Baraza lagoma kuongeza bei ya umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza lagoma kuongeza bei ya umeme

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Dec 3, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  SIRI ya muda mrefu ya kinacholifanya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuendesha shughuli zake kwa kiwango cha chini na kutaka kupandisha bei ya umeme kila siku hatimaye imefichuka.

  Katika hali iliyowaacha vinywa wazi wajumbe na wadau waliokutana jana katika kikao cha kujadili maombi ya Tanesco ya kutaka kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 155, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo William Mhando alikiri kuwa wanashindwa kufanya kazi kikamilifu kutokana na ukosefu wa fedha, na kwamba wanaidai serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kiasi cha sh bilioni 137 ambazo zingefidia gharama za uendeshaji wa shirika hilo.

  Kujulikana kwa madeni hayo, kuliwafanya wajumbe wengi waliokutana katika mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) na kuwashirikisha timu ya viongozi wa Tanescco wakiongozwa na mkurugenzi wake pamoja na wajumbe wa bodi ya Tanesco akiwamo Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa (CCM) kukataa ombi la shirika hilo la kutaka kupandisha bei ya umeme.

  Akichangia katika mkutano huo, mwanaharakati na mdau wa maendeleo, Renatus Mkinga, alisema haiwezekani wananchi waumizwe na kubebeshwa mzigo wakati serikali ikikalia fedha za Tanesco.

  Mkinga bila kutafuna maneno alisema ni lazima serikali ilipe madeni yanayofikia sh bilioni 87 huku Zanzibar ikidaiwa sh bilioni 50 ambazo zitaliwezesha shirika hilo kuimarisha shughuli zake.

  Mdau huyo aliwashambulia viongozi wa serikali kwa kile alichokiita kutokuwa na huruma kwa watu wake kiasi cha kusababisha mgawo wa umeme.

  "Hivi sasa suala la umeme linaendeshwa kisiasa zaidi kuliko utaalamu na hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa na kukosekana kwa uzalendo na uhuru kwa wananchi. Kama bei ikipandishwa, tutashuhudia wizi ukitamalaki," alisema Mkinga.

  Alieleza pia kutofurahishwa kwake na kitendo cha watumishi wa Tanesco kupewa uniti 700 kila mmoja, kwa madai kuwa kinachangia kurudisha nyuma maendeleo kwa kulifanya taifa kuwa na tabaka la watu wenye nacho na wasio nacho kila kukicha.

  Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Ushauri la Serikali, William Buhunire, alisema baraza hilo licha ya kupitia ombi hilo la dharura la Tanesco la kupandisha umeme kwa asilimia 155, wamelitaka shirika hilo kufanya juhudi kukusanya madeni yake kwa wadaiwa sugu.

  "Hakuna sababu wala haja ya kuongeza bei ya umeme kwa kiwango kikubwa, lazima mhakikishe mnakusanya kiasi hiki kikubwa cha fedha na muandae mnyumbuliko wa kuwabaini wale wote mnaowaita wadeni sugu ili waweze kulipa fedha hizi," alisema Buhure.

  Alisema Tanesco ilipaswa kuonyesha gharama halisi na badala yake wametumia gharama za ziada za kulisha umeme wa dharura kutoka kwa kampuni za Symbion na Aggreko pamoja na mafuta ya mitambo yao.

  "Hali kama ikiachwa na Tanesco kuruhusiwa kupandisha umeme, inaweza ikaleta madhara makubwa na hata kuathiri uchumi wa nchi na inaweza kuwafanya wawekezaji wasivutiwe tena kuja nchini kwa kuogopa gharama za uendeshaji," alifafanua Buhure.

  Naye Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma zinazodhibitiwa na Ewura, Profesa Jamidu Katima, alisema kutokana na utafiti uliofanyika imebainika kuwa Tanesco imeshindwa kutoa mchanganuo unaosababishwa na gharama za umeme wa dharura.

  "Gharama za Tanesco kuzalisha umeme ni sh 139,293 huku mapendekezo ya mwaka 2012 ni 248,536 sawa na asimilia 74.84, hizi ni baadhi tu ya gharama ambazo hazipaswi kuongezeka na hazina uhusiano na dharura iliyopo hivi sasa nchini," alisema Profesa Katima.

