Elections 2010 Barua ya wazi kwa tume za uchaguzi tanzania

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Ndugu waTanzania napenda kuchukua fursa hii ili kila mpenda amani wa Nchi hii na walio nchi za Nje waweze kufahamu kuwa ,picha inayopatikana katika kura za maoni kupitia Chama kikuu Tanzania CCM ni sura mbaya sana ambayo imesababishwa na Tume hizi za Uchaguzi kwa kuendesha Chaguzi zisizokuwa za haki zisizo na uwazi na ukweli ,Chaguzi zilizojaa udanganyifu uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na Tume hizi za Uchaguzi Tume kuu ya Tanzania na ile Tume ya Zanzibar.

Udanganyifu ambao umefanywa na tume hizi umejenga taswira ndani ya wananchama wa CCM wagombea kuwa wakishapita katika kura hizi na kufanikiwa kuvuka kikao chao cha mwisho basi wao tayari wanajihesabu ni wabunge wa Bunge la Tanzania au ni wawakilishi kwa upande wa Zanzibar.

Taswira au tukionacho hivi sasa ni ugombea wa nafasi hizo ndani ya Chama Cha CCM ukiwa umejaa malalamiko yaliojaa dhulma rushwa upotoshwaji wa matokeo na kutumika kwa mamluki ili kumsaidia mtu avuke kwa idadi ya kura za wizi ,kwa ufupi hawana uchaguzi wa haki ndani ya chama chao, tumeona hawa wanaoshughulikia ruswa wakikamata hapa na pale bila ya mafanikio yeyote ile zaidi na wao wanakuwa na mtu wao ambae aidha hakupita hivyo wanatumika katika kumsakia nafasi yule walienae kapuni aidha na kwa wao kupewa chochote.

Chimbuko la yote haya ni ukiukwaji wa uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Tukiangalia chaguzi kuu zilizopita utaona ni kwa kiasi gani tume hizi zilitumika pia kukishirikishwa vyombo vya dola katika kuipatia CCM ushindi wa kishindo ,ushindi unaomkosesha hata mpinzani kujua kura yake na ya mkewe zimekwenda wapi maana hakupata hata kura moja.

Mikakati na mbinu hizo iliyorahisisha ushindi wa CCM kwa asilimia miamoja ndio inayotumiwa na wanachama wa CCM katika kusaka nafasi hizo za ubunge na uwakilishi ,kuna wanaCCM wanaruhusa au wana nguvu ya kuweza kutumia vyombo hivyo bila ya woga na hakuna wa kuwahoji kwa kuwa pengine nae alishiriki katika siku zilizopita kuvishirikisha vyombo hivyo ili CCM iibuke kidedea ,hapo utaona hawatashindwa kuvitumia vyombo hivyo katika mambo binafsi ukiwemo uchaguzi iwe hata ni rafiki yake ndie anaegombea kupita katika harakati za mwanzo.

Tume hizi inawezekana kabisa zinajua athari ya kutumika kwake katika kuifanya CCM ishinde kwa wizi ,na matunda ndio haya tunayoyaona leo ,kumejaa ukiritimba na rushwa pamoja na wizi tokea kwenye chaguzi za ngazi za chini ,hili ni gonjwa linalohitaji dawa kabla halijawa gonjwa sugu.

Uchaguzi ni jambo ambalo linahitajiwa kufanywa kwa haki bila ya kupendelea upande wowote ule ,watu wahusika wa tume ni lazima wajue kuwa wamebeba dhamana ya Nchi nzima na sio kuwa wamebeba dhamana ya kuifanya CCM ishinde,dhamana ambayo walionyesha kuwa wameibeba katika chaguzi zilizopita na matokeo yake ni uendeshwaji mbaya wa utawala katika nchi hii ambao haujapata kutokea.

Raisi ambae amepewa ushindi ameendesha nchi kwa nguvu za ziada nguvu za uvumilivu na kwa upole usiovumilika kwa wananchi ,hivyo kumfanya aonekane hana alilolitenda isipokuwa kusukuma siku ili muda upite,alihitajiwa kuchukua hatua za nguvu dhidi ya ufisadi lakini hakuweza ,sababu ushindi wake una hitilafu ,wanaovuruga ndio waliomsaidia kumfanya ashinde kiurahisi.

