha na si kutenganisha
Unalo jukumu la kulinda heshima ya kila mwanachama wa chama cha mapinduzi na hupaswi kutumia lugha zisizo na staha si tu kwa mtu yeyote bali watu waliokuzidi umri
Ndugu Bashiru, wewe umeachiwa chama na mtangulizi wako mheshimiwa Kinana, of all the people wewe siyo mtu wa kumuita mzee Kinana Mpumbavu PUBLICLY kila mtu akisikia!. Hayo maneno yako ni makali sana ndugu Bashiru, hebu kaa kitako, yafikirie maneno yako kisha uone kama umetenda sahihi!.
Ndugu Bashiru si vizuri kutumia Clip zilizodukuliwa na kuachiwa kinyume cha sheria kubase judgement yako ya kutukana mtu!
Kama kweli ulikuwa unakusudia kugusia waraka wa wazee wetu ndugu Kinana na Mzee Makamba ungejikita katika waraka ambao umeachiwa kwenye vyombo vya habari badala ya clip za mazungumzo private ya watu wawili.
Ndugu Bashiru, Mzee Makamba ni Mtu mwnye umri mkubwa sana kukuzidi, hebu Jiweke kwenye viatu vyako kumuita mpumbavu.
Ndugu Bashiru, hata kama wazee wetu wametenda kosa, si vipo vikao vya nidhamu vya chama ambavyo wewe ni miongoni mwa wasimamizi wakuu, vipi uanze kutumia lugha mbaya na za ukakasi namna hiyo?
Ndugu Bashiru,hivi umeshindwa hata kidogo kusemea maneno ya kashfa na ya kejeli ambayo ndugu Musiba amekuwa akiwashutumu hawa wazee, kweli huoni uchokozi dhidi ya hawa wazee ila tu umeona stahiki yao ni kuwaita Wapumbavu?
Kweli leo Katibu mkuu anawaita Makatibu wakuu wa chama chake wastaafu ambao ni victims wa kutukanwa kila mara, watu waliotukanwa na mwanaharakati ambaye ameachwa atambe, kisha wakadukuliwa, na udukuzi huo ukatumika kisiasa dhidi yao, Leo hao wazee kweli unawaita Wapumbavu?
Ndugu Bashiru rudisha moyo nyuma na uombe radhi.Ulichokifanya siyo maadili ya Kitanzania. Siyo maadili ya Kiislamu
Na certainly siyo maadili yanayompasa katibu mkuu