Barikiwa leo.. yes leo

CHIBA One

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
558
Reaction score
2,103
Baba Mungu nakushukuru kwa uzima, Afya, na neema yako hata tukaiona siku ya leo.. Mungu Naomba usikie kuomba kwangu hata ukatende sawa sawa na mahitaji ya watu wako..

Mungu nnayekuamini uliyetenda na kuniokoa kabla hata sijazaliwa Nakuja kwako leo nikiomba kwa ajili ya wako hawa na ukawabariki leo katika jina lako

WAGONJWA, waponye na kuwapa uzima leo Bwana wa majeshi, gusa madhaifu yao, gusa kuugua kwao na ukawape uzima katika jina la yesu.

UCHUMI, kaguse njia za vipato na uchumi kwa huyu mwenye mahitaji ya kimaisha baba, kamuinue, fungua baraka na njia za kipato akakidhi mahitaji yake na familia yake Jehova.. Najua wewe ndiye utoaye Baba kamguse leo baba, akasahau machungu na maumivu ya maisha, Mguse leo Bwana.

KAZI, NDOA, AFYA NJEMA, MISONGO YA MAWAZO... Mungu mwenye Nguvu, mfalme wa wafalme, nani kama wewe bwana? Naomba leo ukaongee na nafsi zao, ukasimame na matamanio yao ya kazi, ukalete amani katika ndoa zao, ukalete Afya katika maisha na miili yao, Ukawapa amani katika kuishi kwao, Badilisha maisha yao leo jehova, mienendo yao wakakutumikie na kukuabudu wewe, ukalete faraja ndani ya mioyo yao.. Gusa Mungu wangu, Gusa kila doa katika kuishi kwao.. Mungu nnayekuamini, Napokea na kusema asabte kwa ajili ya mtu huyu, watu hawa, vijana hawa, mabinti hawa, wazee hawa,

Ni wewe peke yako unaweza kuwatoa hapo walipo Mungu..utukufu na heshima urudi kwako jehova.. Ni katika jina la mwanao yesu kristo tunaomba AMEN.
 
Meseji nzuri. Ubarikiwe sana mkuu na Mungu akatende kwa ajili yao wote

Amen
 
Watu wanazipita nyuzi Kama hizi sijui kwanini. Ubarikiwe mtoa mada ingawa kiukweli nimesoma juu juu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwasababu ni ujumbe wa Mungu.
 
Amina mwenyezi mungu kaguse mionyo ya watu hasa wale wanaohitaji msaada na huruma yako
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…