Bariki fedha yako

Bariki fedha yako

Wakishua org

Member
Joined
Feb 23, 2023
Posts
20
Reaction score
33
Amani iwe nanyi wana jamvi 🙏🏾 Nipo hapa kuweza kushirikishana katika namna bora ya "kubariki fedha zetu" Kuna waandishi wengi sana Duniani ila kuna huyu Nguri mwandishi Robin Sharma ambae kaandika zaidi ya vitabu 10 maarufu na kimoja wapo ni "NANI ATALIA,SIKU UKIFA?"

FmrDBz9X0AEqq3Y.jpeg

Katika kipengele namba 25 kazungumzia "kubariki fedha zetu" kwa kunukuu aliweza andika hivi "Kila wakati kumbuka kubariki fedha kila unapotoa. Iombee kuwa baraka kwa yeyote itakae mfikia, pia iamuru huko iendako ikatumike kulisha wenye njaa na kuwavisha wasio na nguo pia iamuru kurudisha zaidi ya ulicho toa". Zingatia maneno haya 🤔📌

Mwana jamvi mwenzangu kwa nini tusitumie Ushauri huu?

Katika maisha yetu ya kila siku "Unapolipia chakula mgahawani, kimya kimya bariki walio fanikisha kukuwekea chakula:

Mkulima aliekuza kikiwa shambani, msafirishaji kutoka shamba mpaka mtunzaji ghalani pamoja na mmbembaji.

Unapofanya malipo ya ada za watoto, kwanini usiwabariki kwa walimu wote wanao tumia muda wao kuwafundisha wanao pamoja na wote wanao watunza salama! Pale unapofanya manunuzi ya bidhaa katika duka/kibanda, unaweza kumbariki muuzaji/mmiliki kuweza kukua kwa mtaji mtaji wake pamoja na kuleta maendeleo ya maisha yake kupitia fedha yako. Kuna ule usemao, "Mikono itoayo zaidi ndio hubarikiwa zaidi katika utafutaji"

Napenda kuhitimisha kwa kusema hivi dunia ya sasa imebadilika sana kumekua na fedha zinazopatikana kwa njia za kishirikina na halali, hivyo kwa kuwa hatuwezi kuzitambua na njia pekee ni kuzibariki/ kuziombea kila tunapozipata au tunapotoa kwa watu wengine.🙏🏾🙏🏾
 
Nimesoma vitabu vingi vya huyo guru. Nimejifunza mengi na vimenibadilisha jinsi ninavyoyachukulia maisha
Kitu ninachopenda zaidi Sharma sometimes ana recall toka kwa waandishi wengine hivyo akichanganya na mambo anayoyaona katika jamii, basi hufanya uandishi wake kuwa bora zaidi.
 
Back
Top Bottom