Baraza la seneti

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Wana jamvii,
Nimetafakari sana mstakabali wa taifa letu katika mfumo huu wa vyama vingi nikaona kuwa mbele kuna giza totoro. Hivi ni nani anapanga vipaumbele vya taifa letu? tunaliendesha taifa letu kwa dira ya nani?mi ninaona kwa sasa chama kilichoko madarakani ndicho kinachopanga vipaumbele hivyo mfano, MKUKUTA, MKURABITA , MEM, MES n.k na mara nyingi vipaumbele hivyo vimekuwa ni matokeo ya vipaumbele vya UN, mfano millenium Dev goals na nyingine.

Kwangu hii naiona ni hatari sana kwasababu nchi yetu na raslimali zetu na hatima yetu inategemea UN na wanasiasa walioko madarakani ambao siku za hivi karibuni wameonekana kuwa wabinafsi na wa kujilimbikizia mali.

Kwa nini kwenye katiba mpya tusiwe na baraza la seneti? baraza hili liundwe na watu maalumu, professional and politicians pia.. mfano maraisi wastafu na majaji, ( kama tu wana sifa zinazotakiwa na wako tayari kupoteza uvyama wao baada ya kustafu), watu wenye sifa zilizotukuka katika jamii, watu wa type ye desmond Tutu,nk, bila kujali dini zao au kabila ila uwezo wao kama hazina ya taifa.

Wajumbe hao hawatakuwa wanavyama wa vyama vya siasa , watakuwa watanzania, wazalendo, watu wanaoangalia maslahi na mstakabali wa taifa letu.

Baraza hilo litakuwa na kazi ya kupanga vipaumbele vyetu kama taifa , mipango ya muda mrefu na mfupi, litajadili na kuweka malengo kwa ajili ya kulifikisha taifa katika ustawi halisi wa kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Kazi ya vyama vya siasa itakuwa siyo kupanga sera bali kueleza namana gani wanasiasa wao watafanya ili kutufikisha kule ambako baraza letu la taifa, baraza la seneti limepanga kwenda.

Wanasiasa hawatakuwa na muda wa kutuchezea sarakasi (mfano, mara huyu aje na sera ya kuunganisha masomo ya fizikia na kemia kuwa somo moja kabla ya mwenzie kurudisha kuwa mawili tofauti) na kutuuingiza kwenye nikataba feki tena ya muda mrefu kama miaka 100

Wanasiasa watapimwa kila baada ya miaka mitano kwa swali hili; kwa miaka mitano tuliyokupa ni hatua gani tumepiga kuelekea kwenye malengo yetu kama yalivyopangwa na baraza letu la seneti? kama amefanya kwa kiwango cha kuridhisha atapata nafasi ya kuendelea, la hajaweza atapigwa chini.

Nchi hii inahitaji waonaji, wazalendo na watu wenye moyo wa taifa hii ndio wapewe nafasi ya kutupa dira ya tuendako na siyo wanasiasa ambao sera zao mara nyingi ni za kuwahadaa wananchi ili waendelee kutawala, no wonder wanaweza kutoa ahadi ( mfano barabara za angani au kusomesha watoto wetu bure nk) huku wakijua fika kuwa ahadi hizo hazitekelezeki, ilmradii tu wapewe dhamana ya kuongoza.
Nawasilisha
 
mkuu umeshasema wajumbe ni pamoja na maraisi wastaafu wakati hui huo unataka wajumbe wasitoke kwenye vyama, mkuu.acha kuchanganya mambo
 
mkuu umeshasema wajumbe ni pamoja na maraisi wastaafu wakati hui huo unataka wajumbe wasitoke kwenye vyama, mkuu.acha kuchanganya mambo

Soma vizuri, kwanza nimesema mfano, halafu nikasema kama watakidhi sifa za kuwa wana seneti... hili ni wazo tu, kama likipita basi tutajadili namna ya kuwapata wajumbe hao wa baraza!!!
 
mimi naona ni vizuri wangetofatisha ubunge na uwaziri. yani wabunge wangebaki tu kutetea watu wao majimboni kwao alafu mawaziri wakawa ni watu wa kawaida wenye elimu ambao sio wanasiasa. imagine mtu kama dr. ulimboka anakua waziri wa afya. mtu kama huyu anajua shida zote ambazo watu wanahitaji. kila wizara ingepata watu kama hao nadhani nchi ingepiga hatua.
 
Hiyo seneti itakuwa ulaji mwengine wa CCM na watoto na vimada wao wakiwamo akina Makamba, Kawawa, Nyerere, Mwinyi, Karume, Lusinde Malecela nk. Katika nchi hii hao ndio watu maalumu, professional and politicians pia.. mfano maraisi wastafu na majaji, watu wanaojiona wana sifa zilizotukuka katika jamii, watu wanaojiona ni type ye desmond Tutu,nk, bila kujali dini zao au kabila ila uwezo wao kama hazina ya taifa.

Utakuwa mtaji mwengine wa vigogo.
 
Back
Top Bottom