Basata katika kashfa nzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Basata katika kashfa nzito

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mizizi, Jul 13, 2010.

 1. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuna uwezekano mkubwa sana Balaza la sanaa Tanzania kuingia katika Mgogoro mkubwa na kuliingiza Taifa katika hasara Kubwa.

  Si hivyo tu, pia Image ya Tanzania inaweza kuingia doa kwa Uzembe ama kutokuwa makini kwa watu wachache ambao waliopewa mamlaka.

  hii ni kutoka na sakata la Mafia Dance Festival. hili ni tamasha ambalo lilitarajiwa kufanyika Kule kisiwani Mafia kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 15 Augost mwaka huu. Tamasha hilo lilitarajiwa kuhusisha wageni zaidi ya 3000 kutoka barani Ulaya, vikiwemo vikundi mbali mbali kutoka tanzania na nje ya nchi. kidogo unaweza kufananisha na Jahazi Festivals kule zanzibar.

  Basata walitoa kibali kwa waandaaji, waandaaji wakafanya maandalizi yote, yakiwemo yale ya kuuza ticketi na kuingia mikataba na mashirika mbali mbali ya kutoa huduma za usafiri na mengineyo.

  Baadhi ya waliotarajia kufika kuhudhuria tamasha hilo wengi lishafanya malipo ya ticket za ndege kutoka ulaya na kufanya booking za hoteli Tanzania na kule Mafia.

  Mwisho wa siku, kutokana na presha kutoka kwa wamiliki wa hoteli wachache kule Mafia, waliona tamasha hili halina manufaa kwao, na linaweza kuthreat biashara zao, wakaamua kupitisha mlungula kwa viongozi wa wilaya, zaidi mkuu wa wilaya ya mafia, na hivyo akashawishi tamasha lisifanyike Mafia. cha kushangaza, basata, waka revoke kibali walichokitoa kwa waandaaji hawa,

  sasa waandaaji, wanampango kabambe wa kuifikisha Basata katika vyombo vya kisheria vya kimataifa, na kudai fidia kutokana na hasara zilizotokana na maamuzi yao
  Zaidi tembelea MafiaDanceFestival
   
 2. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna gazeti niliwahi kusoma kuna makala mtu aliandika kutoka Mafia kuhusu tamasha hili na kuhusisha na ushoga, hivyo akasema tamasha hili linakuja na mashoga, pia alisema litachafua mazingira akiwa na maana ya maadili kutokana na mashoga watakaokuja na pia uchafu wa mazingira kutokana na uchafu watakaoacha hao watu 3,000.- kutokana na maandalizi duni kama vyoo, nk. kutokana na udogo wa kisiwa chenyewe kuweza kuhudumia watu 3,000.- sikumbuki nilisoma wapi lakini aliorodhesha vitu vingi kama vilitizamwa tena huenda ndio sababu walisitisha tamasha hilo.
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  BASATA waende course ya event management. Kama wanatoa tu vibali bila kuzingatia mambo muhimu ni tatizo. Je, mtu anatoka mbali utajuaje kama ni shoga kama hajajitambulisha hivyo?
   
 4. m

  matejoo Member

  #4
  Jul 14, 2010
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada mbona unakuwa biased kiasi hicho? Huelezi hata kidogo sababu za BASATA kufanya hiyo revocation? Hayo mambo ya Ushoga wewe hukusikia? Malalamiko ya uharibifu wa mazingira hukuwahi kusikia pia? Just make a balanced presentation my friend na watu watachangia kwa uhuru.
   
 5. w

  wasp JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wacha sheria ichukue mkondo wake na watayarishaji wa tamasha waifilisi nchi hili wenye nchi wapate akili ya kuajiri watu weledi. Angalizo: Rada ilikula kwetu ingawa yule mama wa kidhungu (Clare Short) pale London alipiga kelele akiwaonea huruma watanganyika maskini mpaka akafika ikulu Dodoma lakini wapi tuliishia kuambiwa sisi ni wavivu wa kufikiri.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Woga wa nini? Acha washitaki na basata wakishindwa walipe ndo itakuwa fundisho.
   
Loading...