Barua ya wazi kwa mkuu wa wilaya mpya ya Morogoro

Nalipa kodi ndiyo kazi yake haswa na nina haki ya kuhoji kodi yangu inatumika vipi, hasa pale ninapoona mikoa ya wenzangu mpaka barabara za kuvukia ng'ombe zina lami.
We jifungie huko huko kwenu tununguo, njoo mjini uone brother.

hahahaaaaaa,we unafikiri kila mtu ni wa tununguo,kusanyeni kodi za kutosha za mazao yenu,limeni kibiashara na si kimazoea,lami zitawafuata zenyewe tu
 
Mheshimiwa mkuu wa wilaya heshima nyingi pia natumai umzima kiafya.
Ama baada ya salamu, nikupe pole kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya wilaya hii. Ndiyo, pole. Pole kwa kuwa nafahamu changamoto ambazo utaenda kukutana nazo katika wilaya hii. Labda nikwambie tu, wilaya hii nahisi ndiyo wilaya yenye vichekesho vingi kuliko wilaya nyingine yoyote ile.

Baadhi ya vituko hivyo ni kama ifuatavyo:
1. WILAYA HII OFISI ZAKE ZIPO KATIKA WILAYA NYINGINE.
Kifupi majengo yanayotumiwa na wilaya hii yapo katika halmashauri ya manispaa ya Morogoro hivyo hakuna jengo la halmashauri ndani ya wilaya husika.

2. HAKUNA HATA MITA KUMI ZA BARABARA YA RAMI.
Hii ni moja ya wilaya ambayo toka uhuru awajawahi kuona hata kipande cha mita kumi za rami pamoja na umuhimu wa eneo la morogoro vijijini kwa kuwa na eneo kubwa la ardhi inayofaa kwa kilimo.

3. HAKUNA HATA SHULE MOJA YA SEKONDARI YA JUU (ADVANCE LEVEL)
Katika wilaya hii hakuna hata shule moja ya sekondari ya juu yaani advance level. Shule kongwe katika wilaya nzima ni Matombo sekondari.
Ila, karibu na usiogope

4. HOSPITAL YA WILAYA KITUKO.
Hospitali ya wilaya ipo sehemu moja inaitwa Tawa naamini watakupeleka na utaiona wewe mwenyewe. Kama ingekuwa Dar es salaam naamini ningeifananisha na kituo cha afya cha tabata au Tandale kwa mtogole.
Ila karibu usiogope, tutakupeleka

5. UKUBWA WA WILAYA YENYEWE NAYO NI CHANGAMOTO
Kijiografia wilaya ni kubwa yenye vijiji vingi ambavyo vingine havifikiki kirahisi. Vijiji vya Nyingwa, Lanzi, Lumba, Kitengu, Dehele, Mwangazi na kiunza. Vijiji hivi nilivyokutajia, kuna watu wanakufa hawajawahi kuona gari. Kuna maeneo mengine sijui hata kama serikali yenyewe kma inayatmbua.
Ila karibu usiogope tutakupeleka.

Tafadhali ukija huku, acha ujuaji shirikina na watu, nakwambia hivyo kwa nia njema tu, kwa kuwa nawajua watu wa huku vizuri pengine kuliko wewe.
Karibu sana mheshimiwa, karibu mkuu wa wilaya. Labda wewe unaweza ukawa tumaini jipya la wilaya hii, maana hawa wabunge wamepita wengi hatujawa na manufa nao.

Wakuu wa wilaya nao wengi walikuwa ni wale wale.

Ni mimi mwenyeji wako.
Changamoto ni nyingi sana, sijui kwanini hii wilaya imesahaulika kiasi hiki, na wananchi wake hawajawahi kufanya mabadiliko ya wabunge wake kwa kujaribu upinzani, sijui no kuridhika au kuna jambo behind. Hata manispaa nako barabara ni full mahandaki karibu kila baada ya mita ishirini
 
hahahaaaaaa,we unafikiri kila mtu ni wa tununguo,kusanyeni kodi za kutosha za mazao yenu,limeni kibiashara na si kimazoea,lami zitawafuata zenyewe tu

Hujielewi wewe. Kumbe wewe upo kwenu kagera unajihusisha kupinga mambo y morogoro kana kwamba wewe ni mkazi wa huku.
Haya wahi lumumba kchukue buku mbili yko
 
Changamoto ni nyingi sana, sijui kwanini hii wilaya imesahaulika kiasi hiki, na wananchi wake hawajawahi kufanya mabadiliko ya wabunge wake kwa kujaribu upinzani, sijui no kuridhika au kuna jambo behind. Hata manispaa nako barabara ni full mahandaki karibu kila baada ya mita ishirini

Kuna bwege hapa linadai lami ipo. Bora wewe useme labda atakuelewa.
 
