Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais

Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais

Mzee wa Ndogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
204
Reaction score
79
Kwanza napenda kukupa pole kwa kazi ngumu ya kuendeleza nchi yetu.Pili nakupa pole kwa umakini wako katika kujenga Chama Tawala ili kiendeelee kutupatia kile kilichodhamiria.

Jana nimesikiliza hotuba yako kuhusu ilani ya Chama Chetu na Utekelezaji wake..nawapa Pongezi wote wanaofanikisha hili.

Nimepata shida kidogo pale uliposema wapinzani hawana cha kusema watasema Uongo kwa sababu kila kitu kipo sawa...Mheshimiwa Raisi hivi tumewahi kufikiria kwa nini upinzani umekuwa kwa kasi kipindi hiki?Nikusaidie tu.

Kuwa Mpinzani si kwamba watu wanapenda,la hasha ni kwa sababu ya mambo yafuatatyo:

Huduma Mbovu za Jamii.

Miundombinu Duni

Mfumuko wa Bei wa bidhaa mbalimbali

Hali mbaya ya maisha ya Mwananchi wa kawaida.

Rasilimali zisizotufaidisha kabisa.

Ufisadi pamoja na Rushwa

Unyanyaswaji wa Wananchi na Chombo cha Usalama(Polisi)

Huduma Uchwara katika baadhi ya taasisi za Serikali

Na Nyinginezi nyingi tu...

Sidhani si swala la kijidai kwamba tuna Umeme katika baadhi ya vijiji au Usafiri wa Treni Dar es salaam.

Haya mambo nadhani tulitakiwa tuwe nayo zamani na wala si sasa...Tanzania hii si ya kupambana na ujenzi wa barabara au shule ...Tanzania hii ilipaswa iwe beyond than that kwa rasilimali mbalimbali tulizonazo kama tungekuwa na mikakati ya ujumla na wala si ya kushibisha matumbo yetu.

Mheshimiwa Raisi najua una kazi nyingi za Ujenzi wa Taifa lakini naomba ujipe muda utafakari na kujiuliza ni wapi tumekosea?Wapinzani si wa kukejeli na wao ni chachu yetu kwa ajili ya kuleta maendeleo Nchini.

Tumefika wakati mpaka tunamsikiliza Shibuda?huoni Mh Shibuda kama ni mtu asiyejitambua?hajui anazungumza nini?kwa ufupi ni Mropokaji.

Nakutakia kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yako na Mwenyezi Mungu akujaalie afya Njema.
 
Barua nzito hii na ina mapendekezo ya msingi sana.
 
Ni kweli lakini umekosea sana kumpa pole kwa ujenzi wa taifa! je, ni taifa lipi analolijenga yeye?
 
Wanachama wote mjiulize,sio ajiulize mwenyekiti peke yake
 
Kikwete ni mwiba kwa wenye husuda na chuki na taifa hili
 
natamani waangamie wote kama walivyo pale dodoma...kizazi cha magamba kipotee

mungu akulaani kabisa kwa dua yako ya husuda na chuki kwa watanzania wenzako. Tutofautiane kwa hoja
 
Kikweke ni rais bora au bora rais? kama Leo yaani wengine wanacho sema ni uongo tu ilimradi wapate misifa! mi c chukii ccm nachukia baadhi ya viongozi wake!
 
Kwanza napenda kukupa pole kwa kazi ngumu ya kuendeleza nchi yetu.Pili nakupa pole kwa umakini wako katika kujenga Chama Tawala ili kiendeelee kutupatia kile kilichodhamiria.

Jana nimesikiliza hotuba yako kuhusu ilani ya Chama Chetu na Utekelezaji wake..nawapa Pongezi wote wanaofanikisha hili.

Nimepata shida kidogo pale uliposema wapinzani hawana cha kusema watasema Uongo kwa sababu kila kitu kipo sawa...Mheshimiwa Raisi hivi tumewahi kufikiria kwa nini upinzani umekuwa kwa kasi kipindi hiki?Nikusaidie tu.

Kuwa Mpinzani si kwamba watu wanapenda,la hasha ni kwa sababu ya mambo yafuatatyo:

Huduma Mbovu za Jamii.

Miundombinu Duni

Mfumuko wa Bei wa bidhaa mbalimbali

Hali mbaya ya maisha ya Mwananchi wa kawaida.

Rasilimali zisizotufaidisha kabisa.

Ufisadi pamoja na Rushwa

Unyanyaswaji wa Wananchi na Chombo cha Usalama(Polisi)

Huduma Uchwara katika baadhi ya taasisi za Serikali

Na Nyinginezi nyingi tu...

Sidhani si swala la kijidai kwamba tuna Umeme katika baadhi ya vijiji au Usafiri wa Treni Dar es salaam.

Haya mambo nadhani tulitakiwa tuwe nayo zamani na wala si sasa...Tanzania hii si ya kupambana na ujenzi wa barabara au shule ...Tanzania hii ilipaswa iwe beyond than that kwa rasilimali mbalimbali tulizonazo kama tungekuwa na mikakati ya ujumla na wala si ya kushibisha matumbo yetu.

Mheshimiwa Raisi najua una kazi nyingi za Ujenzi wa Taifa lakini naomba ujipe muda utafakari na kujiuliza ni wapi tumekosea?Wapinzani si wa kukejeli na wao ni chachu yetu kwa ajili ya kuleta maendeleo Nchini.

Tumefika wakati mpaka tunamsikiliza Shibuda?huoni Mh Shibuda kama ni mtu asiyejitambua?hajui anazungumza nini?kwa ufupi ni Mropokaji.

Nakutakia kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yako na Mwenyezi Mungu akujaalie afya Njema.

Pamoja na hayo umesahau safari za kila siku za raisi(omba omba)bila kuwa na tija unachopata huko hakifikii unachotumia kwenda kuomba
 
Umesahau moja la muhimu angeachia ngazi ya Uenyekiti ili kidogo awe mkali kwa wala rushwa,wapokea rushwa,mafisadi na wahujumu uchumi wetu wote walio ndani ya Chama Chetu Cha Chukua Chako Mapema.
 
huu waraka ataupata nadhani baada ya mwaka mmoja kwa jinsi alivyo busy na kujiandaa na safari za hapa na pale kupitisha bakuli la misaada isiyotuneemesha zaidi ya kutuongezea madeni mpaka uvunguni.
 
Pole kwa lipi? kodi za wananchi zinaliwa, upinzani utazidi kusema ukweli, wilaya ya nzega madini yanaenda ulaya wakati hospitali ya wilaya haina x-rays, maji nzega hakuna,barabara mbovu, natamani kusia muda wa jk uishe hata kesho
 
Back
Top Bottom