  Alisema baraza hilo linapinga hatua ya watumiaji wengine kulipia gharama za wafanyakazi wa Tanesco zipatazo sh bilioni 16 huku ikiitaka Ewura kutoyakubali maombi hayo.

  Awali akiwasilisha mada katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhando, alisema Tanzania imekuwa ikitoza gharama za chini kwa watumiaji wa umeme ikiwa tofauti na nchi nyingine.

  "Kutokana na hali hii, tunaiomba Ewura iidhinishe ongezeko la bei ya dharura, ambapo bei ya wastani ya kuuza umeme hivi sasa ni sh 141 kwa uniti ipande hadi sh 359 kwa uniti kuanzia Januari 2012, na sababu kubwa ni kuiwezesha Tanesco kukabiliana na gharama za uendeshaji kutokana na juhudi za kuondoa mgawo wa umeme," alisema Mhando.

  Hatua ya kupingwa ongezeko la umeme, imekuja siku chache tu baada ya mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika (CHADEMA) kupinga hatua hiyo, akieleza kuwa itawaumiza wananchi wa kipato cha chini.

  Mnyika alisema badala ya kupandisha, serikali kupitia shirika hilo, ingetafuta mbinu nyingine za kupata fedha za kuendeshea shughuli za Tanesco badala ya kuwaongezea wananchi bei ya umeme.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Serikali inadaiwa Shilingi bilioni 137 na TANESCO badala ya kulipa deni hilo ili kuboresha huduma za TANESCO imeenda kuongeza posho kwa Wabunge kwa kiwango cha kutisha.

  Kweli hii Serikali vipaumbele vyake vimekaa kushoto kushoto, labda wanasubiri TANESCO ishindwe kabisa kufanya kazi ili wapate nafasi ya kuanzisha makampuni yao ya usambazaji wa umeme ambapo bei ya umeme huo itakuwa haishikiki kabisa.
   
 3. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Serikali ya ccm ni serikali sikivu itasikia kilio cha TANESCO itawaruhusu kupandisha bei ya umeme tupende tusipende.:A S 465:
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  kwenye reli wamefanikiwa sana, maana sasa hivi usafirishaji wa mizigo kwa malori umetamalaki, na hayo malori ni mali ya viongozi wa seriakali. Sasa wanahamia tanesco, then watakuja afya, mwishowe nchi hii watabaki peke yao na familia zao tu...........
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja yako kamanda!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kufanya hivyo walipe deni lao kwanza la Sh 137 billion badala ya kuwabebesha mzigo mkubwa walipa kodi ambao wameshaelemewa na gharama kubwa za maisha.
   
 7. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Vuteni subira, miezi mitatu siyo mingi sana.
  Bei itapanda tu wanabodi
   
 8. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizo ni pamoja na wanazodai DOWANS au?
  Naomba ufafanuzi wadau
   
 9. c

  chegreyson JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 736
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 60
  Hivi hawa tanesco wanayajua maisha ya Watanzania au wenzetu wapo sayari nyingine?
  Kupandisha umeme kwa kiasi kikubwa namna hii, na kutokana na ukweli kwamba mchanganua wa gharama za uzalishaji hauonyeshi undani wa ukokotoaji wa hesabu zake, inaweza kuwa janja ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuwalipa Dowans.
  Bajeti ya wizara ya nishati ilipita baada ya benki ya Stabic kuikopesha serikali Tshs 250bn, hinyo ni dhahiri kuwa tunalazimishwa kulipia mkopo pamoja ya riba klwa Stabic bank.
   
 10. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Mpaka sasa bei ya umeme Zanzibar ni dogo kuliko tunayolipa sisi bara. Hata kama gharama zitapanda bara ndo tutakaoumia. Bado SMZ haioni aibu inashindwa/goma kulipa deni! Tumechoka kubeba mizigo wa wazanzibar.

  Hivi sheria ya TANESCO haiwapi nguvu kuikatia serikali umeme? Kila mwaka taasisi zinakuwa na bajeti na umeme ni sehemu ya matumizi yanayoainishwa laki OC ikija nikulipana posho tu. Hivi hata kama serikali italipa ikija kuilipa TANESCO baada ya miaka mitano fedha itakuwa na thamani ileile?

  Wananchi tusimame tuisadie TANESCO kwa kuishinikiza serikali kulipa deni
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Hizi ni pesa ambazo TANESCO wanatakiwa walipwe (ziingie kwenye account ya TANESCO) na Serikali za Bara (87 Billioni) na Visiwani (50 Billioni) ile ya Dowans ni pesa ambazo zinatakiwa zitoke kwenye account ya TANESCO ili kuwalipa Dowans pamoja na kuwa waliohusika kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mkataba ule fisadi ni viongozi wa Serikali na si wa TANESCO ndio waliohusika.
   
 12. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Ningekuwa menaja wa TANESCO ningefunga LUKU kwenye kila taasisi ya serikali. Ukienda POLISI kwota au megereza utashangaa kukuta wake zao ndo wazalishaji wa barafu kwa ajiri ya kuwauzia wafanya biashara. Hawalipii umeme na hawajui gharama yake. Tumeonewa kiasi cha kutosha sasa tufike wakati tukomeshe tabia hizi za serikali kunyonya watu wake
   
 13. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Miaaaaaaaaaaaa!
  Piga luku mpaka JW alafu ataibuka kaka mkuu "ooo jamani taasisi zingine mziache mtaingilia maswala ya usalama" ovyoooo!
  kwani bajeti zao zinazopita bungeni si mpaka matumizi ya umeme au hayo hamna?
   
 14. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mie ndio hapo napoishangaa hii serikali! tena pale kilwa road police kwenye zile flat mpya wamepiga marufuku matumizi ya mkaa, sasa mwendo wa pale ni majiko ya umeme na gas! nambie sasa watumiaji wengi ni umeme! laiti wangejua gharama yake.....!?
  wanachekelea umeme wa bure, wananchi wa kawaida wanaumizwa.
   
 15. N

  Njaare JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Huku ndo kufikiria kutumia makalio. Kwetu umeme unatakiwa uwe chini kwa sababu tuna vyanzo vingi vya umeme wa bei nafuu. Tanesco ifikirie kuachana na mikataba feki ijikite kuzalisha umeme kutumia mito iliyopo, makaa ya mawe nahata ikibidi isomeshe wataalam kwa ajili ya kuanza kutumia wa nyukilia.
   
 16. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Bei ipande tu watu tule good tyme!!
   
 17. T

  Taso JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Taarifa ya professa Katima haijaenda shule. Kwanza 248,536/= kutoka 139,293/ = sio ongezeko la 74%, Na huwezi "kupendekeza" gharama za kuzalisha zitaongeza, una "project, una kadiria, gharama zitaongezeka. Unless of course the meaning is lost in translation, as I would certainly expect from our shoddy press.

  TANESCO ianze kutumia pre pay system kwa serikali, kama wanavyotufanyia raia, LUKU!

  Zanzibar kama tarrifs zao ziko chini, basi ni kukosa creativity Wabongo, ma dealer wanunue vocha ZNZ waje kutuuzia Bara.

  Na Zanzibar walishasema hawatolipa ng'oo. Hivi kwa nini tunawa kiss a$$ Wazanzibar?
   
 18. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  wangepandisha tu iyo bei ya umeme,watz tumezidi mno woga. maisha bora kwa kila mtz.
  nyway hivi hii serikali viongozi wake wana akili timamu? au ni wenda wazimu.
  just check, mlalahoi alipe kodi...waitumie vibaya na malaya wao huko...then ailipie
  serikali bill ya umeme? kodi mmefanyia nini? kuna haja ya serikali yetu kuwa na dini
  ili walau vinongozi wake wawe na huruma na maadili
   
 19. a

  adobe JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Enyi ewura,twaomba saana muwalazimishe hao tanesco wawalipishe wafanyakazi wao.unit 700 ni nying sana wanaweza kutumia ovyo ovyo watakavyo hizo ni sawa na tshs 120000 kwa mwezi.tanesco msipende kula jasho la wengine.hao hao ukitaka wakufungie umeme wanataka rushwa.kuna mmoja aliniambia nimpe laki tisa ndo ajeniunganishia.ushahid ninao wa namba na sms aliyonitumia.
   
 20. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Natamani sana hii bei ipande nadhani FF atajua kuwa CCM ni wrong number. Hivi kwanini Tanesco wasifanye kama shirika la nyumba
   
Loading...