Hujielewi wewe. Kumbe wewe upo kwenu kagera unajihusisha kupinga mambo y morogoro kana kwamba wewe ni mkazi wa huku.
Haya wahi lumumba kchukue buku mbili yko

Duhh!,mluguru wewe kweli chenga,umejuaje kama mie ni wa kagera??,unaniyeyusha,ngoja nipalilie minanasi yangu hapa shambani kwangu kinole
 
Kwa hiyo huko kwenu kinole ndiyo kuna lami? Kweli ccm itatawala sana mpaka watu wa aina hii wafe.
 
shida uelewa wako upo duni,unadhani kila tatizo ulilonalo sababu ni ccm,toka nje ya box wewe,maarifa unayo?,ubunifu je?,sio kulalamikalalamika tu
 
Kwa hiyo nje ya box ndiyo mimi nije kujenga barabara za lami?
Nije nijenge shule nzuri za advance katika wilaya?
Nijenge hospital ya wilaya yenye hadhi ya wilaya?
Hivi ulishawahi kuwaona warugulu wenzio wanavyotia huruma wakija hapa hospital ya mkoa?
Kwa taarifa yako mimi ni daktari hapa hospitali ya mkoa, wagonjwa wengi wanatoka katika wilaya hii na wameifanya hospital hii kuwa kama hospital ya wilaya ya morogoro.
Wake up and start to live bro.
 
Mkuu Tawa huko lumba chini hakuna hata network n shida tupu
Mkumbushe aje huku kibogwa juu make wale wengne wanaishia Tawa na kurudi mjini
 
Kwa hiyo nje ya box ndiyo mimi nije kujenga barabara za lami?
Nije nijenge shule nzuri za advance katika wilaya?
Nijenge hospital ya wilaya yenye hadhi ya wilaya?
Hivi ulishawahi kuwaona warugulu wenzio wanavyotia huruma wakija hapa hospital ya mkoa?
Kwa taarifa yako mimi ni daktari hapa hospitali ya mkoa, wagonjwa wengi wanatoka katika wilaya hii na wameifanya hospital hii kuwa kama hospital ya wilaya ya morogoro.
Wake up and start to live bro.
Huyo hajaona uhalisia wa matatizo ya Nyingwa, Lanzi, Lumba, Kitengu, Dehele, Mwangazi na Kiunza!
 
Kwa hiyo nje ya box ndiyo mimi nije kujenga barabara za lami?
Nije nijenge shule nzuri za advance katika wilaya?
Nijenge hospital ya wilaya yenye hadhi ya wilaya?
Hivi ulishawahi kuwaona warugulu wenzio wanavyotia huruma wakija hapa hospital ya mkoa?
Kwa taarifa yako mimi ni daktari hapa hospitali ya mkoa, wagonjwa wengi wanatoka katika wilaya hii na wameifanya hospital hii kuwa kama hospital ya wilaya ya morogoro.
Wake up and start to live bro.

we dakitari au dakatara unayelaumulaumu tu ccm na unayeconlude kuwa natokea kagera bila haya,utafikiri umefanya utafiti,nyie ndio wale matabibu wa kufanya operesheni ya kichwa badala ya mguu kwa kuwa hata hamtafiti,serikali ikuletee lami hv hv tu bila kufanya cost benefit analysis,hospitali sawa,wabunge wenu wamefanya nn huko bungeni kuhusiana na suala hilo,mnawachagua wenyewe halaf mnakuja mitandaoni kulalamika wakati sasa hivi ulitakiwa uwahudumie wagonjwa,we upo JF,halafu unalaumu laumu serikali tui
 
Sidhani kama ghorofani upo sawa
 
Kuhusu Namba 1

du aliyeandika hajui anachoandika.kimsingi wilaya ya morogoro haijui na asipotoshe jamii.wilaya ya morogoro ina halmashauri mbili ambazo ni halm ya manisp na halm ya wilaya ambapo ofisi za wilaya zipo mansp.
 
utakuwa daktari wa vichaa tu wewe na si tulio timilifu

Hata jinsi unavyoandika unaonekana kabisa wewe ni mgonjwa gorofani. Unahitaji tiba bro wahi mapema utakuja utupe tabu baadaye.
 
tehh tehh tehh,daktari upooo??,wagonjwa wa kitengo chako cha mataahira walikufanya uwe busy nini?,kwenye mkato unaunganisha sentensi,ghorofa,unaandika gorofa,sekondari ulisomea shule ya kata ya TAWA nini??,kajifunze vizuri kuandika hati za kiswahili halafu ndio uje tena uongee na mimi,umesikia daktari feki wewe?
 
Back
Top Bottom