BARIADI: Wanafunzi wagoma kushinikiza Mkuu wa shule kutohamishwa

Asovene

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
213
216
Kwa mujibu wa ITV habari leo saa 2 usiku wanafunzi wa Bariadi sec wamefanikiwa kwa kupambana na polisi kuandamana na kushinikiza mkuu wao wa shule kutohamishwa kituo cha kazi.

Haya ni maandamano ya kwanza kufanikiwa tangu utawala huu mtukufu ambao kila kinachofanyika ni MUNGU kuingia madarakani.

Asanteni wanafunzi mmetupa somo kumbe kila kitu kinawezekana na sisi tunaye Mungu.

====

Wanafunzi waandamama kupinga kuhamishwa kwa Mkuu wa shule.

ZAIDI ya Wanafunzi 600 wa shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo katika halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga barabara kuu ya Bariadi –Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Deus Toga.

Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri,lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi la polisikuzuia ghasia (FFU) kuwazuia kwenda katika ofisi hizo.

Hata hivyo wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabara hiyo waliamua kuandamana tena kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa jambo lililoshindikana pia baada ya askari hao kuwazuia tena eneo la Hospitali teule ya mkoa (Somanda).

Baada ya hali hiyo wanafunzi hao ambao ni kidato cha kwanza hadi cha sita waliamua kukaa katikati ya barabara huku wakiimbanyimbo za kushinikiza kuwa hawamtaki mwalimu Paul Lutema ambaye alikuwa amepelekwa kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Na huo ni moshi tu. Waswahili wanasema ngoma ya watoto haikeshi lkn wamefanikiwa japo km kawaida policcm lazima wasababishe vurugu kwa kutotumia akili.
NGOMA YA KIKUBWA YAJA PUNDE KWA JINSI TULIVO NA HASIRA NA UONGOZI HUU WA KIIMRA UPENDELEO NA KUJIKWEZA NA KUJIFANANISHA NA MUNGU
 
Think before act, sasa wewe unashangilia, una elezea ama?
Maana walicho kifanya wale wanafunzi ni kukiuka sheria sasa una andamana unaenda kufunga barabara kuu, halafu madai yao mwalimu asihamishwe, inaingia akilini?
Labda wange goma kuingia darasani.
l wish na mimi ningekuwa moja ya wale askari ninge gawa dozi haswa hadi akili zao zikae kwenye mstari.
 
Think before act, sasa wewe unashangilia, una elezea ama?
Maana walicho kifanya wale wanafunzi ni kukiuka sheria sasa una andamana unaenda kufunga barabara, halafu madai yao mwalimu asihamishwe, inaingia akili?
l wish na mimi ningekuwa moja ya wale askari ninge gawa dozi haswa hadi akili zao zikae kwenye mstari.
Unauliza kama inaingia akilini? Kwani wanafunzi walitaka nini na wamepata nini? Vyeti unavyotumia ni vyako kweli?

"Think before act?" Huko shuleni ulienda kusomea ujinga?
 
Kwa walimu au mwajiliwa yoyote hurusiwi kufukuzwa kazi wakati wa mgomo...Tena kwa walimu wa serikali ambao masharti yao ni yakudumu ni rahisi sana kugoma...na katika serikali nyepesi ya kugomea ni hii kwa sababu haiwezi kuajiri hata nusu ya waliyopo kazini,haiwezi hata kulipa mafao ya nusu ya waliyopo.huu ni wakati muafaka
 
Think before act, sasa wewe unashangilia, una elezea ama?
Maana walicho kifanya wale wanafunzi ni kukiuka sheria sasa una andamana unaenda kufunga barabara, halafu madai yao mwalimu asihamishwe, inaingia akili?
l wish na mimi ningekuwa moja ya wale askari ninge gawa dozi haswa hadi akili zao zikae kwenye mstari.
Akili za kushikiziwa hizi. Hazina tofauti na zile za kolomijez
 
Unauliza kama inaingia akili? Kwani wanafunzi walitaka nini na wamepata nini? Vyeti unavyotumia ni vyako kweli? "Think before act?" Huko shuleni ulienda kusomea ujinga?
Majibu yako tu, tayari yanaonesha na wewe ni wale wale tu, ukikimbizana na kichaa na wewe utaonekana kichaa.
Endelea kushabikia ujinga.
 
Think before act, s
WhatsApp Image 2017-03-06 at 16.38.14.jpeg
asa wewe unashangilia, una elezea ama?
Maana walicho kifanya wale wanafunzi ni kukiuka sheria sasa una andamana unaenda kufunga barabara kuu, halafu madai yao mwalimu asihamishwe, inaingia akilini?
Labda wange goma kuingia darasani.
l wish na mimi ningekuwa moja ya wale askari ninge gawa dozi haswa hadi akili zao zikae kwenye mstari.
inaonekana mwalimu wao alikua fair lazima wagome tu maana inaonekana alikua anawakaushia hata wakinywa wine
 
wanafunzi wanasumbua wakati mh.mtukufu akifungua uwanja wa kivita wa jeshi ..... i wish i could be RPC
 
Kwahiyo polisi waliwashindwa wanafunzi au kihezo cha(wanafunzi)kimewabena, na ukizingatia dai lao halikuwa na ulazima kuwanyima???

Maana sioni hii ikiwezekana kwa watu wazima kama waalimu, kwamba nao wataachiwa.
 
Back
Top Bottom