Barua kwa wanaume mliooa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,257
2,000
BARUA YA SABA KWA WANAUME MLIOOA:- .
(Mahususi kwa wazinzi na wapenda michepuko)

---Nakala kwa:----
Wanaume wengine wote.
Wanawake wote.

Ndugu wanaume wenzangu,
Ninawasalimu kwa salamu za bajeti iliyosomwa juzi kati.

Naamini wengi wengi hamzifurahii barua zangu na ushahidi ninao kwa kuangalia mnavyouchuna hata ku-like. Poleni sana kwa lugha ngumu ninazotumia, lakini sina jinsi. Wengine mmeniambia mbona nimewaandama ninyi pekee na nimewaacha wanawake? Jamani! Jamani! Kwanza mimi siandami mtu, pili ni kwamba mraba wangu mimi upo hapa. Kama mke wako unaona ni kimeo ama kapinda, hebu mkabidhi Rose Shaboka na Winnie Nzobakenga ama Irene Mbowe, watamnyoosha na kumkarabati. Mie mraba wangu ni wanaume na ndio ninaoulima na kuupalilia kwa bidii.

TWENDE...

Mithali 6:32 inasema, "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake".

Tangu nilipolifahamu andiko hili nilipata kimuhemuhe cha kulichunguza kwa kina kwa sababu kichwani kwangu nilikuwa najiuliza maswali makubwa mawili:-

1). Inaposemwa huyu mtu(mwanaume) akizini anakuwa hana akili, Je, zinakuwa zimeenda wapi?
2). Huko kuangamia kunakosemwa kunatokeaje?

Ukiacha maswali hayo mawili, andiko hilo (Mithali 6:32) lina mambo mawili niliyoyaona:-
1) Inataja habari ya tendo la ndoa (lenyewe kama lenyewe)
2) Inataja tendo la ndoa kufanyika nje ya ndoa.

Katika kutafiti nikagundua kwamba akili za mwanaume huwa zinapotea kwenye tendo la ndoa (lenyewe kama lenyewe) na then, risk (hatari) ya kuangamia huwa inatokea pale tendo hili linapofanyika nje ya ndoa. Nimekuacha? Usijali! Utanipata tu vizuri muda si murefu.

Bahati nzuri nilisoma na kufundisha Baolojia, so, imenisaidia kulielewa vizuri hili jambo. Kuna tofauti tatu kubwa zilizopo baina ya mwanamke na mwanaume wanapokuwa katika msisimko wa tendo la ndoa.

MWANAMKE:-

a). Nguvu za mwili humuishia na mwili hulegea kabisa
b). Aibu huongezeka.
c). Uwezo wa akili hupanda kufikia kimo cha juu kabisa. (Hesabu ama swali ambalo asingeweza kusolve katika hali ya kawaida, anaweza kusolve katika hali hii)

MWANAUME:-
a). Nguvu za mwili huongezeka mara dufu
b). Aibu hupotea kabisa.
c). Uwezo wa akili hushuka na kufikia zero hasa wakati wa "mshindo". (Hata hesabu nyepesi ya moja ongeza moja anaweza kukosea na kusema sabini)

NDIO MAANA...

Mwanamke anapokuwa katika msisimko wa tendo la ndoa, kutokana na aibu hutaka lifanyike katika privacy kubwa ilhali mwanaume akishapandwa na midadi yuko radhi lifanyike hata barabarani (aibu haipo). Kutokana na akili kufikiria vizuri mwanamke huwaza vitu vingi wakati wa tendo hili (mimba zisizotarajiwa, magonjwa, siri kufichuka kama ni tendo la kimichepuko n.k), wakati mwanaume yeye huwa hawazi chochote zaidi ya kutaka kumaliza hamu (kwa sababu uwezo wa akili unakuwa umeshuka). Kutokana na mwanaume kuwa na "minguvu" na mwanamke kuwa "legevu", wakati huu, ndio maana kuna mambo wanawake hulazimishwa kwa nguvu kuyafanya ambayo wasingekubali katika hali ya kawaida. Enewei, ngoja nisiende ndani sana maana hapa sio inbox.

SIRI USIYOIJUA

Wanawake ambao huridhishwa kikamilifu katika tendo la ndoa huwa na uwezo mzuri sana wa kufikiri, kupanga mambo na kufanya kazi kwa bidii. Nguvu za mwili za mwanamke hurejea katika hali ya kawaida ikiwa ataridhishwa wakati wa tendo hili. Asiporidhishwa huweza kubaki amelegea na mtepetevu kwa siku nzima ama zaidi. Kwa upande wa wanaume ni kwamba:- wanaume wanaoendekeza sana ngono, uwezo wao wa kufikiri, kupanga mambo na kufanya maendeleo hushuka. Na ndio maana kuna kupungukiwa ama kuishiwa nguvu za kiume lakini ni nadra kusikia mwanamke kapungukiwa nguvu za kike. (Please usichanganye, mafaili. Wanawake huwa wanapungukiwa ama kuishiwa hamu na sio nguvu. Nguvu ni maalumu kwa ajili ya wanaume). Asomae na akafahamu!

