TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,673
- 1,571
Mheshimiwa mkuu wa wilaya heshima nyingi pia natumai umzima kiafya.
Ama baada ya salamu, nikupe pole kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya wilaya hii. Ndiyo, pole. Pole kwa kuwa nafahamu changamoto ambazo utaenda kukutana nazo katika wilaya hii. Labda nikwambie tu, wilaya hii nahisi ndiyo wilaya yenye vichekesho vingi kuliko wilaya nyingine yoyote ile.
Baadhi ya vituko hivyo ni kama ifuatavyo:
1. WILAYA HII OFISI ZAKE ZIPO KATIKA WILAYA NYINGINE.
Kifupi majengo yanayotumiwa na wilaya hii yapo katika halmashauri ya manispaa ya Morogoro hivyo hakuna jengo la halmashauri ndani ya wilaya husika.
2. HAKUNA HATA MITA KUMI ZA BARABARA YA RAMI.
Hii ni moja ya wilaya ambayo toka uhuru awajawahi kuona hata kipande cha mita kumi za rami pamoja na umuhimu wa eneo la morogoro vijijini kwa kuwa na eneo kubwa la ardhi inayofaa kwa kilimo.
3. HAKUNA HATA SHULE MOJA YA SEKONDARI YA JUU (ADVANCE LEVEL)
Katika wilaya hii hakuna hata shule moja ya sekondari ya juu yaani advance level. Shule kongwe katika wilaya nzima ni Matombo sekondari.
Ila, karibu na usiogope
4. HOSPITAL YA WILAYA KITUKO.
Hospitali ya wilaya ipo sehemu moja inaitwa Tawa naamini watakupeleka na utaiona wewe mwenyewe. Kama ingekuwa Dar es salaam naamini ningeifananisha na kituo cha afya cha tabata au Tandale kwa mtogole.
Ila karibu usiogope, tutakupeleka
5. UKUBWA WA WILAYA YENYEWE NAYO NI CHANGAMOTO
Kijiografia wilaya ni kubwa yenye vijiji vingi ambavyo vingine havifikiki kirahisi. Vijiji vya Nyingwa, Lanzi, Lumba, Kitengu, Dehele, Mwangazi na kiunza. Vijiji hivi nilivyokutajia, kuna watu wanakufa hawajawahi kuona gari. Kuna maeneo mengine sijui hata kama serikali yenyewe kma inayatmbua.
Ila karibu usiogope tutakupeleka.
Tafadhali ukija huku, acha ujuaji shirikina na watu, nakwambia hivyo kwa nia njema tu, kwa kuwa nawajua watu wa huku vizuri pengine kuliko wewe.
Karibu sana mheshimiwa, karibu mkuu wa wilaya. Labda wewe unaweza ukawa tumaini jipya la wilaya hii, maana hawa wabunge wamepita wengi hatujawa na manufa nao.
Wakuu wa wilaya nao wengi walikuwa ni wale wale.
Ni mimi mwenyeji wako.