Barua Kutoka Ughaibuni - Rais Uwezo Wa Kutatua Matatizo ya Umeme tunao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua Kutoka Ughaibuni - Rais Uwezo Wa Kutatua Matatizo ya Umeme tunao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zakumi, Jan 5, 2011.

 1. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,809
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Ndugu Wazalendo,
  Kwa mara ya kwanza nilimuona Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, JK, nchi Marekani miaka mitano iliyopita katika mkutano wa waTanzania waishio Marekani ya kaskazini uliofanyika mjini Washington DC baada ya kuchaguliwa kuwa rais.

  Katika mkutano huo, rais alisema alikabiliwa na mambo matatu makubwa: Ujambazi, matatizo ya umeme na mvua. Leo hii ni mwaka wa tano kamili. Tatizo la umeme bado lipo palepale. Na katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka amesema kuwa moja ya sababu za kushindwa kwa kutafutiwa ufumbuzi tatizo hilo ni kujitoa kwa mwekezaji kwa sababu ya matatizo ya uchumi wa kidunia. Ifuatayo ni maoni yangu kwa ndugu rais.


  Ndugu rais, ngoja nikupe vipande vyangu vya mawazo. Kama Ndugu Basil Mramba aliweza kusema kuwa ndege ya rais ni lazima kununuliwa hata kama wananchi watakula nyasi. Na mimi nakwambia kuwa watanzania tunao uwezo wa kujenga mitambo ya umeme hata kama gharama zake zitatufanya tule udongo.

  Na kwa kutumia msemo wa baba wa taifa kuhamasisha watanzania kupigana vita. Nitasema uwezo wa kujenga mitambo tunao, sababu ya kujenga mitambo zipo. Kinachoshindikana ni nia ya nyinyi viongozi kuwa waadilifu na wakweli.

  Vifuatazo ni sababu za kuonyesha kuwa uwezo na sababu kuwa tunazo. Idadi ya watanzania ni 40milioni wenye vipato vyenye kutofautiana. Pamoja na tofauti yao, wapo watanzania wenye kipato cha kuweza kuchangia ujenzi wa vinu vya uwezo tofauti. Kwa kuanzia watanzania wanaweza kuchangia kinu cha 40MW. Na mafanikio ya kinu hicho yatahamasisha watu kuchangia vinu vyenye uwezo mkubwa.

  Najua mtashangaa ni jinsi gani watu wanaweza kuchangia. Tanzania tunalo soko la share, Dar Es Salaam Stock Exchange. Ianzishwe kampuni ya wenye SHARE na yenye kuongozwa na wazalendo waadilifu na wenye kuaminika. Na baada ya hapo zitangazwe share. Manunuzi ya share hizo zitumike kujenga kinu. Mapato yatakayotokana na uzalishaji wa umeme wa kinu hicho yarudi kwa wawekezaji na vilevile yatumike kuongeza tija ya kampuni hilo.

  Ndugu rais umetumia miaka mitano mitakatifu kuzunguka duniani kutafuta wawekezaji. Ukweli wa mambo wawekezaji wengi waliopo nje watafanya yale niliyokwambia. Watachukua pesa kutoka kwenye mifuko ya share, au mifuko ya kustaafu na kuleta mitambo Tanzania. Na sababu ya mwekezaji kujitoa kwenye mradi wa Mtwara ni kushindwa kupata pesa kwenye mifuko mbalimbali kutoka mifuko hiyo kuathiriwa na matatizo ya uchumi.

  Sioni sababu ya mwekezaji kuja na mtaji na kupata faida ya zaidi ya 25% kwa pesa zitokanazo stocks, mifuko ya uwekezaji au mifuko ya kustaafu. Hiyo mifuko inaweza kuchangiwa hapohapo na faida kubaki hapohapo Tanzania. Hivyo kwanini mzunguke nje kutafuta misaada na wawekezaji wakati mkijisafisha tu katika safu zenu vitu hivyo vitapatikana hapo hapo nyumbani?

  Ndugu rais sababu za kuwa mitambo ya umeme hipo. Kwanza umeme ni biashara nzuri na yenye kuitajiwa na watanzania wengi. Utaongeza matumizi mazuri ya gesi na makaa ya mawe na kutoa ajira kwa watanzania. Utaimarisha ubora wa maisha yetu.


