Barua ya mwisho toka kwa mwanangu Chambondala (NIFANYEJE WADAU?)- PART I | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya mwisho toka kwa mwanangu Chambondala (NIFANYEJE WADAU?)- PART I

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mkulungwa, Feb 22, 2011.

 1. m

  mkulungwa Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwako Baba mpendwa shikamoo!!
  Salamu zangu kwenu nyumbani, mimi ni mzima hofu ni kwenu mlio mbali na upeo wa macho yangu!!
  Dhumuni la barua hii ni kukushukuru kwa yote ambayo umekuwa ukinifanyia katika maisha yangu, pia nataka kutoa sononeko langu kuhusu maendeleo yangu kimasomo; Baba naomba unisamehe sana kwani matokeo yangu tangu nije hapa shuleni sio mazuri. Taarifa ya muhula uliopita nimeshika nafasi ya kumi na tisa (19) kati ya wanafunzi ishirini (20). Nimepata wastani 80%, nisamehe baba nitajitahidi zaidi.
  Baba, Kuna mambo ambayo yamesababisha nipate alama hizo naomba uangalia ni jinsi gani utanisaidia kuyatatua:-
  i.[FONT=&quot] [/FONT]Ukosefu wa masomo ya tuition (ziada) niwapo shule na pale niwapo likizo. Wenzangu wote hapa shuleni hulipiwa masomo ya ziada wakiwa likizo na mara warudipo shuleni huwa wameshamaliza kusoma ‘angle’ zote za mitihani. Huko huwa wanasolve papers zote na walimu wetu hutoa mitihani toka kwenye past papers.
  ii.[FONT=&quot] [/FONT]Ukosefu wa marking scheme. Baba taka usitake mfumo wetu wa mitihani siku hizi ni wakurudishia maswali ya miaka iliyopita (hakuna maswali mapya). Ukininunulia vitabu kama ufanyavyo wewe, unanipotezea muda kwani mpaka nisome nielewe concept ni muda mwingi sana!! Ukiwa na marking scheme unakariri waswali na solutions zote mpaka ushibe, baada ya hapo inabakia kucheua tu kwenye paper. Baba kama huniamini naomba waulize kina daria wanaosoma shule zinazoongoza Tanzania, hivi ndivo wanavyosoma na ndio maana wanarudia shule zile zile tu. Ukiwaleta huku hawawezi kitu.
  iii.[FONT=&quot] [/FONT]Ukosefu wa walimu wazuri wa English; unajua baba mitihani yetu tunafanya katika lugha ya English, shule yetu haina walimu wazuri wanaoongea kingereza safi, wengi wao wanagongea tu huku wakifumba macho. Wanaeleweka na kujitahidi sana baba, lakini inatufanya sisi tusiongee kwa mapozi. Please baba nipeleke shule za international nikaboreshe lugha nami personality yangu ikae juu. Kwani hutaki mwanao nionekane msomi niongeapo?
  iv.[FONT=&quot] [/FONT]Shule yetu kutokuwa katika kumi bora ; nadhani hili baba umeshuhudia kupitia matokeo ya form four. Inaniuma sana kwani inatufanya tukitembea mjini tusiheshimike. Ningesoma Maryan nahakika kwa nafasi yangu hii hii ningetesa bongo.
  v.[FONT=&quot] [/FONT]Ukosefu wa laptop baba. Hii sasa ni kitu muhimu sana, ule wakati wa kusoma vitabu vikubwa kama Nelcon, Lambart nk umepitwa na wakati. Siku hizi mambo yapo kwenye mtandao, ukibofya tu mambo kede kede unanyonya unatemea tu kwenye assignment. Wenzangu hawakeshi tena sasa. Pia twitters facebook usiseme.
  Baba najua nimekuchosha kwa mahitaji yangu mengi, nakuomba uyaangalie kwa umakini wake unitatulie yale ambayo kwako yanaingia akilini kwani nakuaminia baba yangu kwa mbinu zako za kujitetea.
  With love and care,
  Mkamba Chambo(mtoto wa mwisho)
  N.B baba elfu tano kwa siku haitoshi maisha magumu weka angalau book 10.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  daaah umenifurahisha sana..umeiandika kwa usanifu wa hali ya juu walahi nai print nije kumpa mwanangu gaude asome jinsi kizazi hiki kilivopata shida
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Asante kwa uandishi murua uliojaa mafunzo yenye hekima kuhusu hali halisi inayokabili watoto/wadogo zetu!
   
 4. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hata mm nimeikubali kaka. Ubunifu umetulia na ndiyo hali halisi ya elimu yetu Tanzania
   
 5. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  huyu mtoto hatari kwa mahitaji, na ww uliyetumiwa barua hiyo, mtimizi mwanao hasa hitajio la mwisho kwa haraka zaidi kabla hajaanzisha andamano juu yako. Iko poa sana.
   
 6. m

  mkulungwa Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru wazee kwa comment zilizo tukuka, bado natafuta jibu la huyu kijana:mullet:
   
 7. M

  MBANINO Member

  #7
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu safi sana kwa ujumbe wako mzito.

  Umeweza kuutazama mfumo wetu wa elimu kwa mapana makubwa na kubaini mambo mengi ya ajabu ambayo yapo katika mfumo wa elimu hapa nchini kwetu.

  Ni ukweli ulio wazi bila Marking scheme na ku-solve past papers sio rahisi kwa kijana kufaulu katika mfumo wetu wa sasa. Maana mfumo hauruhusu kujisomea na kuwa creative bali una-support those who are good in cramming past papers.

  Athari la hili ni kuwa na wasomi ambao itakuwa vigumu kuweza ku-fit katika market ya ajira. Pia kuishia kuendeleza mawazo ya wengine na kushindwa kutumia elimu hiyo kuboresha na kuinua maisha ya Mtanzania katika mazingira yetu.

  Pili, hebu tuangalie hizi shule ambazo zipo katika 20 bora, je zinafanya hivyo kwa kuwa na ufundishaji mzuri au ni kwa sababu ya kuondoa wanafunzi wote ambao wanaonekana hawawezi kukariri marking schemes? Maana utakuta shule inaanza na wanafunzi 70 na wanaomaliza ni 40 tu, tujiulize hao wengine wamepotelea wapi? Ni kweli ya kwamba uwezo wao mdogo au ni usanii tu?
   
 8. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Karbu jamvini, hiyo barua ni hali halisi ya elimu zetu hapa bongo. imetulia na ina mantiki saa bigup
   
Loading...