Basena awatema Boban, Chuji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Basena awatema Boban, Chuji

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by kilimasera, May 22, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KOCHA wa Simba, Mosses Basena amewachuja Haruna Moshi, Athuman Idd pamoja na wachezaji wote wasiokuwa na leseni za CAF kwenye safari ya Zanzibar, huku kipa wa kimataifa wa Kenya, Willis Ochieng jana asubuhi akifanya mazoezi na klabu hiyo inayotaka kumsajili msimu huu.

  Kikosi cha Simba jana mchana kilianza safari ya kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya siku tano ya maandalizi yao ya mechi ya kuwania kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca Mei 28.

  Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kikosi cha Simba kilichoondoka jana kilikuwa na wachezaji wale ambao walikuwa kwenye usajili uliokwenda CAF baada ya kocha Basena kuomba wafanye hivyo.

  Uamuzi huo wa kocha Bassena unawafanya maswahiba wawili Haruna Moshi 'Boban' na Athuman Idd 'Chuji' walioteka macho ya wengi tangu waliporejea kwenye kikosi cha Simba wiki hii kuendelea kubaki jijini hapa.

  Chuji msimu uliopita alikuwa akiichezea Yanga, wakati rafiki yake Boban yeye alikuwa amefungiwa kutokana na uamuzi wake wa kuvunja mkataba na klabu ya Gelfe IF ya Sweden.

  ''Wachezaji wote ameondoka isipokuwa wale wapya ambao majina yao hayapo CAF na tumefanya hivyo kutokana na kocha mwenyewe kuwataka hao tu atakaowatumia ili aweze kujua kikosi chake kimeiva kiasi gani kuliko kuwa na watu ambao hawatamsaidia katika mchezo huo wa Jumamosi,'' alisema Mtawala.

  Hata hivyo Mtawala alisema timu hiyo itarejea Dar es Salaam, Jumatano kwa ajili ya safari yao ya Alhamisi kwenda jijini Cairo, Misri tayari kwa mchezo huo utakaochezwa Jumamosi saa 12:00 jioni.

  Alisema wachezaji hao wataungana na wenzao baada ya mchezo wa Wydad kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame inayoanza kutimua vumbi Juni 21 nchini Sudan.

  Kocha Basena amesema haitaji mechi yoyote ya kirafiki na kwamba anajikita kuwatengeneza wachezaji kisaikolojia ili waweze kufanya vizuri kwenye mechi yao na Wyadad Casablanca ya Morocco.

  Basena alisema hayo kwenye mazoezi ya timu yake kwenye uwanja wa Taifa na kusema kuwa hataki mechi yoyote ya kirafiki kwa vile anahofia majeruhi wakati wana mechi ngumu mbele yao.

  "Sidhani kama huu ni muda muafaka wa kucheza mechi ya kirafiki, sidhani pia kama mazoezi ninayowapa yanatosha kufanya vizuri kwenye mechi yetu na Wydad, ninachoweza kusema kwa sasa nawakazania zaidi kuwatengeneza kiakili 'Saikolojia' ili warudi mchezoni,"alisema Basena.

  "Naweza kucheza mechi ya kirafiki halafu wachezaji wangu wakaumia, itakuwa ni doa tayari kwenye timu, muda wenyewe wa kufanya maandalizi ni finyu cha muhimu ni kuwakazania kuwajenga kisaikolojia warudi mchezoni,"alisema Basena.

  "Akili zao walishajenga wameondolewa kwenye mashindano, lakini bahati wamerudishwa tena mashindanoni, nafikiri tutacheza vizuri na Wyadad, nitajitaidi kwa nguvu zangu zote kurudisha morali ya wachezaji wangu wajue wana kibarua kigumu mbele yao, kama ni gari basi tumeshakimbia asilimia 50 kwa muda mfupi niliokaa na wachezaji nimegundua wana vipaji sana, cha muhimu wawe makini wajitahidi wacheze mpira wa hali ya juu ili waweze kusonga mbele kwenye mashindano.

  Wakati huohuo; Kipa wa kimataifa wa Kenya, Willis Ochieng amewasili nchini na kuanza mazoezi na Simba inayotarajiwa kufanikisha usajili wake wiki hii. Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana Ochieng alisema kuwa alifurahia kufanya mazoezi na kikosi hicho cha Simba na pia matumaini yake ni kwamba Simba watavutiwa naye na kumsajili.

  "Nashukuru nimefika salama, nimefurahi kufanya mazoezi ya pamoja na wenyeji wangu na ni matumaini yangu watavutiwa na mimi na hatimaye nitasaini mkataba wa kuichezea Simba,"alisema Ochieng.

  Kuhusu mazungumzo kati yake na viongozi wa Simba, Ochieng aliyemaliza mkataba wake Novemba mwaka jana katika klabu ya IFK Mariehamn ya nchini Finland alisema alitarajia kukutana nao jana jioni kwa ajili ya kuweka sawa mpango wa kuichezea klabu hiyo.

  Mbali ya IFK, Ochieng pia amewahi kuzichezea klabu ya Mumias Sugar ya nchini Kenya pamoja na Free State ya Afrika Kusini.
   
 2. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa siyo mahala pake mkuu.Ondoa hiyo thread
   
Loading...