Bashe atumika kutoa rushwa Nzega - Takukuru mpo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bashe atumika kutoa rushwa Nzega - Takukuru mpo?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Sep 25, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bashe afichua hatari zinazoikabili CCM Nzega
  Na Lucas Macha  25th September 2010  [​IMG]
  Hussein Bashe.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wenyekiti, makatibu kata na matawi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya ya Nzega mkoani hapa, wamesusa kushiriki kampeni za Uchaguzi Mkuu wa jimbo la Nzega.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hatua inatokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hatua yao ya kumuunga mkono mshindi wa kura za maoni aliyekuwa na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, Hussein Bashe.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kauli hiyo ilitolewa na Bashe katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Tabora, uliofanyika Nzega jana.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Bashe alisema baadhi ya wenyeviti na makatibu wa kata na matawi, walimueleza kuwa baadhi ya viongozi wa CCM katika ngazi za mkoa na wilaya, waliwatishia kuwa waliomuunga mkono (Bashe) wataangushwa katika uchaguzi huo. Alisema kutokana na mazingira ya vitisho hivyo, baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Nzega, akiwemo Katibu wake Hilda Kapaya wanaishi kwa hofu.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Hali ya kisiasa katika chama wilaya ya Nzega ni mbaya kwa sasa…watendaji wa chama wanaishi kwa taabu kutokana na watu wachache walionipigia majungu na fitina taifani….nasema nitapambana nao kwa maslahi ya chama na siyo ya kwao,” alisema.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Bashe alisema hana kinyongo na tukio lolote linalohusiana na mchakato wa kura za maoni, lakini anaamini kuwa baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Tabora walishiriki kummaliza ili asigombee ubunge.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Kulikuwa na viongozi walioshiriki kunimaliza na vikao vyote vilifanyika mkoani…..lakini mimi sina kinyongo wala kutogombea ubunge hakunipi homa,” alisema.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema anajivunia kuwa mwanachama wa CCM na kwamba hana mpango wa kujiunga upinzani licha ya kuwepo shinikizo la kumtaka afanye hivyo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema hakuingia katika siasa kwa kubahatisha, bali anaijua nyanja hiyo kwa vile ni raia halali wa Tanzania.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kauli ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa Taifa, John Chiligati, kuwa kutokana na utata wa uraia wake (Bashe), alivuliwa uanachama na nyadhifa alizokuwa nazo, ilikuwa yake binafsi (Chiligati) na si CCM.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema Chiligati hakuwa na mamlaka ya kisheria kutamka maneno hayo.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Narudia tena hii ni hatari watu ama kikundi cha watu wanakutanikia ofisi ya CCM mkoa na kupanga kuwa Bashe siyo raia bali msomali hivyo hana sifa… hii ni hatari sana kwa mustakabali mwa Taifa,” alisema.Hata hivyo Bashe alisema atashiriki zaidi kwenye kampeni ili wagombea udiwani, mbunge na rais kupitia CCM waibuke na ushindi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo Bashe aliahidi kuendelea kuchangia maendeleo hasa kwa maeneo aliyowahi kuwaahidi wakazi wa Nzega. Alitumia mwanya huo kugawa baiskeli 152 kwa wenye viti wa matawi na pikipiki 21 kwa kila kata jimboni humo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande wake, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Rotam Aziz, alisema mambo yaliyotokea dhidi ya Bashe yamepita na kwamba ilikuwa `ajali ya kisiasa’.[/FONT]
  CHANZO: NIPASHE


  0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
   
 2. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135


  Kutoa baiskeli 152 na pikipiki 21 ni rushwa, I bet my testicles that the money to get these motorcycles is not Bashe's.... will this help???
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Bashe bado ni msomali na analamba miguu ya bwana wakubwa wake akiogopa wasimsulubu. Hakuna jingine kabisa hizi zingine ni porojo porojo tu.
  We Bashe sikiliza dogo, hakuna kitu kinaitwa ajali ya kisiasa. Wewe endelea kutumika tu kama kanda mbili wakupeleke ****** na bafuni kisha wanakuacha nje mlangoni wakati wao wanaingia ndani vyumbani mwao. Hao ndio sisi m ya kina Rostam.

  Anyway tarehe 31.10 twatoa hukumu kwa sisi m na Dr Slaa atakuwa rais wa awamu ya tano na tutafuatilia issues zote na kama walikusingizia tutawatia hatiani kwa kukuvunjia heshima na kama itadhihirika wewe ni msomali itabidi uanze taratibu za kujiandikisha utanzania wa kukopa.

  CHAGUA DR SLAA CHAGUA CHADEMA
   
 4. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nimepiga hesabu ya haraka haraka hizo baiskeli 152 na pikipiki 21 jumla ni kama Tshs. 33,160,000/=, Nakuunga mkono mkuu, Bashe kwa furaha gani hasa atoe pesa yote hiyo? sina uhakika na kipato chake halali lakini haingii akilini kwamba hiyo ni hela yake kaamua kusaidia tu. Huyo atakuwa ametumwa tu ili kupunguza hasira za wana Nzega ambao walikuwa waelekee kuitosa CCM na Kigwangala wao.
   
Loading...