Barua ya wazi kwa JPM- Sheria ya Bodi ya Mikopo ya mwaka 2016

nimekluelewa unapodai kua kuna asilimia 6% za kuongezeka kwa deni kila mwaka kitu amacho sio sahihi hata kidogo, na hata mdau mwingine amekuelewesha kua baada ya kuanza kulipa hakuna extra costs nyingine kama umeshaambiwa deni lako ni milion 16 ndio hizo utakazolipa kwa kipindi hicho. sasa hoja yako sijui ni ipi hapo. mana unajaribu kuaminisha watu kua deni litaongezeka kila mwaka kiasi kwamba litakua deni la maisha. wacha kupotosha watu, deni linatakiwa kulipwa ili wengine nao wanufaike pia. Pia uelewe kwamba kwa kupitia uchambuzi wako huo unaweza ukafanya mtu akaacha kuomba mkopo ilihali sio kweli kabisa na ungemsaidia na angelipa na vizuri tuu na maisha yangeendelea. tatizo tulitaka tusilipe kabisa ndio shida inapokuja. kama sheria umeona ina shida leta hapa hicho kifungu tukijadili ili kisije kikaanza kutumika vibaya ila usidanganye na mfano ulioutoa ni wa uongo kabisa.

Nakushauri uendelee kujifunza au fuatilia vyema hiyo sheria ya 2016.

Sio ujinga kutokujua. Ujinga ni kuzungumzia kitu ambacho hujafanyia uchunguzi kwanza kujua kinachozungumziwa kina uhalisia.

Na wasio jua sio Wewe tu, ni wengi sana.

Na hicho ndiyo kinasikitisha zaidi.
 
nimeanza kulipa mkopo tangu ikiwa 8% sijui 6% na hata ilipokua 15% nimeendelea kulipa, sijaona unachokisema mkuu. labda kuna baadhi ya watu wanafanyiwa hivyo ila sina uhakika. ila kwa mwendo huo mambo yangekua magumu sana. kila mtu angeona hicho kitu ila sijaona bado wacha muda utaongea zaidi.
 
Kwako John,

Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao . Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA Yaani watoto wa maskini.

Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria ANGAMIZI kwa watoto maskini.

Sheria imeweka wazi ( Watz wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.

Kwa mfano.
Daktari ambae amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30.

Basic salary yake ni 1.5 Mil
Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo,

Helsb 225, 000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension. 80, 000

Total deduction 642, 510 TSH
take home yake ni 857,590 TSH —ana watoto na anasomesha!
-----------------------------

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil ( 225,000X12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil , atakuwa amepunguza deni lake hadi 27, 300,000TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27, 300, 000 TSH.

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000+ 1.8 Mil sawa na 29, 100, 000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambaye ni 1.8

Hivyo 26,400,000+ 1.8 mil

Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.

Yaani, Ikiwa una pension ya 15 Mil , na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi,maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out , ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni , ni deni la maisha hasa waliosoma makozi ya sayansi kama udaktari, Nesi, famasi , na injinia na wale waliosoma nje ya nchi.hawa wote madeni yao si chini ya 25Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.

Mapendekezo

1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika na hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu maredioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato WaTZ wengi haijui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu itolewe kwa Sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli ? Doh tutapata laana katika nchi.

USHAURI.

1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho, hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake, you need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akuelewesheni ni hatari sana fuatilieni haya mambo.

Rais JPM tunaomba ufanyie kazi hayo mapendekezo kwa heshima na taadhima .

Wako Raia Mwema.
Kamanda maoni na ushauri wako uko vema

1. Nakubaliana na wewe kuwa wazazi ambao wana uwezo wasiwaruhusu watoto wao waingie kwenye mikopo hii.

2. Nakubaliana na wewe pia hii kitu inaitwa Value Retention Fee inayotozwa 6% iangaliwe kwa maana ya utaratibu wa kuikata au kuikokotoa.

Hata hivyo,
1. Kuhusu hiyo tozo ya asilimia 6 ninavyofahamu ni tozo kwenye 'outstanding balance'. Kwa hiyo ukilipa, hiyo 6% sio kwenye principal loan. Ingekuwa hivi, hakungekuwa na waliomaliza madeni yao pale HESLB.

2. Kuhusu pensheni, ikiwa mnufaika atafuata matakwa ya sharia na kuanza kurejesha ndani ya miaka miwili baada ya kuhitimu, anaweza kumaliza ndani ya miaka kumi - maximum. Sasa, wengi tunajificha, tunakimbia na tunakuja kukutana na deni lishakua kubwa na penalty juu. Waajiri wasomeshe wafanyakazi wao kwa bajeti zao na kupitia mipango ya mafunzo ili wafanyakazi wasikope HESLB.