  Nia ya kununua share hazipo kwa sababu ya uongozi mbaya toka tumepata uhuru. Siku zote viongozi wetu mmetufanya watanzania kuwa ni watu wa kufanya vitu vidogovidogo tu. Mkitaka ujenzi wa shule au uwanja wa michezo mtatulazimisha tuchangie. Lakini kwenye vitu vya maana mnaona kutembeza mabakuli nje ya nchi ni sifa kubwa sana.

  Vilevile mnaogopa kutuchangisha kwenye miradi mikubwa kwa sababu mnaogopa kuwa mkishindwa tutaandamana pale mkiboronga. Wale wazee waliofanya kazi kwenye shirikisho la Afrika mashariki wanawasumbua. Hivyo mnaogopa kuchukua dhamana, kwa sababu nikitoa mchango wangu mkubwa na ukashindwa kuleta umeme nitakufanyizia kwa njia yoyote hile. Iwe kwe uchaguzi, uchawi, au sayansi nitakufanyizia tu.

  Ndugu rais kama tungekuwa na uongozi imara katika mambo ya biashara, ninakuakikishia kuwa watanzania wanao uwezo wa kununua share zenye uwezo wa kuanzisha kampuni la kuzalisha umeme. Na kama wazo ili lingeanza miaka mitano iliyopita, kwa sasa hivi taifa lisingekuwa kwenye matatizo ya umeme.

  Wako katika ujenzi wa taifa,
  Za10
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  wenzako sio kwamba hawajui , bali nia na azma yao ni kutuibia tu, ndio maana mtambo wa $7m za usa wao wana mkopesha mwekezaji au wako tayari kumlipa huyo mwekezaji? mara kumi ya hiyo hela
   
 4. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,052
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  Maisha bora kwa kila mtanzania, Kasi, nguvu na ari zaidiiiiiiii, aliingia kwa kishindo hata aliitwa MALAIKA, kumbe...........................
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Ni kweli kabisa, Watanzania 'Uwezo Tunao' kwa kiasi kikubwa sana na endapo kila mmoja wetu TUTAUTAMBUA SIRI KUBWA HIYO basi moja kwa moja hakuna kujililiza ovyo kwamba tunaonewa wala kuibiwa na kikundi au kusakamwa na umasikini wa kupindukia kila leo.

  Kinachohitajika hapa ni kwamba KATIKA 'VITA' VYA MABADILIKO YA NGUVU YA UMMA kamwe hakuna kikundi chochote cha kushughulika na ushabiki wa wengine uwanjani. Lakini kinachotakiwa ni kila mmoja wetu kuwa MCHEZAJI HODARI kwa nafasi yake na ule ule uwezo mdogo aliojaliwa na Mwenyezi Mungu.

  Hata siku moja hakuna wa kumomba Mungu kwa udhati kabisa akaondolewe maadui UDHALIMU NA UFISADI na wafadhili wake hata akapewa MAWE. Hivyo, naunga kauli ya Ndg Zaikumi hapo juu kwamba kweli Wa-Tanzania kwa pamoja UWEZO TUNAO; kila mmoja awajibike kwa nafasi yake kuleta mabadiliko ya kweli nchini mwetu Tanzania sasa hivi!!!!
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zakumi acha ubishi. Uwezo huo kwa sasa hatuna. Labda baada ya miezi 36 kwa mujibu wa maneno ya Rais:  Ndugu wananchi;
  Mwaka 2010 haukuwa na utulivu wa kutosha kwa upatikanaji wa umeme. Mara kadhaa kumekuwepo na matukio ya kukatika na mgao wa umeme kutokana na uharibifu wa mitambo ya kuzalisha umeme hasa katika kituo cha Songas na vituo vya TANESCO. Pamoja na hayo tatizo la msingi ni uwezo wa uzalishaji wa umeme kuwa mdogo kuliko mahitaji. Hivyo basi, hitilafu katika mtambo mmoja au kituo kimoja cha kuzalisha umeme huzua tatizo kubwa la upatikanaji wa umeme kwa nchi nzima.

  Ndugu Wananchi;
  Katika kukabiliana na tatizo hilo miaka mitano iliyopita, TANESCO kwa msaada wa Serikali, imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme kwa MW 145 (MW 100 Ubungo na MW 45 Tegeta) kwa kutumia gesi asilia. Bahati mbaya mpango wa kuzalisha MW 300 kule Mtwara kwa kushirikiana na sekta binafsi, haukufanikiwa baada ya mwekezaji kushindwa kupata fedha kwa sababu ya mgogoro wa masoko ya fedha ya kimataifa. Kama tatizo hilo lisingekuwepo umeme huo ungekuwa unakamilika au kukaribia kutumika hivi sasa.

