Barua ya pole kwa mzee Sumaye

Barua ya pole kwa mzee Sumaye

Sasa kamwambie dikteta uchwara naye na mafisadi wenzie wote warudishe nyumba za Watanzania walizokwapua yeye akishirikiana na fisadi Mkapa na mafisadi wengine ndani ya Serikali ile ya kidhalimu.

upload_2017-6-13_14-5-10-jpeg.565291
Ndio ameshaanza hivyo!
 
Salaam nyingi
Mzee wangu kwa niaba ya wanyonge wenzangu nakupa pole kwa yote yanayokukuta tangu uhame chama cha kidhalimu na kuingia chama cha wanyonge,yamekukuta mengi mzee kunyang'anywa mashamba bila kufuata taratibu duh ni unyama ulioje kwa serikali dhidi ya raia wake,

Pamoja na yote mzee wangu labda nikuulize lile shamba wewe hukudhulumu maana muosha nae huoshwa sasa kama wewe ulichukua kibabe kwa kujisainia hati mwenyewe ni kosa najua wewe sheria ya ardhi unaijua ni mali ya serikali hivyo wameamua kuchukua kilicho chao

Nakumbuka yale maneno yako ukitaka mambo yako yakunyokee weka bendera ya CCM najua ulipitiwa,mzee kipindi cha utawala wako watu walilia na kusaga meno kwa kudhulumiwa mashamba na viwanja na nyinyi mlitoa matamko mazito kisa tu waliofanya uovu ni washirika wenu na nyinyi wenyewe

Nakumbuka kuna ndugu yangu alipoteza maisha Bulyanhulu ni kipindi cha uongozi wako lakini hukuchukua hatua na wale walidhulumiwa,labda nikuulize mkuu wewe ukiwa ni kiongozi mkuu wa serikali ulipataje ardhi yote ile bila ya dhuluma pole mzee wacha wachukue vyao

Mzee wangu hivi lile shirika la ndege ilikuaje,nikupe angalizo tu ukiingia pale ofisi kwetu omba kumbukumbu ya hotuba za nyuma tuliahidi tukichukua nchi cha kwanza ni kuwang'anya ardhi mafisadi wote wa CCM.

Mzee mbona umekuwa muoga wa sindano namna hii mwenzio Lowassa anagugumia kiutu uzima.

Kumbuka atakayeua kwa upanga nae atauawa kwa upanga.

Pole mzee
Acha aisome namba....
 
Mimi hili siwezi kulishangilia manana,
Ubaguzi ni Kama kula nyama ya mtu.
Kauli ya rais ilisema tuwaache wazee wetu
Wapumzike, wamelitumikia taifa hili
Swali langu ni je, ukihama ccm unakuwa kijana?
Au utumishi uliotumikia taifa unayeyuka?
 
Mimi hili siwezi kulishangilia manana,
Ubaguzi ni Kama kula nyama ya mtu.
Kauli ya rais ilisema tuwaache wazee wetu
Wapumzike, wamelitumikia taifa hili
Swali langu ni je, ukihama ccm unakuwa kijana?
Au utumishi uliotumikia taifa unayeyuka?
Wacha tuone ni nani atakaefuata!
 
Back
Top Bottom