Barua kwenda MORUWASA

nyembeason

Member
May 4, 2009
44
95
Mkurugenzi-MORUWASA

Mazimbu Road

MOROGORO

TANZANIA, East Africa


Ndugu,


YAH: UKOSEFU WA MAJI KWA MUDA MREFU-MITAA YA BIGWA VISIWANI, NJIAPANDA BIGWA.

Kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Kwanza kabisa nakupa pole kwa majukumu mazito uliyonayo ya ujenzi wa taifa. Najua wazi hilo ni jukumu zito ulilonalo, ingawa pia ni wajibu wako kuhakikisha unalitekeleza vyema na kwa weledi jukumu hilo ulilopewa na kuaminiwa na mwajiri wako, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pili, napenda kutoa mapendekezo yangu juu ya UKOSEFU MKUBWA wa maji unaendelea katika mji wa Morogoro, hasa maeneo ya Bigwa visiwani na njiapanda Bigwa. Binafsi nimeguswa mno na tatizo hili, na pengine limedhoofisha ujenzi wa taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja, hasa wazalishaji wadogo wanaouziwa maji kwa bei kubwa au kuchota maji machafu ya vijimito.

Tatizo kubwa zaidi ninaloliona mimi kwa Shirika lako unaloliongoza, MORUWASA, ni kukosekana kwa hekima na busara ya kawaida (rational distribution of water resources) katika kugawa RASILIMALI MAJI. Mathalani, kuna maeneo maji yanapatikana kila wakati lakini maeneo mengine hakuna maji kwa kipindi mpaka cha robo mwaka (Miezi 3 mpaka 4 bila maji).
 

Attachments

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom