Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,593
2,767
Mhe Rais. Kwanza nikutakie kila la kheri katika kazi hii nzito uliyokabidhiwa na Wananchi wa Tanzania kuwaongoza ili wafikie kilele cha ustawi. Ni imani yangu kuwa Mwaka 2019 utakuwa wa Baraka na neema zitokazo kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili yako na kwa ajili ya Watanzania kwa ujumla wetu.

Pili, ninalazimika kutumia njia hii ya wazi kukuandikia waraka huu ili kukumiminia dukuduku langu ambalo ni imani yangu kuwa utasoma, kutafakari na kuchukua hatua stahiki.
Hoja yangu kwako ningependa ichukue kichwa kisemacho:
NANI BOSI WA MWINGINE KATI YA RAIS NA MWANANCHI?
Mhe Rais, tangu enzi za kale tawala duniani zimechukua mifumo yenye sura kuu mbili:- i) Tawala za Kifalme ii) Tawala za Ki-jamhuri
  • Katika utawala wa Kifalme, mfalme ndiye mtawala mkuu na wananchi huwa ni raia tu. Hapa ndipo tunapopata maneno “subjects” na “citizens” yakiwa na maana mbili tofauti.
  • ‘Subjects’ ni neno linalotokana na maneno mawili ya Kilatini ‘sub’ na ‘jacio’ ambayo yakijumuishwa humaanisha “aliye chini ya mamlaka ya mwingine”
  • Mhe, kwenye tawala za kifalme, mfalme ndiye mamlaka ya juu katika nchi (KATIBA) na watu wengine wote ni (subjects) watumwa tu, japo katika kupunguza ukali wa maneno, Kiswahili kilitafsiri neno ‘subjects’ kama ni raia, kiuhalisia ni watumwa wa mfalme.
  • Hebu tuyatafakari maneno haya ya Bwana Yesu Kristo kuhusu mifumo ya ki utawala:
  • Na wale kumi waliposikia walikasirika sana. Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu, na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.” Mathayo 20:24-28.
  • Hapa Bwana Yesu anazungumzia mfumo wa tawala za kifalme, zenye kutumia nguvu na zisizojali haki za watu, maana kwao watu walikuwa ni watumwa tu (subjects).Bali haishii kwenye mfumo huo, anawaonyesha wafuasi wake mfumo ulio bora zaidi. MFUMO WA KIDUGU, ambamo kila mmoja ni sawa na mwenzake, na mkubwa huwa ni mtumishi tu wa wadogo. Kwa hakika mfumo wa Ki-jamhuri ulifafanuliwa vyema na Bwana Yesu japo tayari miaka mingi nyuma Warumi walikuwa wameuanzisha pamoja na kwamba haukudumu sana baada ya kuingiliwa na tamaa ya Makaisari; akianza Kaisari Julius.
  • Pia tukifahamu jinsi wafalme walivyokuwa wanapatikana, basi tutajua kwa uhalisia ni nini hasa maana ya mahusiano haya kati ya mfalme na raia wake. Daima katika utawala wa aina hii raia huisikia na kuitegemea sauti ya mtu mmoja tu - Mfalme.
  • Hii si mada yangu muhimu sana kwako kwa leo, maana kadiri karne zilivyosonga na watu katika nchi mbalimbali kujitambua waliamua kuondokana na adha hii ya kuwa watumwa wa mtu mmoja na ukoo wake kwa kisingizio cha kuchaguliwa na Mungu.
  • Waliamua kuingia katika taratibu za Jamhuri. Mapambano yalikuwa makali, lakini mwisho raia walishinda na kuanzisha Jamhuri katika nchi zao. Mfano mzuri ni Mapinduzi ya Ufaransa yaliyomwondoa mfalme Louis XVI.
  • Utawala wa Ki-jamhuri: Huu ni utawala wa watu kuchaguana na kupata VIongozi miongoni mwao kidemokrasia. Msingi wa utawala wa kijamhuri ni watu; (the people reigns supreme). Watu hutengeneza KATIBA; na katika katiba ya jamhuri ‘watu’ hawa hujulikana kama “wananchi” (citizens). Hawa si raia (subjects), bali ni “wana wa nchi.” Ndiposa Bwana Yesu akawaita “wana ni mahuru” katika jibu lake maarufu kwa watumishi wa makuhani waliokwenda kumdai kodi. Mathayo 17:24-27.