3. Kwa mwaka 2018/2019, waombaji mikopo ya HESLB umri wa juu ulikua miaka 33 na kwa 2019/2020 umri wa juu ni miaka 35, kwa hiyo mnufaika anaweza kumaliza akiwa na 40 kama amesoma degree ya miaka mitano. Bado wale madogo wanaomaliza form VI na miaka 20 na akasoma degree ya miaka 5 anamaliza na miaka 25. Ana grace period ya miaka mwili, ananza kulipa na miaka 27, anaweza kumaliza deni na miaka 32.

4. Kuhusu makato ya asilimia 15 kushuka hadi 8 au 10, hili tujadiliane. Lakini, mimi nikikatwa asilimia 15 na nikamaliza deni mapema naona ni bora kuliko kukatwa hiyo 8 kwa muda mrefu.

Ila Kamanda, haya maoni naamini jamaa wa Bodi wameyapata na watayafanyia kazi. Na waongeze kutoa elimu, tusije ingia chaka.
 
Yes, 6% ni Kwenye outstanding balance. But the point here is that, kui apply hiyo 6 % kwa kila mwaka hata kama umeanza kulipa deni lako, is it fair? Au hiyo sheria imewekwa kwa mantiki ganj ?

Maana 6% inalipwa kila mwaka mpaka unamaliza deni lako
 
Mkuu, naomba nipatie mbinu ya kumpata huyo dancer kwenye avatar yako niweke kwenye whatsapp yangu
Bila bumu nisingeweza kusoma so naishukuru sana bodi kwa hilo, ila baadaye nilikuja ‘kukengeuka’ na kuona hilo deni ni kubwa mno bora niache kuajiriwa kuliko kukatwa nitumike bure.... hiyo ni pesa pekee ya serikali ambayo kama raia nimeifaidi so kama hakuna namna nyingine ya kuniwajibisha nje ya ajira naomba tu tusisumbuane.
Serikali siwadai ajira ili wanilipe mshahara, nami msinidai bumu tufanye kama nimechukua GAWIO langu kama raia mwema.... win-win situation na kwa kweli sina mpango wa kulipa.
 
Mkuu nikusaidie kidogo uzoefu maana tunalingana miaka ya kumaliza chuo.
Mimi nilimaliza chuo 2013 bba accounts. Wakat namaliza deni langu lilikuwa milion saba kama na nusu hivi maana nilipata mkopo only 40%. Kisha nikasugua gaga mtaani 3 good years. Mwaka 2016 january nikaajiriwa taasisi flan hiv. Hiyo taasisi ukiajiriwa utake usitake ndan ya miez 3 unaanza kukatwa deni kama ulisomeshwa na bodi.
Napewa barua ya kisaini kuanza kukatwa naona deni limepanda from 7m to 10m. Kucheki kumbe kila mwaka baada tu ya kumaliza chuo wanaongeza 1m. 10% ambayo ni laki 7penalty na laki 3 na kiduchu ndio hiyo value retention jumla 11 kasoro kama laki 2 hiv. Ila nashukuru sasa bado kama 4m nimalize ambapo baada ya miaka 2 na nusu nitamaliza, ila daah si mchezo hiyo 15% maana ukijumlisha makato yote ni 44-50% ya mshahara wanaondoka nao serikali.
Mkuu, angalia kiasi kilichobaki halafu kaulizie bodi wakuambie unadaiwa bei gani.

Niko government. Nilikatwa kwa miaka 2 mfululizo na salary slip ikawa inasoma kiasi kidogo tu. Nilipokwenda kutaka statement ili niiuzie benk mkopo nikakuta wameongeza hela ndefu tu. Nilipokaa nao wakaniambia hiyo ya juu ningeanza kuilipa baada ya kumaliza ninayoiona kwenye salary slip.

Nilichoka balaa.
 
Dawa ya hiyo bodi ya mikopo ni kuwaacha tu wakate hela yao ya kwenye salary slip hadi pale deni lao litakapokwisha.

Hata mimi walipo nipandishia makato hadi kufikia hiyo 15% nilishangaa nilipowatumia email kujua deni langu ili nilipe ikibidi (maana hayo makato yanaumiza sana); nikajibiwa deni tofauti kabisa na lile la kwenye salary slip! Salary slip ilikua inasoma milioni moja na point ya deni lililobaki halafu wao wakanijibu nadaiwa milioni tatu kasoro!

Nilichokifanya ni kuwapuuzia tu na nikavumilia. Deni lilipoisha tu kwenye salary slip, na makato yao yakasitishwa. Hata hizo takataka zao nyingine za rentation fees sijui walizonibambikia hata sikulipa. Nb: Rai kwa wazazi/walezi; Kama uwezo unaruhusu, ni bora mara mia kugharamia ada ya chuo kwa unayemsomesha ili tu kumkomboa na huu unyonyaji unaofanywa na bodi siku za usoni.
Mkuu, kama uko serikalini usishangae unaanza kukatwa tena.