Tumeona mbinde ndani ya CCM ,mapambano ndani ya bunge ,na wezi kukamatwa wakiwa na mikia (Msemo wa kiswahili unaosema anaekamatwa na mkia ndio mwizi wa ng'ombe) lakini hatua za kisheria zimeshindwa kuchukuliwa na hata kama zimechukuliwa hatua za utekelezaji wa hukumu haukuonekana ,sababu ushindi wa watu hawa wanajuana ni namna gani walivyoshinda hivyo kila mmoja anamwogopa mwenzake kuwa atamwaga mboga ikiwa ugali utamwagwa.

Matatizo yote hayo yanatokana na tume hizi za Uchaguzi kuendesha uchaguzi kiupendeleo,uendeshaji ambao muathirika nambari one ni mwananchi mpiga kura aliekwenda kuchagua anemuona ndie atakaemuokoa katika kuing'oa Tz na majanga mbali mbali lakini Tume inamupitisha mtu mwengine asiejua thamani ya mwananchi mpiga kura ,hii ni dhambi kubwa sana inayofanywa na Tume hizi.

Ndio utaona wabunge na wawakilishi wengine na hata Mawaziri hawaonekani na wananchi wala hawapiti huko waliko wananchi kuwajulia hali zao pamoja na matatizo yanayowakumba,leo tunamsikia au tunawasikia waheshimiwa wakisema eti mwananchi asiambiwe rudi kesho !! Leo ikiwa imebaki masiku tu kushuhudia unyongwaji mwengine wa waTanzania utakaotekelezwa naTume ya Uchaguzi.

Tume ni lazima ijirekebishe na isimuonee haya mtu yeyote yule kwani watu hawa hawajawa Raisi wala hawajawa Wabunge au wawakilishi ni raia wakawaidda wanaogombea nafasi za uongozi wa nchi hii ambao wanapatikana kwa kura za wanaokwenda kushinda kwenye vituo vya kura kuanzia asubuhi hadi jioni wakitegemea haki itatendwa na Tume kwa kutoa matokeo yasiokuwa na kasoro na yenye uwazi usiopingika popote pale ,ila matarajio yao yanazimwa na tume kwa kutoa matokeo ya uwongo na kumpendelea mtu fulani ndio au chama fulani ndio lazima kishinde.

Kama tume hizi zitatenda haki iliyowazi hawatakuwa na sababu ya kuchelewesha matokeo hata sekunde moja ,kituo kinafungwa kura zinahesabiwa zinatangazwa hapo hapo kupitia redio au televizion na wa[iga kura waliomajumbani waliokamata kalamu na upande wa karatasi wakijumlisha kwa kila mtajwa ,kwamba tume wanamaliza kutangaza matokeo yote na alie nyumbani tayari anajumlisha au ameshapata matokeo kamili na kujua nani ameshinda na nani ameshindwa ,haiwezekani mnaweza kutoa vikao vya bunge kwenye stream za ITV mkashindwa na hili la uchaguzi wakati mitandao ya simu imeenea Tanzania nzima.

WaTanzania wapo katika hatua za mwisho za kuivumilia hali hii ya unyongwaji wa haki zao.Iko siku watasema basi na haipo mbali.
 
Heko mkuu, tunahitaji barua kama hizi zisambae nchi zima zinabndikwe kila mahali ili watu washuhudie kila sehemu mambo ya ajabu yanayofanywa na CCM. Wakubali wasikubali nchi imewashinda hata kama watashinda lakini rushwa iko ngazi zote za nchi hii kuanzia kwa mabalozi hadi ikulu. Jamani toweni mawazo sasa tufanyeje? Wazo kuu ni kupiga kura, kuhamasisha watu wakapige kura, lakini la msingi ni kuhakikisha tunalinda kura zisiongezeke wala hakuna udanganyifu popote pale.

Cha msingi ni Back_up nammanisha tuwe na mbinu mbadala wa kuhakikisha tunashindwa kwa halali na sivy ilivyo sasa. Naimani watanzania wa leo ni tofauti na wale wa 2005. wanajua kila kitu saizi kinachoendelea, tena yale mabomu 20 ya Dr yatawahamasisha wengi sana kupiga kura mwaka huu tuonee sasa.
 
Back
Top Bottom