  • Mwanafalsafa mmoja ameandika yafuatayo :-
  • “Subjects look up to a master, but citizens are so far equal, that none have hereditary rights superior to others. Each citizen of a free state contains, within himself, by nature and the constitution, as much of the common sovereignty as another.
  • In the eye of reason and philosophy the political condition of citizens is more exalted than that of the noblemen. Dukes and Earls are the creatures of kings and may be made by them at pleasure; but citizens posses in their own right original sovereignty”
  • The term “subject” is used rather than citizen because in a Monarchy the monarch is the source of authority in whose name all legal power in civil and military law is exercised. The people of a monarchy in former time were regarded as the monarch’s subjects who were under certain obligations such as owing allegiance to and thereby entitled to the protection of the crown.”
Mhe Rais, tukiangalia tafsiri ya maandiko hayo hapo juu tutagundua kuwa katika tawala za kifalme, bosi wa raia ni mfalme, naye mfalme anaweza kugawa raia hao katika madaraja ya kitabaka anayotaka kwa kusudi la kudumisha ufalme wake. Hii ni kinyume kabisa na utawala wa Ki - Jamhuri ambapo mwananchi (citizen), ndiye mwenye mamlaka ya juu ya maamuzi ya utawala kwa jinsi anvyohitaji aongozwe na kutendewa kama mtu huru.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaweka bayana jambo hili katika msingi wake ulio kwenye utangulizi kwamba: KWAKUWA SISI wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru,haki undugu na amani.
Mhe, misingi ya SISI wananchi (WE the people - citizens) wa Tanzania ni:- i) UHURU ii) HAKI iii) UDUGU na iv) AMANI
Kwa hakika hii ndiyo misingi inayotufanya kuwa watu huru (citizens)katika Taifa huru. Si Taifa huru tu, bali pia linalofuata mfumo wa kidemokrasia ambao umewekewa sheria ya katiba iliyoanzisha vyama vingi vya siasa.
Utekelezaji wa misingi inajengwa katika mihimili mitatu mikuu:-
i)Serikali ii) Bunge iii) Mahakama
Madhumuni ya vyombo tajwa hapo juu ni kuhakikisha kuwa Tanzania inajengwa kwa misingi ya uhuru, haki, udugu, na amani; kwa serikali kufuata barabara ya demokrasia (Democratic road)
Mhe, Ibara ya 8 (1.): (a), (b) na (c) inasisitiza juu ya “Ukuu wa watu (“ the supremecy of the people (citizens))” katika ujenzi wa Taifa lao.
“(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo:
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
Ibara ya 9.
Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;
(b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
(c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumyonya mtu mwingine;
(d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;
(f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu;
(g)kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu;
(h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
(i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;
(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha limbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.”
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Juu ya

