Glasnost
JF-Expert Member
- May 18, 2017
- 266
- 259
Hivi karibuni Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bwn. Mngereza alitoa kauli na onyo kwa wasanii wa kizazi kipya kuwa waangalifu na kufuata sheria za nchi bila kukiuka maadili ya kitanzania. Hii ni baada ya wasanii Jux na Vanessa Mdee wakiwa Mwanza katika tamasha muziki la usiku kupigana denda kwenye steji.
Namnukuu, “Sijui ni shetani gani amewaingia hawa vijana wanamuziki maana kila siku wanaonesha vitu vya ajabu visivyokuwa na maadili wanapokuwa jukwaani”, mwisho wa kunukuu.
Inachekesha na kusikitisha kiongozi aliyeaminiwa kuwa na akili timamu na uwezo wa kufanya kazi bila ubinafsi,chuki kusema kwamba kunyonyana ndimi hadharani ni kosa. Yaani kiongozi tena mkuu wa taasisi unaimbia jamii ya watanzania kuwa kulana denda ni kosa na kwa sheria ipi?
Ni wakati sasa hawa viongozi wajue mipaka yao na ufahamu kwa maana ya kutambua tofauti kati ya maoni, maamuzi na uhalisia wa jambo, kutenganisha hisia, tabia na kazi, sio jambo unacholichukia au kutopendezwa nalo ni kosa kwa sababu tu wewe hupendi au una madaraka ya kufanya utakacho.
Suala la uvumilivu ni muhimu sana hata kama kwako sio kitu au jambo linalokupendeza tena kwenye vitu vidogo kama watu kupigana mabusu au kulana ndimi hadharani. Sasa baadhi ya viongozi wanaingilia uhuru wa mtu wa jinsi ya kuvaa, kutembea, kunyoa na hata jinsi ya kuzungumza.
Si mda mrefu sana tuliona baadhi ya wasanii nyimbo zao zikifungiwa na TCRA na kuitwa na Basata kueleza kwanini wanapotosha jamii na kuvunja “maadili ya kitanzania”. Nyimbo kama Bongo bahati mbaya ya Young D au Nampa papa ya Gigy Money sikuona ubaya wake. Hivi unaposema “papa” ni tusi kwa kutumia kamusi gani? Au Bongo bahati mbaya una maudhui mabaya, ni yapi hayo? Maana wimbo wa Young D kwa tafsiri ya chap chap ni wimbo wenye maisha ya vijana wengi wa vijiweni waliokata tamaa na wenye ndoto za kusaka maisha nje ya Tanzania. Uzuri wa wimbo huu ni uko very comical na unaelezea kilichopo nchini kwetu, so what’s wrong with that?
Kwa miaka mingi sasa Tanzania imekuwa na viongozi na wadau mbalimbali wenye upeo mdogo au ukosefu wa maarifa juu ya nini maana ya utamaduni. Utamaduni ambao wengi uuzungumzia ni ule utamaduni wa kidini na sio wa makabila japo kuwa nchi hii haina dini lakini watu wana dini na “wadini kwelikweli”. Mafundisho ya dini na aina ya maisha wanayoishi ndio yamekuwa sababu za msingi kupinga kile wanachoona hakifai bila kujua au kwa makusudi kutojali kwamba nchi hii haina dini na uhuru wa mtu kukandamizwa ni kosa na dhulma.
Wanazungumzia maadili yanayovunjwa, wakati tuna makabila zaidi ya mia moja yasiyofanana kwa mambo mengi tu ya msingi. Imefika wakati tuambiane ukweli kuwa hii nchi haina dini na maamuzi ya kidini yapingwe na yasiwe sheria/amri. Pia sheria za uvunjifu wa maadili ni za kutazamwa upya maana zimekaa kidini na sio kiuhalisia kutokana na mazingira yenyewe.