Baraza la Usalama la Taifa

Mods mngefuta au kurekebisha ID ya 'jansonbourne' against 'Janson Bourne' na swala kama ili muwe nalo makini na serious, otherwiz mtaigeuza JF kuwa FB...
 
Wakuu huyu si Jason Bourne mliye mzoea huyu ni Jasonbourne! ametumwa kuvuruga wasomaji kwa kumwaga upupu! Kwanini mods wanaruhusu tofauti ya space kama ID mpya? Rekebisheni haraka ID ziwe na tofauti ya wazi!

Hivi mkuu Jason Bourne (mzee wa hutaki unaacha) alienda wapi?
 
Kwa akili yangu nijuavyo mimi

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2) Rais wa SMZ
3) Mkuu wa Usalama wa Taifa
4) Mkuu wa Majeshi
5) IGP
6) Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Bungeni
7) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
8) Jaji Mkuu wa Tanzania
9) Waziri wa Ulinzi na Usalama
10) Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 17, kifungu cha 267 kifungu kidogo cha 1 kinasema kutakuwa na Baraza la Usalama la Taifa na wajumbe wafuatao:
a) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio
Mwenyekiti
B) Makamu wa kwanza wa Rais
C) Rais wa Zanzibar na Makamu wa pili wa Rais
D) Waziri Mkuu

Kifungu kidogo cha 2 :Mwenyekiti anaweza kumualika mtu yoyote kushiriki katika kikao cha baraza la usalama
Kifungu kidogo cha 3
Kinasema kutakua na Sekretarieti ya baraza la Usalama la Taifa itayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi

Majukumu ya baraza ni

Kuunganisha sera za ndani, sera za nje na za kijeshi kuhusiana na Usalama wa Taifa ili kuwezesha taasisi za kiulinzi
kushirikiana kikamilifu
B) Kupokea na kutathimini taarifa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Taifa na taasisi za serikali kuhusiana na usalama wa nchi
C. Kutekeleza majukumu mengine yoyote kama Rais atakavyoagiza.

My take:
Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama huingia kwa nafasi zao
 
Lipo na linafanya kazi; Mara ya Mwisho tulisikia tamko la Baraza la Usalama wakati ile Meli ilizama Zanzibar (Is slander).... Tamko lilisomwa na Katibu Mkuu kiongozi..... kwa Hiyo kwa haraka haraka wajumbe watakuwa wafuatao
1. Rais.....
2.Katibu mkuu kiongozi...
3....................
4.....................

Namba 2 hapo CS anaingia kwenye kikako cha Sektretarieti ya baraza la Usalama wa Taifa anakua ndio Katibu wa sekretarieti ya baraza la Usalama wa Taifa
 
Lipo lakini sidhani kama linafanya kazi kama linafanya kazi ni karibia na uchaguzi kwa ajili ya kudhibiti wapinzani na kutoa maelekezo utoaji wa matokeo hasa ya urais
 
Back
Top Bottom