IKO HIVI:-

Ule muda ambao mwanaume akili yako inakuwa kwenye "sifuri" na ukakutana na mwanamke ambae hakutakii mema, ni rahisi kukumaliza. Pamoja na nguvu za mwili zinazoongezeka kwa mwanaume, lakini nguvu hizo zinakosa maana kwa sababu akili inakuwa haipo. Mwanamke uliepo kifuani mwake ndie anakua ameshika rimoti na anaweza kuku-control vyovyote atakavyo pamoja na minguvu yako, maana akili saa hiyo unakuwa "huna".

Kuna mambo matatu ya kufahamu yanayoweza kutusaidia wanaume:-

1). Mwanamke yeyote (awe wa ndoa, awe kahaba, awe mchepuko) anaeitambua siri ya tofauti nilizokutajieni anaweza kulitumia tendo la ndoa ku-controll akili ya mwanaume kwa mema ama kwa mabaya. Ndio maana Shetani huwa anacheza na uwezo wa mwanamke anapotaka kumuangusha, kummaliza ama kumbomoa mwanaume. Mungu nae akitaka kumsimamisha na kumwimarisha mwanaume humtumia Mwanamke. Naweza nisieleze yote hapa hadharani, lakini tambua kwamba kuna siri za kiroho na za kimaumbile za hatari sana katika tendo la ndoa. Wanawake mlioolewa, hebu kamateni pointi hapa japo juu juu, sawa enhee?

2). Ahadi zinazotolewa wakati wa tendo hili huwa zina nguvu na roho kubwa sana. Ukitaitiwa wakati wa tendo hili na ukajikuta umeropoka ahadi maybe ya kumjengea mtu nyumba, kumnunulia gari ama kumfanyia lolote, aisee, hilo litakuganda. Kupitia tendo hili unaweza kuikana familia yako, unaweza kuingiziwa chuki ya kumchukia mke wako hadi wewe mwenyewe ukabaki unashangaa. Ndio maana jamaa yetu Samson alipojichanganya kuahidi kutoa siri za nguvu zake, lilimganda hadi akaja kutimiza na kujimaliza.

3). Kutokana na 1 na 2 hapo juu, wanaume tunashauriwa kuitoa miili yetu kwa wake zetu pekee kwa ajili ya tendo hili la ndoa, just kwa ajili ya usalama wetu. Mke wako mnaependana hata akiamua kupenyeza matakwa fulani fulani wakati wa tendo hili, uwe na uhakika inakuwa ni kwa manufaa yako na familia yenu. Jambo la kuelewa ni kwamba hakuna mwanamke nje ya mke wako anaetembea na wewe at the same time useme anakuwazia mema. Kitendo chake cha kuutoa mwili wake kwako akijua una mke, ujue tayari Shetani amesham-sponsor kukuangamiza na muda wowote atakumaliza "totally".

Naamini mnapata vitu vya kuwasaidia hata kama nawakwaza.
Ni mimi,
[HASHTAG]#SmartMind[/HASHTAG]
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,269
2,000
Somo zuri sana. Japo kulielewa na kulifuata mafundisho yake ni mtihani mgumu kwa watu wengi.
 

Zooluline

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
208
225
mi niliombwa buku ten tu na mchepuko wakati wa tendo tben sikutoa. ina maana nilikua na akili zangu timamu, wallet ilikua ina uhai wa laki tatu kwa jeanz..
 

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,419
2,000
Mwanaume akisha zini na mwanamke basi akili yake inahamia kwenye kichwa cha chini kwa muda na kichwa cha juu kinabakia empty.

Na ndio maana ukiombwa hata lakini muda huo unaitoa tu tena haraka, Ila baadaye akili zikisharudi kwenye kichwa cha juu unaanza kujiuliza hivi niliitoaje ile laki?

Wanawake ni shetani wadogo.
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,221
2,000
3). Kutokana na 1 na 2 hapo juu, wanaume tunashauriwa kuitoa miili yetu kwa wake zetu pekee kwa ajili ya tendo hili la ndoa, just kwa ajili ya usalama wetu. Mke wako mnaependana hata akiamua kupenyeza matakwa fulani fulani wakati wa tendo hili, uwe na uhakika inakuwa ni kwa manufaa yako na familia yenu.


Takwimu zinaonesha kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume, je wanawake wasiokuwa na wanaume miili yao ni totauti na wale wenye waume, je wao hawana haki ya kutimiziwa haja za miili yao, kama wana haki je watimiziwe na wanyama mwitu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom