mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,577
- 11,202
Mkuu! Rejea kichwa cha thread hapo juu. Naamini kuwa u mzima wa Afya hapo magogoni.
Naamini kuwa u mzima wa afya sisi huku sio wazima ndio maana tukaamua kukuandikia barua hii kupitia kwa Mtwa mkulu. Mkuu twaamini pia kuwa ama wewe ama watu wako wa karibu wataiona barua hii ya simanzi hivyo ipo imani kwamba itakufikia. Lengo la barua hii ni kueleza jambo ambalo ni very serious! Ni hasara kubwa ambayo serikali yako imeingia na vifo vya zaidi ya watu sabini. Kutokana na unyeti wa suala hili mtiifu raisi nakuomba uupate ujumbe huu mpaka mwisho na mods msiuondoe huu uzi ni taarifa za moja kwa moja kutoka mgololo Mufindi.
Mkuu tulikuwa wadogo japo nakumbuka kuwa katikati ya 2002-2003 serikali yako chini ya rafiki yako Benjamin Mkapa na Frederick sumaye waliuza kiwanda cha karatasi mgololo kwa Rai groups.
Mkuu! Ikumbukwe kuwa kiwanda hiki kilipata kuwa kiwanda kikubwa zaidi afrika ya mashariki na Kati, Kwa uzalishaji wa karatasi bora kilikuwa cha tatu kwa umashuhuri kikitanguliwa na kile cha South Africa na kile cha Norway. kwa fedha za ufadhiri na kwa fedha za wavuja jasho wakulima wa Tanzania Mwalimu Nyerere alidunduliza na kutumia nguvu kubwa kutengeneza kiwanda hiki .
Mkuu;
Ukirejea kumbukumbu za wizara ya Viwanda na masoko utaona serikali ilitangaza Mara ya mwisho bei ya kiwanda hiki kuwa ni kiasi gani lakini kiliuzwa kwa bei sawa na bure M30 tu! Kama sita kuwa sahihi utanisamehe kwani taarifa hizi ni Nyeti mno zilifichwa na serikali zilizotangulia lakini ninachojua kuwa hata kiasi hicho hapo juu hakikulipwa chote asilimia kubwa wali apply kwa mkopo na kuahidi kulipa kwa awamu.
Mkuu;
kumbuka kuwa Fedha tajwa hapo juu ilikuwa ni kwa kiwanda tu! Hivyo basi kile kijiji cha wafanyakazi chenye hekari kadhaa na Nyumba zaidi ya 600 alipewa bure! Pia Eneo la kijiji Camp ya sawala Yenye heavy machine like cartapilar na Garage kubwaa! Nyumba zaidi ya 50 nayo alichukua bure!
Lile shamba la hekari 18,000 kumi na nane Elfu ambalo mwalimu alitarajia siku tukipata akili tutapanda miti nalo pia tuligawa buree!
Sijaongelea Ofisi watu na miundombinu iliyokuwa dar es salaam kwani sijaiona na sitaki kuandika uongo. Rejea huo mkataba unauozo wa kutisha!
Mkuu:
Mkataba huo pia unaonesha kuwa asilimia Saba ya kiwanda kina milikiwa na Rai group, asilimia tatu serikali na Zaidi ya asilimia tisini anamiliki (zimwi) Nimemuita zimwi kwakuwa anaye miliki asilimia hizo hajawahi tajwa ama kuonekana. Hayo juu ni baadhi tu tuliyoweza kukutajia(Nakushauri uwasiliane na Zitto kabwe kuhusu huu mkataba kwani kunataarifa kuwa aliwahi kuonekana pale akiwa POAC kwa shughuli ambayo haijafahamika) Nimezungushia kwakuwa ni tetesi wasiliana na Zitto kwa uwazi.
Mkuu; Sehemu ya barua inayofuata Nakuomba uizingatie, Mungu akupe moyo mgumu wa kusoma na Machozi yawe mbali. Ni mateso shuruba na vifo Vya watu hayo halo juu ni yenu serikali. Mwaka 2005 wafanyakazi mgololo waliitisha mgomo kutokana na kazi za shuruba zinazoendelea mpaka hivi Leo ,fedheha na madai ya mshahara. Serikali ya mabavu haikuwafumbia macho iliwapiga na kuwatesa na kwakushirikiana na Muhindi wafanyakazi zaidi ya 800 walioshiriki mgomo walifukuzwa kazi. Iliripitiwa kuwa hakuna vifo vilivyotokea japo tunajua kuwa Mr Kilumile alifia Guest Makambako akijaribu kukimbilia nyumbani kwa wazazi wake ilembula. Nesi mwingine alipatwa na mshituko na kufariki siku chache baadae.
