Barua ya kupangiwa kituo cha kazi

Barua ya kupangiwa kituo cha kazi

Joined
Apr 6, 2013
Posts
74
Reaction score
14
Nashukuru kwa dua zenu,nimeitwa kazini kupitia utumishi.Naomba kujua barua nitasubiri muda gani? au nifanyeje niipate?
 
Nashukuru kwa dua zenu,nimeitwa kazini kupitia utumishi.Naomba kujua barua nitasubiri muda gani? au nifanyeje niipate?

kawaida barua hua zinachukua muda inategemea na sehemu uliyopo mkuu,km unaitaka haraka nenda ofisi za utumishi huwa wana copy kaichukue,mim yangu ilikaa km 1 month hv ndo nikaipata mkuu mana siyo wanapotoa tagazo kwenye website ndiyo wanazipost hizo barua
 
Nenda sehemu uliyopangiwa kazi utakutana na barua yako.ukifika ulizia ofisi za utumishi,kama barua yako imefika.
 
Kwani JF ndio wamekuita kazini mpaka uje kuuliza humu barua yako ya ajira?

Wewe acha wivu, yote hiyo coz mwenzio kaitwa we hujaitwa. We mambo yote yanayouliziwa hapa JF yanakuaga yametokea hapa JF? Grow up dude.
 
Nenda sehemu uliyopangiwa kazi utakutana na barua yako.ukifika ulizia ofisi za utumishi,kama barua yako imefika.

Hawatampokea.

Nenda Jengo la maktaba, uliza sekretariati ya ajira chukua barua yako. Usisubirie hata posta...................... panda gari hata kesho!
 
Hawatampokea.

Nenda Jengo la maktaba, uliza sekretariati ya ajira chukua barua yako. Usisubirie hata posta...................... panda gari hata kesho!

sawa mkuu,ni mawazo tu,anaonekana anaharaka,ndo mana tuliotangulia tunampa alternative.BT CHA MSINGI ANGETAKIWA KUSUBIRIA BARUA YAKE POSTA,COZ ALIPO APPLY ALIAMBATANISHA,P.O.BOX.........
 
Nenda utumishi kaifwate hiyo barua, kisha utaripoti ulipopangiwa. Barua itaeleza. Its best kuripoti kazini before tarehe 15, maana utalipwa mshahara wa mwezi wa tano. Baada ya hiyo tarehe hulipwi. So the sooner the better.
 
hongera sana angalau unatia moyo kwa sisi ambao bado, sina cha kukushauri nakutakia tuu kazi njema pia mshahara wako wa kwanza usisahau kupeleka shukrani kwa mungu baba mana hiyo ni kwa neema tuu pamoja na wazazi au walezi walio kusomesha
 
sawa mkuu,ni mawazo tu,anaonekana anaharaka,ndo mana tuliotangulia tunampa alternative.BT CHA MSINGI ANGETAKIWA KUSUBIRIA BARUA YAKE POSTA,COZ ALIPO APPLY ALIAMBATANISHA,P.O.BOX.........

Sijui ilikuwa ni kwa kisa hiki tu, sina uhakika.

Yupo ndugu mmoja, alisubiri barua hadi mwezi ukapita. Akafunga safari hadi dar, sekretariet. akachukua copy akaenda kituo alichopangiwa.

Cha ajabu, kwenye kituo kipya walikuwa wameshaandaa taarifa kuwa mtumishi mpya hajaripoti hivyo waanze tena mchakato!

Huu ni ukweli! Nchi hii ina mambo mengi! Si kila mtu atafurahi kuona kimemo chake kukosa kipaombele!
 
Nashukuru kwa mawazo na ushauri mzuri,na ahidi kuufanyia kazi haraka.Mungu azidi kuwa nanyi.
 
Hongera kwa kupata kazi tumikia taifa kwa ari, nguvu na kasi...
 
kakomae mkuu life unaliona lilivyo! waoneshe uwezo wako kijana!
 
Pamoja sana wanajf nashukuru barua nimeipata,imebakia kuripoti kituo cha kazi.NEVER GIVE UP,GOD IS GREATER!
 
hongera sana na mshukuru mwenyezi mungu kwa kukupigania sasa ni wakati wako wa kulitumikia taifa katika njia ambayo itampendeza mungu na usiwasahau wazazi wako katika kila hatua uipigayo kaka!
 
Sijui ilikuwa ni kwa kisa hiki tu, sina uhakika.

Yupo ndugu mmoja, alisubiri barua hadi mwezi ukapita. Akafunga safari hadi dar, sekretariet. akachukua copy akaenda kituo alichopangiwa.

Cha ajabu, kwenye kituo kipya walikuwa wameshaandaa taarifa kuwa mtumishi mpya hajaripoti hivyo waanze tena mchakato!

Huu ni ukweli! Nchi hii ina mambo mengi! Si kila mtu atafurahi kuona kimemo chake kukosa kipaombele![/QUOTE
hao walioandaa taarifa ya utumishi walikuwa sahihi. ndo sharia ya kazi inasema hivyo
 
Back
Top Bottom