muonamambo
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 875
- 545
Mh Rais kwanza napenda kukusabahi na kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuingoza nchi yetu vizuri.Pamoja na mapungufu machache ya kibinadamu bado mazuri ni mengi na ya kusifika.
Utekelezaji wako wa kuondoa ufisadi serikalini na Tanzania kwa ujumla, kuhimiza uwajibikaji, kuongeza makusanyo ya kodi( japo lina mapungufu), Ujenzi wa reli, Ujenzi wa barabara ili kurekebisha foleni Dar es Salaam, Ununuzi wa ndege( japo kuna mapungufu) , kurudisha nidhamu serikalini na nchi kwa ujumla.
Kwa hayo yote nakupa pongezi za dhati na nazidi kukuombea hekima, nguvu na afya ili uendelee kuiongoza vyema Tanzania.
Yapo mapungufu machache ambayo si mada ya barua hii hayo nitayazungumzia siku zijazo.
Mh. Rais, Si kawaida yangu kuandika barua za wazi lakini nimeona labda njia hii inaweza kukufikia kwa kuwa wewe mwenyewe umekiri kuwa huwa unapitia mitandao. Pia kwangu Mimi kuweza kukuona ana kwa ana imekuwa ni vigumu.
Mh. Rais, Kwenye kampeni zako ulikuwa na agenda kubwa ya "Tanzania ya Viwanda inawezekana" na nadhani ndio agenda ya CCM. Kwa kulitambua hitaji hilo nakuandikia Waraka huu kukupa ushauri ambao una hiyari ya kuuchukua au kuuacha.
Mh. Rais, Ili Tanzania tupige hatua kwenye viwanda na kuwa super economic country in East Africa tunatakiwa tufanye yafuatayo.
Mh. Rais Ukumbuke tu kwamba uendelezaji wa viwanda ni kitu cha muda mrefu na mafanikio yake huchukuwa muda mrefu bali hudumu na yananufaisha watu wengi.
Mh Rais sisi si wa kwanza kufanya haya Ghana wanafafanya na yameanza kuzaa matunda. Wachina , Malaysia na Asia ya Kati wame fanya na wamebadilisha uchumi wa nchi zao
Baada ya miaka kumi kodi zinawezwa kuanza kurudishwa taratibu bila kuathiri ukuuwaji wa viwanda.
Mwisho napenda tena kukupongeza kwa Kazi nzuri unayoifanya na nipende kusema tu hatujachelewa "Tanzania ya Viwanda inawezekana"
Wana JF wenzangu mnaruhusiwa kuongeza ushauri mnaona unafaa au kuondoa use usiofaa bila matusi wa mambo ya Vyama . Kwani matusi na Vyama havijengi Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki serikali ya JPM
Muonamambo
April 2017

- 1. Tuanzishe mpango wa kuwawezesha wazawa kutengeneza viwanda ... "Stimulation package special for local businesses to create agricultural industry" Simulation hiyo itumike kama 'Result based finance" kea kiwanda kitakachofanikiwa kufikisha malengo. Malengo yanaweza kuwa kufnikiwa kufungua kiwanda husika, Idadi ya waajiriwa, uanzishaji wa uzalishaji nk.
- Kwa zingatia kuwa maendeleo ya viwanda ni suala endelevu na linalohitaji Kati ya miaka 5-30. Napendekeza suala hilo lisichukuliwe kwa pupa na lifanyiwe utafiti wa kina .
- Tanzania bara ( maana siamini kwenye muungano) ina mikoa 20 na kila mkoa una Wilaya Kati ya 4-7 . Kwa kukadiria tuna wilaya zisizopungua 100.
- " Tuanzishe kampeni endelevu ya "Kila wilaya viwanda 20". Hivi visiwe vya serikali kwani serikali imeshashindwa kufanya biashara. Bali viwe na vya watu binafsi wafanyabiashara wazalendo, Joint venture na makampuni au matajiri wa nje, au wawekezaji wa kutoka nje.
- Viwanda hivi view via kuzalisha na kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo Kama " Value Added Agricultural, Processing, Packaging industries" nk
- Ifanyike study ya kuchunguza kila mkoa na rasilamali ghafi zilizopo, aina ya Mazao yanayolimwa na any opportunity iliyopo inayowezwa kuendeleazwa.
- Kisha serikali itowe orodha ya Viwanda vinavyohitajika kila wilaya na Aina ya uwekezaji unaohitajika ( mfano Viwanda vya Matunda Tanga vinatakiwa 10 vyenye uwezo wa kuzalisha Tani 100,000 kwa Mwaka ya Mapunda, kuajili watu 20,000 nk)
- Wafanyabiashara wazalendo wanaweza kuunganisha nguvu au mmoja mmoja wapewe nafasi ya kufungua viwanda hivyo. Pale ambapo wazawa wamekosekana basi JV na makampuni ya nje yaruhusiwe kwa masharti ya kumpa mzawa / wazawa asilimia 50 ya shares.
- Yatengwe Maeneo maalumu ya Viwanda na yajangwe marengo ya kiviwanda yanayofikika na yatolewe bure kwa wawekezaji. Maeneo hayo yanatakiwa yawe yanafikika kirahisi na yasiwe mbali sana na makazi ili vijana watakaoajiriwa waweze kufika kwa gharama ndogo. Kufikika huko pia kutarahisisha usafirishaji wa raw materials na end products.
- Mh Rais . Ondoa kodi zote za import duty, VAT kwa vifaa , machines zitakazoagizwa kwa ajili ya Viwanda hivyo kwa kipindi cha angalau miaka 10-15.
- Mh Rais,Toa kodi zote za WHT, capita Gain na Cooperate Tax kwa Viwanda hivi kwa muda wa miaka 5 ili viweze kujiimalisha.
- Maeneo yaliyotengwa yapelekewe huduma muhimu Kama Umeme na Maji na barabara ili kuimarisha uzalishaji.
- East Africa pekee inakadiliwa kuwa na watu wasiopungua Million 100. Hii ni sawa na kaya Million 20 . Hili soko kubwa sana la kuanzia kwa Viwanda vyeti.
- Kwa viwanda 20 kila wilaya tunaweza kutengeneza viwanda 2000 baada ya miaka 5 vyenye kuajili vijana na wahitimu wasiopungua Million 1( kwa wastani wa vijana 500 kwa kiwanda
- Chain value ya viwanda itatengeneza mahitaji ya biashara za usafirishaji wa mizigo, watu Mabati, pikipiki na a Kaji, ufundi mchundo, bidhaa za chakula ( mama ntilie, migahawa), macahapisho, packaging, Mali ghafi zingine zisizo za kilimo nk. Hizi zote zinaweza kuleta ajira ya watu wasipungua laki 5
- Kuwepo kwa viwanda kutaongeza mahitaji ya bidhaa za kilimo na hivyo kuongezq ufanisi wa kilimo chetu na kuinua uchumi wa Wakulima.
- 18. Wawekezaji wazawa waruhusiwe kukopa bank chini ya Guarantee ya serikali yenye riba ya BOT
- Simulation package inawezwa kuchangiwa kupitia kwenye vyanzo vifuatavyo
- Ushuru mdogo kwenye bidhaa za utalii
- Ushauri mdogo sana kwenye mafuta
- Misaada ya Donors countries
- Mikopo isiyo na riba toka kwa mataifa marafiki