  Kwa sasa TANESCO ina mipango kadhaa inayoendelea nayo ya kuongeza uzalishaji wa umeme nchini. Kwa msaada wa Serikali ndani ya miezi 12 ijayo, TANESCO itaongeza uzalishaji wa umeme kwa MW 160, (MW 100 Ubungo kwa kutumia gesi asilia na MW 60 Mwanza kwa kutumia dizeli nzito). Kwa kushirikiana na sekta binafsi pia, ndani ya miezi 36 ijayo TANESCO wanatarajia kukamilisha ujenzi wa vituo vya umeme huko Kinyerezi (MW 240) Somanga Fungu (MW 230) na Mtwara (MW 300). Inatarajiwa pia kwamba katika kipindi hicho mradi wa kuzalisha MW 200 pale Kiwira utakamilika.
   
 7. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwanini msirudi kusaidia taifa sasa?
   
 8. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  sipendi hata kujadili suala la umeme, ni la kutia machungu sana...sijui nani amewaloga viongozi hawa?
   
 9. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160

  hivi mamito yote hayo tuliyonayo tunashindwa kweli kuwa na vituo vikubwa vya kuzalisha umeme, Tanzania tulivyobarikiwa na muumba Mwenyezi Mungu ishu ya umeme haitakiwa liwe tatizo tuna Makaa ya mawe gesi mito upepo na urenium lakini bado.

  Ili tuwe na maendeleo umeme haupingiki kuna vitu vinne muhimu ambavyo vikiimarika maendeleo yanakuwepo

  1. Chakula tuna mabonde kibao na mito kibao lkn hatuna uhakika wa chakula ntu akiwa hana uhakika wa kula hawezi fanya kazi huku akili ikiwa imetulia na inawezasababisha hata vita
  2. Afya
  3. Elimu
  4.Miundombinu
  lakini vyote hivi haviwezi kuimairika kama hakuna umeme. Umeme ni muhimu kuwa nao bila umeme utasindikaje chakula na kukihifadhi. bila umeme utamchunguza mtz kubaini ugonjwa unaomsumbua. Bila umeme utafanyaje utafiti na majaribio mashuleni ili upate wataalamu wazuri
  bila umeme traffic light zitafanyaje kazi

  Kweli kuchagua CCM ni kuchagua maafa sasa nazidi kumuelewa Dr. Slaa
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,809
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Companero,

  Mkuu huna nia ya kufanya vitu vikubwa zaidi ya kutoa michango ya shule za msingi, sekondari na viwanja vya michezo. Hizo ndio jitihada za mtanzania alizopangiwa na serikali yake, IMF, WB na nchi wahisani.

  Katika hotuba hiyo ya rais, anasema kuwa private sektor ilishindwa kwa sababu mwekezaji kushindwa kupata fedha kwa sababu ya mgogoro wa masoko ya fedha ya kimataifa.

  Hayo masoko ya fedha za kimataifa hayachapishi pesa au kuokota. Yanatumia pesa za mifuko ya kustaafu, mifuko ya manispaa za miji, bonds , hedge funds n.k

  Na haya masoko yanakuja Africa kwa sababu profit returns ni kubwa kuliko profit returns zinazopatikana kwenye nchi zao. Hivyo hao investors wako tayari ku-cross boarders.

  Kama faida ni kubwa Africa, kwanini waAfrica wasiimarishe masoko ya ndani ya pesa? NSSF ni soko la ndani la pesa. DES ni soko la ndani la pesa.

  NSSF wako tayari kujenga daraja la kigamboni. Lakini kwa hesabu zangu za haraka haraka, uuzaji wa nishati una faida kubwa na ya uhakika katika kipindi cha muda mfupi kuliko ujenzi wa daraja.

