BASATA wawafikirie viziwi kwenye tungo za muziki na filamu

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Wiki iliyopita kuna filamu moja niliangalia, ilikuwa na ujumbe mzuri sana wa kujenga nchi, lakini leo kuna wimbo mmoja wa muziki nimesikiliza na kuuangalia ulikuwa na ujumbe mzuri sana kwa msikilizaji na mtazamaji.
Lakini ghafla mawazo yangu yakawafikiria sana viziwi. Je ujumbe wa filamu na muziki ule uliwafikia viziwi? Sidhani kwani haukuwa na mtafasiri wa lugha ya alama.

Hapo nikaanza kujiuliza ni kwa jinsi gani hili kundi maalum linanyimwa haki yake ya kupewa taarifa na habari zihusuzo jamii yao na nchi yao.
Nikawaza labda BASATA wanaweza kuweka kipengele cha kulazimisha wasanii kila filamu na wimbo uwe na ukalimani kwa wa lugha ya alama ili kuwapa burdani na elimu zitokanazo na filamu na muziki walemavu hawa wa kusikia.
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo nayo inaweza kuweka utaratibu maalum wa kisera na kisheria ambao utatoa mwongozo kwenye jambo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtazamo wangu naona Bora serikali ungetilia mkazo juu ya elimu ya kupambana na Corona Kwa watu wenye UHITAJI MAALUMU.
Kundi hili linahitaji kupewa kipaumbele Kwenye gonjwa hili na namna ya kujilinda kuliko huo UJINGA uliopo Kwenye nyimbo na filamu ..

Kuna haja gani ya watu wenye UHITAJI MAALUMU kupewa tafsiri ya miziki hii inayosifia NGONO,POMBE NA UMALAYA?
 
Viziwi.......sawa, Je Vipofu na Bubu itakuaje?

Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS
 
Back
Top Bottom