Kwa maelezo yao ni kuwa, barua za ongezeko la deni baada ya sheria mpya zimeshatumwa manispaa/halmashauri. Kwa hiyo wataanza kukukata tu.

Aidha, watakubana kwenye mafao, labda ufe
 
Hahaha, nilishaiuzia benki moja hivi.
Mambo ya bodi sio kabisa
Nasikilizia maumivu ya benki lkn najua ndani ya muda fulani nakuwa nimemaliza, sio mauzauza ya loan board.

Dancer angenipunguzia maumivu mkuu:cool::D

Dancer anakodishwa bei nafuu, mikoani tunatuma pia.... kwa maelekezo zaidi niPM.
 
Mkuu, kama uko serikalini usishangae unaanza kukatwa tena.

Kwa maelezo yao ni kuwa, barua za ongezeko la deni baada ya sheria mpya zimeshatumwa manispaa/halmashauri. Kwa hiyo wataanza kukukata tu.

Aidha, watakubana kwenye mafao, labda ufe

Sisi wakati tunasoma ada ilikuwa ni laki 6 tu na point kwa mwaka! Boom 2500 kwa siku! Hata wafanye hujuma kiasa gani, hilo deni haliwezi kuvuka mil.2! Isitoshe nilianza kukatwa tangu 2011 kabla ya hiyo sheria yao kandamizi kuanza.

Ole wao wanikate makato yasiyoeleweka kwenye huo mshahara kiduchu ninaoupata; Maana awamu hii inatafuta hela kwa nguvu kwa kuwaumiza wananchi kutokana na kupumulia kwake mashine; Ninajitambua! Nitaongeza % zaidi za kiwango cha kuzingua kazini kuliko hizi za sasa.
 
Mkuu, kama uko serikalini usishangae unaanza kukatwa tena.

Kwa maelezo yao ni kuwa, barua za ongezeko la deni baada ya sheria mpya zimeshatumwa manispaa/halmashauri. Kwa hiyo wataanza kukukata tu.

Aidha, watakubana kwenye mafao, labda ufe

Hili swala Wengi hawajui maskini. Yaani barua zimeshasambazwa kote. Na ukimsumbua muajiri wako anakuambia Nenda bodi, Mimi nafuata maelekezo tu. Malalamiko peleka bodi.

Ukifika Bodi wanakuambia Hii ni sera, haiwezi kubadilishwa.

Unapigiwa calculations za ajabu na kupewa balance yako.
 
IMG_9593.JPG
 
Mkuu hiyo sheria anaijua tu vyema na imetungwa katika utawala wake na yeye mwenyewe ndo ali i sign akijua kabisa ni sheria kandamizi.....huyu mtu kwa anayotufanyia ni kumwacha tu atufanye anavyotaka lakini najua mungu siku moja atashughulika naye ipasavyo
Mungu aje ashughulike naye wakati kura tummempa wenyewe?
 
Sio kwamba hyo 6% inaongezeka kama unakua haujaaanza kukatwa. Yaan grace period ikiisha ndo hyo 6% inaanza fanya kazi. Once ukianza kulipa, ongezeko la 6% linastop. Ndivyo nijuavyo au wamebadilisha?
Hakuna grace period.
 
Hahaha, nilishaiuzia benki moja hivi.
Mambo ya bodi sio kabisa
Nasikilizia maumivu ya benki lkn najua ndani ya muda fulani nakuwa nimemaliza, sio mauzauza ya loan board.

Dancer angenipunguzia maumivu mkuu:cool::D

Inawezekana vipi ?

Maana mfano CRDB riba yao kwa mwaka ni 17% . Loan bodi ni 6% kwa mwaka

Sio kwamba umeongeza mzigo ?
 
Anayeuliza kwamba kapata mkopo kabla ya sheria haisaidii,umeambiwa 6% itaanza kutumika kuanzia tarehe iliyoanza kupokea pesa so hata iwe kipindi cha boom la 2500 kama hadi wanafunga sheria ulikuwa hujamalizana na bodi hii inakuhusu
Hapa aidha ulipe kwa mkupuo au wapunguze riba au sheria ifutwe,Nakushukuru mtoa mada umenifungua macho
wale mnaosema hamtaajiliwa wakati taarifa za wapi mliko zitapatikana kwa data base via usajili wa fingerprint,simu,identity ya taifa,kura,benki,leseni,TRA etc labda uwe mkulima huweki pesa m pesa au bank etc
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Nimesikitika sana daktari anasoma miaka 4 hadi 5 huku ada yake ni kubwa kwa mwaka afu analipwa salary pungufu kidogo ya Technician wa civil aliyeko Tanroads 1,118,000 huku alizidiwa na Injinia aliyesoma miaka 4.Huu upangaji wa salary hauwatendei haki madaktari
 
Back
Top Bottom