Barua ya mapenzi kwa wino mwekundu

Barua ya mapenzi kwa wino mwekundu

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,977
Reaction score
37,879
Mwaka 1995 tulikuwa na mkata majani wetu aliyeitwa Manase. By that time, Manase alikuwa na miaka 25. Huyu jamaa alikuwa smart sana, kwa namna alivyo kuwa anajiweka smart usinge weza kuhisi he was just a standard seven leaver. Alikuwa na bidii sana na alikuwa anajifundisha kiingereza kwa njia ya dictionary..But alikuwa hataki kabisa watu wajue kuwa yeye ni shamba boy. Alikuwa anawadanganya watu ( hususani wasichana ), kuwa yeye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi. Kwa kuwa watu wa mtaani kwetu walikuwa wanajua kazi yake, mingo zake nyingi alikuwa anaenda kupigia mtaa wa tatu kutoka nyumbani kwetu. Nakumbuka aliwahi kupata demu mmoja aliyekuwa anaishi mtaa wa tatu kutoka nyumbani kwetu. Demu alikuwa anasoma kidato cha tano by that time. Manase alimdanganya kuwa yeye ni mwalimu wa shule ya msingi ambaye anajiendeleza kimasomo na ana mpango wa kufanya mitihani ya A-LEVEL kwa Private candidate. Siku moja nilimkuta akiwa anaandika barua kwa kalamu nyekundu, nikamuuliza, Ankal Manase vipi una msiba nyumbani kwenu ? ( Maana tulizoea barua za misiba ndo huandikwa kwa kalamu nyekundu ).. Akaniambia hapana uncle, unajua yule mwanamke wangu niliyekwambia, si anajua mimi ni mwalimu., basi namuandikia barua kwa kalamu nyekundu ili aweze kujiridhisha zaidi kuwa mi ni mwalimu.. Huwezi kuami, Manase aliwadaka wasichana wengi sana kwa gear hii.

* SO NDUGU ZANGU WAALIMU, NINYI NI WATU MUHIMU SANA KATIKA JAMII. MANASE ALILITAMBUA HILO, NA ALIWEZA KUITUMIA TASWIRA YENU KUJINUFAISHA..WHAT ABOUT YOU MWALIMU MWENYE DEGREE? JE
WEWE SI BORA KULIKO MANASE???TAFAKARI NA UCHUKUE HATUA!!!!!!!MNASEMAJE?!!!!! HAKI ELIMUUUUUUU!
 
UMARIDADI huficha umaskini,huku mtaani kuna wakina ankal Manase kibao

sema style zao za kidigital zaidi!!!!!!!!!!

ila ukikuta alivyounyuka si unaweza kusema Kijana ndio huyu kumbe hamna kitu.........
 
UMARIDADI huficha umaskini,huku mtaani kuna wakina ankal Manase kibao

sema style zao za kidigital zaidi!!!!!!!!!!

ila ukikuta alivyounyuka si unaweza kusema Kijana ndio huyu kumbe hamna kitu.........

Imeshakutokea nini ?
 
Kwako ww kunufaika nikupata mademu,inspiration story gani hiyo unayotoa kwa walimu na jamii kwa ujumla?tafakar...chukua hatua
 
Kwako ww kunufaika nikupata mademu,inspiration story gani hiyo unayotoa kwa walimu na jamii kwa ujumla?tafakar...chukua hatua


Nimeongea kishairi kaka, unajua HKL imeniathiri sana, simaanishi mademu, namaanisha namna thamani ya waalimu ilivyo kubwa
 
Back
Top Bottom