Barua Kutoka Ughaibuni - Rais Uwezo Wa Kutatua Matatizo ya Umeme tunao


Keynes,

Haya ni mambo ya uchumi na biashara. Na sioni sababu ya kusubiri 2015. Omar Bashir, Dikteta wa Sudan, anaweza kusimamia spectacular economic growth, kwani viongozi wetu wasiweze?
 
Keynes,

Haya ni mambo ya uchumi na biashara. Na sioni sababu ya kusubiri 2015. Omar Bashir, Dikteta wa Sudan, anaweza kusimamia spectacular economic growth, kwani viongozi wetu wasiweze?

Si umesema uwezo TUNAO/WANAO?

Miafrika...Aah yu wapi Nyani Ngabu?
 
Zakumi majuzi nilikuwa naongea na mwanafunzi mahiri wa Uhandisi wa Madini. Nikamuulizwa kwa nini mnashindwa kuendesha uchimbaji wa madini bila kutegemea wawekezaji kutoka nje. Akajibu kwa ufupi: HATUWEZI. Nilisikitika sana kusikia hivyo. Ila ndio halisi. Tunajiona HATUWEZI. Hivyo uwezo HATUNA.
 
ZA10,
Umesema ...tumekusikia.
Ujumbe utafika kunakohusika hopefully.

WoS,

Namuandikia Rais sio kubeza nafasi yake na juhudi zake za kazi. Nachoomba tu ni serikali kufikiria kuwa watanzania wenye kipato cha kitajiri, watanzania wenye kipato cha middle class na watanzania wenye kipato cha upper working class wanaweza kufanya mchango mkubwa katika sekta ya uzalishaji wa umeme bila kutegemea mwekezaji kutoka nje.

Kwa kuwa sekta hii ina uhakika katika uzalishaji na uuzaji, basi ianzishwe kampuni binafsi ya ubia. Watu tununue share. Kama serikali ya marekani inatoa tax incentives kwenye uwekezaji wa nishati, basi wafanyabiashara wetu na watu wenye kuwekeza ubia kwenye uzalishaji wa umeme wapewe taxi incentives.

Na hili kampuni hilo la ubia liendelee watafuteni wazalendo mahiri na waaminifu kuliendesha hili kupunguza risks.
 

Mt,

Muuza mkaa anapata faida. Muuza kuni anapata faida. Muuza mafuta anapata faida. Hizi nishati zote zinaweza kutolewa na muuza umeme. Hivyo uzalishaji wa umeme ni biashara ambayo watanzania wanaweza kuchangia kwa pesa zao wenyewe. Hii ni kwa sababu kila siku ni lazima watumie nishati.
 
Zakumi,

Nitakuunga mkono kwa kuleta makala nyingine iliyochambua uwezo wa vyanzo vya umeme/maji tulivyonavyo: The curious case of electricity dearth in Tanzania (Dec 17, 2010).

 

Companero,

Wawekezaji sio wataalamu wa madini. Walichonacho ni mtaji na business models. Ethiopia Airline, Emirates, Qatar ni mashirika ambayo yana business models za ku-operate airlines. Na sio mashirika yanayotengeneza ndege.

Botswana walikuwa na business models na mitaji lakini wataalamu wametoka Tanzania, Zambia, Zimbabwe n.k Hivyo uwezo tunao hata katika sekta tusio na wataalamu. Ukuchangisha mtaji mzuri watapatikana experts kutoka nchi yoyote hile duniani.
 
Zakumi nchi hii imejaa wafanyabiashara na wanataaluma wa Biashara. Hadi Serikalini wamo. MBA za kumwaga. Sasa mbona hawawezi? Au modeli zao za biashara zimepitwa na wakati? Pengine elimu yao ni cheti na si ujuzi? Hebu cheki vichwa vilivyo humu: www.ali-ea-foundation.net . Inakuwaje nchi yenye viongozi wote hao wa biashara inashindwa hata kutoa umeme wa uhakika kwa 12% tu ya wananchi wake?
 

Companero,

Ukumbuki ule mjadala wetu miaka zaidi ya saba iliyopita hivi, The Talented Tenth. W.E.B. DuBois? Si baadaye DuBois alikatishwa tamaa nao na kuhamua kuwa mkommunisti kabisa.

Failures za bourgeois na ruling classes zetu zinaniweka njia panda. Nikiwa na waAfrika wenzangu naanza kumkumbatia Nyerere na Kwame. Nikiwa huku viwanja niko free marketier.

America ilikuwa-design kuwa nchi ya kilimo. Liconln anachukua nchi, industrial output ilikuwa less than 10%. Lakini sera zake za federalism na waliomfuatia waliweza kubadili nchi. Viwanda vya nguo vya uingereza vilitegemea pamba kutoka Marekani. Na lilikuwa ni kosa la jinai kusafirisha michoro ya mashine ya nguo kwenda Marekani. Na mtu aliyepeleka michoro hiyo ilibidi akariri mashine nzima.Hiyo ndio elimu na utaifa.

Na katika kipindi hicho kulikuwa hakuna Master, Phd or MBA degrees. Hivyo elimu bila enlightenment haina manufaa kwa jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…