Haki na Usawa:

Ibara ya 12:” (1)binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa.
(2) kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.”
Ibara ya 13: “(1) watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi.”
Baada ya kueleza kwa kirefu dhana yangu hapo juu naomba nitoe maoni yangu jinsi ninavyoitazama serikali yako ya awamu ya tano:
  • Naitazama kama serikali inayojitutumua kutaka kuvunja nguvu za Taasisi zilizotajwa katika Katiba sehemu ya utangulizi hivyo kutoheshimu misingi ya Uhuru, Haki, Udugu na Amani. Taasisi zinazovunjwa nguvu ni Bunge na Mahakama.
  • Serikali inayofanya juhudi nyingi kutoheshimu Demokrasia ya Vyama vingi. “SISI Wananchi (Citizens) wa Tanzania tumeamua” kujenga jamii inayoheshimu utu na usawa kwa njia ya kidemokrasia ya Vyama vingi; kinachoshangaza serikali kwa makusudi inatekeleza mfumo wa kisiasa wa kila siku kana kwamba uamuzi wa wananchi ni demokrasia ya chama kimoja.
  • Ubaguzi wa hadharani: Utendaji wa serikali ya awamu ya tano ni wa kibaguzi tena wa wazi wazi kinyume cha ibara za Katiba nilizozitaja hapo juu.
  • Kwa kutazama kwangu “Watu“ wamegawanywa katika makundi mawili makuu:
  • a. Kundi la “wananchi”; hawa wanatendewa haki zote za kisiasa na za kikatiba kama waungwana walioteremshwa na Muumba kutoka sayari ya juu. Hawa ndio wanaonekana kuwa citizens machoni pa utawala. Miongoni mwao hata kama watafanya makosa sawa na wengine bado watachukuliwa kuwa wao ni malaika.
  • b. Kundi la “watumwa (subjects)” : hili ni kundi ambalo daima linaonekana halina haki zozote za kisiasa na kijamii katika serikali hii. Kwa kifupi ni zaidi ya watumwa “subjects”, ni “Watwana (Serfs)”
  • Wakionewa hatua hazichukuliwi, wakidhulumiwa hakuna anayejali, wakitekwa au kupigwa risasi, hakuna uchunguzi wowote wa kidola, wakitoa maoni yao wanakamatwa, wakishiriki uchaguzi wa kisiasa watafanyiwa kila aina ya vituko vya kidola hadi ushiriki wao kwenye uchaguzi uonekane kama ni uharamia na uhalifu, hawatakiwi kuonyesha hisia zao zilizo kinyume cha serikali kwa maandamano au mikutano ya hadhara hata kama vifua vyao vimejaa malalamiko na manung’uniko dhidi ya serikali, wakipelekwa mahakamani bado serikali itafanya kila mbinu kuhakikisha inatumia sheria ili “watwana” hawa wazidi kusota rumande, hata wale wenye vyama kihalali kwa misingi ya Katiba ya nchi, hukokotwa hadi korokoroni wakionekana wamefanya vikao vyao vya ndani ambavyo ni haki yao wakati huo huo wenzao ambao ni "Citizens" wakiwa na haki ya kujitanua katika nchi kana kwamba ni wao tu waliumbwa kwa ajili ya Tanzania.
  • Nchi nyingi hasa za Kiafrika zimeingia katika vurugu kubwa kwa sababu kubwa moja kwamba pamoja na kwamba nchi hizo kupata uhuru katika mfumo wa Ki – Jamhuri, viongozi wake wengi walijielekeza katika mifumo ya Kifalme (Kiimla) kwa kugawa watu kwenye makundi kama niliyoyataja hapo juu. Wengine ilikuwa ni katika migawanyo ya Kikabila, Kidini au Kivyama. Baadhi hata walitunga sheria za kishetani ili kuweza kudhibiti madaraka yenye kuendeleza ubaguzi. Kwa hakika wanaonyanyaswa kamwe hawakukaa kimya, walijibu mapigo, wengine kwa kuingia msituni na kuanza mapambano, na wengine walio wastaarabu zaidi waliwahujumu watawala hadi wakasalimu amri.
  • Mhe Rais, Afrika na watoto wake imeona madhila mengi sana kiasi kwamba sasa ni wasaa muafaka kwa “Wana wa Afrika” kupumua na kujiongoza kwa ustaarabu wa hali ya juu. Afrika imechoka kudharauliwa na kila bara kwamba Wana wa Afrika na Viongozi wao hawana tofauti na Wanyama walio katika mbuga za Serengeti, kwamba mwenye nguvu ndiye alaye chakula kingi. Tanzania nchi ya Mwalimu Julius Kmbarage Nyerere, Mwanafalsafa wa Ustaarabu kutoka dunia ya Tatu, inayo nafasi ya kuepuka barabara ya Afrika tuijuayo. Nafasi inayoamini kuwa: “Binadamu wote ni Ndugu zangu, na Afrika ni moja.”
  • Mtazamo kuhusu Ukuu wa Tanzania: Nchi yetu yapaswa kuwa nchi yenye Siasa Imara Kidemokrasia. Nchi inayoheshimu Haki za Watu, ikikuza Uchumi wake kwa mlingano wa Ustawi wa Watu wake. Hivyo basi ni mtazamo wangu kuwa sivyo ilivyo katika awamu ya tano. Uongozi wa awamu hii unaitazama Tanzania si kama mjumuiko wa watu wenye mawazo na mitazamo mbalimbali, bali kama kikundi cha wana CCM ambao wote kwa pamoja wanatakiwa kuimba mapambio ya “Wapinzani tuwalete, tuwachane chane tuwatupe.”
  • Kwa hakika haipaswi kuwa hivyo kwa sababu Tanzania inaweza kuwa Dude Kubwa (Giant), Kimkoa na Kimataifa (Regionally and Internationally) katika Nyanja za Siasa za Kidemokrasia na Uchumi. Twaweza kwa kweli kuwa “ Nyonga ya Afrika”(nikuazima maneno ya Profesa Palamaganda Kabudi), kwa yote mawili ikiwa tutadhamiria kuwa watu waungwana (civilized) katika uendeshaji wa taasisi zetu na hasa Taasisi yenye dhima Kuu: Dola ya Tanzania.
  • Mwisho, nakutakia kila la heri nikiamini kuwa hutajisikia vibaya kwa kuyasoma maandiko haya, kwani mimi kama Mtanzania nimeona ni vema nifanye hivi ili kuwasiliana na Kiongozi wangu kwa kueleza ukweli wa moyoni, maana "Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Asante.
 
Nondo nzito
 
...Mhe Rais. Kwanza nikutakie kila la kheri katika kazi hii nzito uliyokabidhiwa na Wananchi wa Tanzania kuwaongoza ili wafikie kilele cha ustawi. Ni imani yangu kuwa Mwaka 2019 utakuwa wa Baraka na neema zitokazo kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili yako na kwa ajili ya Watanzania kwa ujumla wetu.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaweka bayana jambo hili katika msingi wake ulio kwenye utangulizi kwamba: KWAKUWA SISI wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki undugu na amani.
Mimi nitachangia kwa swali fupi tu...asante sana, ujumbe murua umeutoa lakini je, utapokelewa? Kwa nchi hii ilipofikia nina wasiwasi mkubwa na namna barua yako itakavyopokelewa. Bila shaka utakuwa umepata taswira ya mwitikio wa mhusika mkuu baada ya kusoma michango kutoka kwa baadhi ya wahusika wadogo wadogo kwenye hii thread. Inasikitisha, inafadhaisha na inakasirisha kukuta Watanzania wenzetu wakiunga mkono utawala wa kiimla usiojali kama kuna misingi tuliyojiwekea na kukubaliana kuifuata katika uendeshaji wa nchi.

Uzuri ni kwamba ufashisti wa aina hii una maisha mafupi kwani hakuna binadamu anayependa utumwa. Nani, kwa mfano, alijua au hata kuota kuwa ukaburu Afrika Kusini ungekuwa historia? Hata hapa Tanzania, ni swala la muda tu...hata anayenenepa kwa kusukumiziwa tonge mdomoni akilishwa iko siku anakinai akidai uhuru wa kujilisha kwa wakati wake na ole wako ushindwe kutambua hilo. Kiu ya mabadiliko ya kudai uhuru si lelemama na ni mpumbavu tu ataziba masikio akiamini atalala kwa raha kwani kishindo chake ni zaidi ya tsunami!
 
Mafumbo mengi sana sentensi moja tu ingetosha sana. mimi ni ningependa kama ungeongelea bomberdier kidogo na airbus mpya, reli ya umeme, barabara na madawa hospitali namna huduma zilivoboreshwa alafu useme ni uhuru gani wewe unaotaka kama mzalendo.
 
JIWE GIZANI.THE MISSILE OF THE NATION
 
Mimi nitachangia kwa swali fupi tu...asante sana, ujumbe murua umeutoa lakini je, utapokelewa? Kwa nchi hii ilipofikia nina wasiwasi mkubwa na namna barua yako itakavyopokelewa. Bila shaka utakuwa umepata taswira ya mwitikio wa mhusika mkuu baada ya kusoma michango kutoka kwa baadhi ya wahusika wadogo wadogo kwenye hii thread. Inasikitisha, inafadhaisha na inakasirisha kukuta Watanzania wenzetu wakiunga mkono utawala wa kiimla usiojali kama kuna misingi tuliyojiwekea na kukubaliana kuifuata katika uendeshaji wa nchi.

Uzuri ni kwamba ufashisti wa aina hii una maisha mafupi kwani hakuna binadamu anayependa utumwa. Nani, kwa mfano, alijua au hata kuota kuwa ukaburu Afrika Kusini ungekuwa historia? Hata hapa Tanzania, ni swala la muda tu...hata anayenenepa kwa kusukumiziwa tonge mdomoni akilishwa iko siku anakinai akidai uhuru wa kujilisha kwa wakati wake na ole wako ushindwe kutambua hilo. Kiu ya mabadiliko ya kudai uhuru si lelemama na ni mpumbavu tu ataziba masikio akiamini atalala kwa raha kwani kishindo chake ni zaidi ya tsunami!
Ndugu yangu Mag3, ujumbe upokelewe usipokelewe si hoja. Hoja ni kuwa nimetimiza wajibu wangu kama 'Citizen.' Katiba Ibara ya 18 inanipa uhuru huo. Na kwa kweli nachukia Mtanzania mwenzangu hata awe ni kiongozi kunifanya kuwa 'subject.' Haikubaliki.
 
Back
Top Bottom