Wafanyakazi hawa wanasifika kwa uvumilivu
mwaka 1998 waziri Kigoda aliwatukana kwamba "hawajasoma" siku ya mabomu muhindi aliwaita Mbwa. Kwa uaminifu mkubwa wakati kiwanda hiki kimefungwa na serikali wazee hawa walilinda na kutunza kwa uaminifu miundombinu ya kiwanda hiki pasipo upotevu! mwisho wao ukawa huu shaaame!
Baada ya kufukuzwa baadhi wamerejea mikoani makwao na akumbukwe yule aliyerejea bukoba!
Wanachokidai wazee hawa mpaka sasa ni mafao! malipo yao ya halali. Serikali yao sikivu haijawalipa mafao yao hivyokuwapa kipindi kigumu cha maisha wazee hawa.
Kuna makala niliwahi kuisoma ilielezea kuwa mpaka mwaka 2013 wafanyakazi zaidi ya 50 walikuwa wamefariki dunia kutokana na maisha magumu baada ya sakata la 2005. Agharabu idadi hii ilipanda ghafra kufikia vifo 76 mwaka 2015. jambo hili utakubaliana nami kwamba halina mkono wa Mungu! Nakumbuka katika bunge lililopita kwa roho ya kimama bi. Magreth sakaya (MB) aliuliza kuhusu hali ngumu ya wazee hawa hata hivyo serikali sikivu ilionesha bado bado inafanya Tathmini ilikuibuka na mipango na mikakati yenye Sera madhubuti za kuwakwamua wazee hawa.
Katika jitihada nyingine mbunge wa mufindi kusini alidanganya kuwa angeitisha maandamano makubwa kwaajili ya wazee hawa jambo ambalo halijafanyika.
HUZUNI WAKATI WA UCHAGUZI
Mkuu wazee hawa kwa muda mrefu ni wanazi na wakereketwa wa chama tawala wengi wao.
Mwezi october mzee mmoja alitishia kumfukuza nyumbani mwanae ikiwa hata mpigia kura mpinzani.
Mama mwingine akiwa mgonjwa alijikongoja mpaka kituo cha kupiga kura. Aliweza kupeleka kura yake UKAWA ndipo aliposhinda kustahimili alianguka na kupoteza fahamu. mpaka mwisho nafatilia simulizi ya mama huyu kinamama masikini wa mgomo walikuwa wakidunduliza chochote kitu kupigania uhai wa mama huyu zahanati. sidhani kama atakuwa hai!
Mzee mwingine alisema kuwa ni laana kubwa kuipa CCM Kura kwani bila sababu ya msingi amefukia wazee wenzie zaidi ya sabini udongoni!(alieleza kwa ghadhabu na huzuni ya wazi)
Hali inatisha kwa wafanyakazi wa SPM Mgololo. Watu wanakufa kinyama! Watu wanaitamani kesho ama wafe ama uwape mafao yao. Hayo mazuri unayoyafanya Darisalama hayawaingii akilini.Ukisema unatumbua majipu wanapata hisia kanakwamba ujatumbua macho yao kwa upanga wa makali kuwili.Ukijiita Tingatinga wanahisi Scania ya magogo inatembelea vifua vyao!
ukitamka hapa kazi tuu! Unasadifu kazi za shuruba wanazo zifanya kujipatia fedha za madafu japo miili yao wengi wanaumwa. Mkuu katika uchunguzi zaidi niligundua kuwa makamo wako wa Raisi mama Suluhu analitambua vyema hili swala. Katika Campein zako alilitumia suala hili kuombea kura kijiji cha mtwango. Alisema kuwa analitambua hili swala ni mgogoro wa siku nyingi na Ikiwa wanakijiji wa Mtwango wangewapa kura Basi serikali ya awamu ya Tano itawalipa. Mtu mmoja aitwaye kibiki akamwambia kuwa iwapo mtatekeleza mtakuwa mmesaidia sana. Mkuu ni lini mtashughurikia hili suala ambalo ni ahadi yenu katika campain?
Haya ni machache chunguza muheshimiwa utayajua mengi!BADALA YA KUTUMBUA VIJIPU DARISALAMA GEUKIA NA HILI Limewiva kiasi cha kutoa uvundo!
wako mtumbji mwenzio Mtwa Mkulu Mnyakilambo Mkwamisi
Rejea GAZETI JAMUHURI Makala "utata wa gubika mkataba kiwanda cha karatasi mgololo
Rejea kumbukumbu za bunge lililopita yaani Hansadi kuhusu kiwanda cha karatasi mgololo. shukrani!

Attachments
Last edited: