Bashe: Spika Ndugai gombea tena ubunge 2025

Mwana wa Nuru

JF-Expert Member
Dec 3, 2012
519
500
Kongwa. Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kubadili uamuzi wake wa kutogombea tena ubunge wa Kongwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Bashe ametoa kauli hiyo jana jioni Oktoba 11, 2021 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa korosho wa wilaya za Mpwapwa, Kongwa na Manyoni.

Mkutano huo ulifanyika katika Chuo cha Veta Kongwa na Spika Ndugai alikuwa Mwenyekiti aliyeongoza majadiliano ambayo yalianza saa 4 asubuhi- hadi saa 12 jioni.

Bashe amesema mipango mizuri ambayo imeanzishwa na Ndugai haipaswi kubezwa na kuwa akija mwingine huenda asiendeleze kwani kila mmoja ana mipango yake.

"Nilisoma kwenye mitandao kuwa ukitaka kustaafu na Rais John Magufuli, lakini Mungu ana mipango na makusudi yake, leo tuko na Samia Suluhu Hassan ambaye tunakwenda naye hadi 2030, naomba ufikiri namna ya kubadili uamuzi wako," amesema Bashe.

Naibu Waziri amesema itakuwa na maana kama Ndugai atakubaliana na wazo hilo ambalo litampeleka kukamilisha ndoto za watu wa Kongwa hasa kwenye dhahabu ya kijani ambayo ni korosho.
Kauli ya Bashe iliibua shangwe kutoka kwa washiriki wa kongamano hilo ingawa Ndugai mwenyewe hakujibu kitu wakati watu walipokuwa wanapiga makofi.

Katika hatua nyingine, Bashe amesema serikali itahakikisha inakamilisha mipango yake ili wakulima wa Kongwa, Mpwapwa na Manyoni wanufaike na Kilimo hicho.

Ameahidi serikali inakwenda kujenga kiwanda cha kubangulis korosho katika kijiji cha Mbande ili wakulima wavune na kubangua korosho zao hapo.
W
 

Prince Kunta

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
19,080
2,000
Hapo Bashe katumwa kupima upepo kwanza kisha mbilikimo wa Kongwa atakuja kutengua kauli ya kustaafu 2025 kupitia press conference
 

UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,066
2,000
Bashe jamani umekuwa mzee ghafla kwa kuona wazeee waendelee badala ya kushauri damu changa ,vijana wagombee jamani mtu kawa mbuge wa same jimbo kwa miaka karibu 20 jamani pumzika.
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
36,097
2,000
Bashe kawa kama mento,badala ya kuangalia maslahi ya wana Kongwa yeye anaangalia tumbo la mtu mmoja. Ama kweli CCM hawaaminiki,Bashe alikuwa mtu makini sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom