Mkuu, labda hujanielewa vizuri, nianze na msemo huu "SIMBA HATA AKIZEEKA HAWEZI KUWA MBWA" Barca inabaki kuwa Barca, timu kubwa na nzuri kupita timu nyingi tu; jana wacheza kamari hata washabiki wa PSG walibet kuwa Barca anashinda kutokana na timu na historia. lakini Barca wamapungua makali sio kama wale waliopiga Manchester United miaka mitatu iliyopita; ulikuwa ukikutana na Barca unahesabu magoli tu na sivinginevyo. Kingine mkuu hapa sisi ni mashabiki na Ushabiki umo; labda nideclare interest mimi binafsi ni shabiki mkubwa wa Chelsea na Real Madrid. Na ni adui mkubwa sana wa Manchester United, na kidogo Barca. So kuna wakati lazima tuongee kama mashabiki na vilevile kama watu tunaoujua mpira pia. Nimemaliza mkuu...Inshallah