ndugu yako
Senior Member
- Mar 30, 2013
- 193
- 96
Mheshimiwa Rais!
Shikamoo.
kwanza pole kwa majukumu mbalimbali uliyonayo juu ya ujenzi wa taifa hili.
Naandika barua hii nikijua fika kuwa kwa sasa umetingwa na majukumu mazito kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu; uundwaji upya wa baraza lako la mawaziri na kuteuwa wajumbe wa bunge la katiba ni majukumu makubwa sana na kutokana na majukumu haya hupaswi kusumbuliwa na mambo mengine ambayo yanaweza kukutoa katika mstari sahihi wa fikra zako juu ya hatma ya Tanzania yetu!
Lakini mheshimiwa rais wewe ni baba yetu! haijalishi una majukumu makubwa kiasi gani pindi tunapopatwa na matatizo ni lazima tukuambie wewe hata kama ukiamua kujifungia chumbani peke yako na kuacha maagizo kuwa usisumbuliwe na mtu yeyote kwa sababu kuna kazi ya msingi unafanya itatuladhimu kukusubili tu hata kama ni saa nane usiku itabidi tukuambie!
Mheshimiwa rais. Mimi ni kijana niliyemaliza masomo yangu ya shahada ya kwanza mwaka jana katika chuo kikuu kimojawapo hapa nchini! Kama vijana waliowengi nilikuwa na ndoto na mategemeo mengi tu ambayo nikiamua kuyaandika hapa unawezadhani sina akili timamu lakini yote hayo yalikuwa ni ndoto tu!
Mheshimiwa rais! Ajira ndani ya Tanzania hii ni ngumu sana! Japo nina muda mchache sana mtaani ila nimeishaona mazingira ya kuniogopesha! mheshimiwa rais inaogopesha sana pale unapomkuta mtu aliyemaliza chuo mwaka 2010 akiwa bado mtaani anatafuta ajira wakati huo huo wakina sisi tuliomaliza chuo 2011, 2012 na 2013 bado tuna joto la kuzunguka na CV zetu mtaani! huku tukitegemea tena kuongezeka idadi mwezi wa 6 mwishoni mwaka huu!
Mheshimiwa rais! ninaweza kuonekana mzembe na nisiyependa kuushughulisha ubongo wangu badala yake nimekaa tu hapa nangojea kuajiriwa na kwanini nisijiajiri mwenyewe au nisiungane na wenzangu kujiajiri! Lakini ukweli ni kwamba sisi tunaotoka kwenye familia za chini na kati tuna mazingira magumu sana ya kujiajiri tatizo kubwa likiwa ni ukosefu wa amtaji.
Mheshimiwa rais! tunatambua uwepo wa mikopo kwa vijana hasa wale watakaojihusisha na kilimo but process zake zinatufanya tuamini kuwa hiyo mikopo ipo kwenye maandishi tu! sijawahi kuona au kusikia fulani na fulani waliomaliza chuo kikuu wamepokea mkopo toka serikalini! Pia mikopo juu ya fani nyingine tofauti na kilimo ni kama vile hakuna! sasa najiuliza je selikali inataka wote tuliomaliza chuo kikuu tuwe wakulima?!
Mheshimiwa rais! Nadhani pamoja na malalamiko mengi tuliyonayo ila nadhani wizara ya kazi, ajira na maendeleo ya vijana haitimizi wajibu wake! Haiwezekani wizara inayohusika na vijana haina connection na vijana! wizara inayohusika na vijana haijulikani kwa vijana! na hata mpango wa maendeleo wa vijana binafsi nimekutana nao bahati mbaya tu katika harakati zangu za kugoogle! Mheshimiwa rais kwa vile soon unategemea kurekebisha baraza lako la mawaziri hebu jaribu kuiangalia na hii wizara!
Mheshimiwa rais! kulalamika tu haitoshi! nadhani natakiwa kutoa na mapendekezo kidogo! Ajira za kitanzania zinatolewa kiundugu sana hili linatakiwa kukomeshwa mara moja! kuna watu waliwahi kupendekeza ajira za serikalini watu tuwe tunaapply online kama vile watu wanavyoapply vyuo siku hizi kupitia TCU! ndhani hili ni wazo zuri sana na litatoa uwanja wa haki na usawa kwa watanzania wote!
Pili, mheshimiwa rais kuhusu hii mikopo kwa vijana ni kwanini na yenyewe isitolewe kwa kutumia system kama ile ya Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB)?! nadhani matumizi ya system kama ile ya HESLB itasaidia kupunguza urasimu uliopo selikalini!
Mheshimiwa rais! kuna kitu kingine kinaitwa recruitiment agencies!! hawa watu wanatunyonya sana sana sana sana!!!! unapoajiriwa kupitia haya makampuni ni kwamba unafanya kazi kwa almost nusu mshahara kwa maisha yote utakapokuwa umeajiriwa na hawa watu! ninatambua kuwa haya makampuni yanaendeshwa na hiyo sehemu ya mshahara wa hao waajiriwa lakini wanapoamua kukata nusu kabisa ya mshahara tena kwa wafanyakazi zaidi ya 500 tena kwa miaka yote inakuwa sio haki! nadhani serikali yako inabidi iyafuatilie haya makampuni na kuweka uwanja wa usawa na kuondoa huu unyonyaji na kuweka mazingira sawa kwa watu wote yaani muajiri, muajiriwa na huyu mtu wa kati!
mheshimiwa rais! kwa leo yanatosha, naomba nikutakie kazi njema ya ujenzi wa nchi yetu.
Ni mimi;
Ndugu yako.