Nginyai
Member
- Feb 7, 2019
- 10
- 3
Tanzania ni mojawapo kati ya nchi zinazopatkana kusini mwa jangwa la Sahara, Afrika ya mashariki. Ni nchi iliyopata Uhuru mwaka 1961 chini ya utawala wa Mwl.J.K.Nyerere.
Ni nchi changa ukilinganisha na Marekani au Uingereza n.k. Nchi hii bado ni taifa linalotafuta mbinu za maendeleo, maana yake ni taifa linaloendelea. Kwa ujumla Tanzania bado ni taifa masikini katika takwimu za dunia.
Kwa mujibu ya tovuti ya Focus Economics na IMF Tanzania kwa mwaka 2019 ni nchi ya nane (8) kutoka ktk mataifa masikini zaidi duniani, hili ni janga ukilinganisha na mwaka 2016 ambayo tulikuwa wa 25.
Tatizo liko wapi? Na kwann?
Serikali ya John Magufuli inafanya kazi gani kama taifa linazidi tu kuporomoka?? Tangu rais Magufuli aingie madarakani ameagiza ndege nane(8) za kimataifa na tayari nne zimeshafika nchini, ambazo ni Bombardier Q400 mbili, Airbus na Boeng 787 Dreamliner.
Kwa kuangalia ukweli wa mambo ndege hizi hazina manufaa kwa watanzania hususan wa kipato cha chini, na inajulikana kuwa 75% ya watu wa Tanzania ni masikini wanaoishi chini ya dollar moja kwa Siku.
Sasa kwa takwimu hiyo hawa masikini watafaidi vipi usafiri huu ambao ni gharama kuliko usafiri wowote ule hapa nchini? Ni lini Mtanzania anayeishi chini ya dollar moja atafaidi ndege hizi zilizonunuliwa kwa kodi yake?
Miundombinu ya barabara, umeme, Maji, pembejeo za kilimo bado ziko katika hali mbaya kabisa
Lakini cha ajabu na kushangaza ni hatua ya serikali kugharamia ndege zaidi ya nane badala ya kutengeneza miundombinu hiyo.
Ifike wakati watawala wetu wasikie ushauri wa wasomi na wachumi kwa sababu sidhani kama huu ushauri wa kununua ndege badala ya kukarabati miundombinu muhim kwa watanzania wote ni ushauri wa wa wasomi bali ni kikundi flani cha watu wenye manufaa binafsi.
Tanzania ya viwanda inawezekana lakini je, rasilimali tunazo? Ikumbukwe kuwa viwanda vunategemea kilimo kwa 99% , tukirejea nyuma miaka ya 1700 inafahamika kuwa ndo muda mapinduzi ya kilimo yalianza huko Uholanzi (Netherland) na baadae kuenea bara lote la Ulaya.
Kabla ya mapinduzi ya kilimo ulaya hapakuwepo na kiwanda chochote lakini baada ya mapinduzi hayo ya kilimo ndipo ulaya ikaongoza kuwa bara la kulisha dunia kiviwanda.
Tanzania sisi inaonekana tunamwagilia miche huku mvua inanyesha.
Tunataka kuleta mapinduzi ya viwanda lakn rasilimali(raw materials) ziko wapi wakati mkulima anayetegemewa anatumia jembe la mkono na shoka, mkulima huyo huyo hapatiwi pembejeo na ruzuku, sasa je inawezekana?
Sent using Jamii Forums mobile app