  Na kampuni inaweza kuanzishwa kwa wazo. Na wazo hilo likachangiwa pesa kwa watu kununua share pale Dar Stock Exchange. Kuna mifano ya kutumia kutumia masoko ya ndani, lakini kwa sababu huna nia subirini 401K yangu ije iweke umeme.
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zakumi huoni kuwa tatizo lipo katika matumizi ya neno TUNAO? Unamsemea nani unaposema uwezo TUNAO? Je, Kiongozi Mkuu wa Nchi yako uliyemchagua aongoze nchi ama kwa kumpigia kura au kutopiga kura kasema kuwa huo uwezo TUNAO?
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,809
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Ninazo dollar 10,000 benki ambazo haziniingizii faida yoyote. Nipo tayari kutumia fedaha hizo kununua share katika kampuni yoyote itakayowekeza kwenye nishati ya umeme Tanzania. Bado unataka nirudi Tanzania?
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,809
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Companero,

  Nilichoandika mwanzo ni persuasive essay. Na nimetumia rethoric device (tunao), kuonyesha kuwa it's doable. Kwa watanzania wanaofikiri kuwa kuchangia ujenzi wa shule za msingi, na viwanja vya michezo ni shughuli tulizohitimu na hatuna haja ya kurudiarudia, wanajua kuwa uwezo tunao.

  Lakini kwa watanzania ambao sukari ikikosekana wanakimbilia kunywa uji kwa muhogo, nawaomba kawasheni vibatari vyenu na msubirini mwekezaji.

  Wako

  Za10.
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Zakumi,

  KIla kitu tuna uwezo nacho, ni upuuzi wa Viongozi.
   
 15. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,809
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Rev,

  Na mpaka sasa sijaona kampuni la umeme likifiriska kwa kukosa biashara. Hivyo uwekezaji kwenye umeme is almost risk-free investment. Net-group haikuja na mtambo wowote. Kuongoza Tanesco kwa mitaji yetu walipata faida.
   
 16. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Tatizo la uzalendo na wizi a.k.a madili ndivyo vinavyovza maendeleo yetu katika sekta zote.
   
 17. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani kusaidia taifa lako lazima huwe unaishi Tanzania?Wewe unayeishi Tanzania umeshawahi andika makala na kutoa hayo mawazo yako?Tuachane na mawazo mgando jamani.Watu wa sasa wanakuwa challenged kuwa global citizens kutokana na changamoto zinazoikabili dunia.Kila mtu kwa nafasi yake na bila kujali yupo Asia,America au Africa ana nafasi ya kuchangia maendeleo ya Tanzania.Tuachane na mitazamo kuwa kwa kuishi Tanzania ndo tunatoa michango mikubwa zaidi katika maendeleo ya taifa kuliko wenzetu walio sehemu nyingine duniani.
   
 18. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Dowans lazima walipwe kwani inawezekana hiyo ndio ikawa deal ya mwisho ya Jakaya mrisho kikwete,aliingia na EPA atatoka na DOWANS
   
 19. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Zakumi.
  Unataka washirikishe watanzania kwenye miradi ya umeme halafu 10% watapata wapi? Cha ajabu viongozi wa kitanzania hua wanakula 90% katika miradi badala ya hiyo 10%..
  Kaka garama ya kumaliza tatizo la umeme wa tanzania its just 5% of our yearly budget but serikali wamefanya kua ni mradi wao wakuibia watanzania.
  Hapa solution ni kura tu mwaka 2015 maana serikali yote inanuka rushwa.
   
 20. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,612
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Zakumi
  Kwanza nikupe hongera kwa kuanzisha mdahalo huu muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa. Tanzania ya leo inataka kuondokana na umasikini wakati takwimu zinaonyesha ya kwamba miezi 4 na siku kumi nchi inakuwa haina umeme.

  Tanesco imekuwa kampuni kwa miaka 46 sasa, na ni ukweli usio pingika kwamba tatizo la umeme la Tanzania linasababishwa na uongozi mbovu ndani ya Tanesco. Viongozi wa Tanesco ni incompetant na mabwanyenye. Hawana sifa za uongozi wa biashara period.

  Mimi ni mmoja kati ya wale wanao support kuvunjwa kwa Tanesco na kufanya makampuni mawili au matatu. Wazalishaji, wasambazaji na wauzaji. Huwezi kuwa na hizi kampuni tatu ndani ya mmoja. Serikali ishikilie uzalishaji, acheni makampuni binafsi waendeshe usambazaji na uuzaji.

  Tunaweza kuzalisha umeme wetu wenyewe bila kuomba hata sumni kwa mtu yoyote.
   
Loading...