Baraza la sanaa huu ni utapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la sanaa huu ni utapeli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kibogo, Jul 16, 2012.

 1. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  kuna kikundi cha Vijana hapa Nchini wametokea kujifanya ni miongoni mwa wana kamati wanaohusika na Ufuatiliaji wa Hati/haki miliki juu ya kazi za wasanii, sasa watu hawa mara nyingi wamekuwa wakivamia maeneo ya Mikoa ya Shinyanga na Tabora(Hususani katika wilaya za Nzega na Kahama) huku wakitembea na polisi wa maeneo hayo na kukamata mtu yeyote watakaye mkuta akiwa na Computer ambayo ina nyimbo na mtu huyo unyang'anywa computer hiyo na kisha kutozwa faini isiyopungua Tsh. 500,000/= na kisha kuachwa akiendelea na kazi yake, sasa naomba BASATA watoe ufafanuzi juu ya suala hili kwani mara nyingi nchi hii sheria ya kitu furani inapotungwa ujitokeza matapeli wengi na kujifanya ni wahusika na kujipatia kipato kwa njia ya utapeli kama hawa wanaoonekana katika mikoa hii.
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Hapo Dawa ni kuacha wizi wa kazi za sanaa,ata ukitaka basata wakujibu still wewe ni mwizi so lazima ushughulikiwe,acha wizi wa kazi za wasanii
   
 3. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  1. Hapo ndugu naona unanihukumu kwa kazi ambayo sihusiki nayo, mi nia yangu ni hawa BASATA kuwa na mfumo mzuri ambao hautachangia matapeli kuingilia kazi za kamati hiyo na kuchafua jina la BASATA hata wewe hapo ulipo na kasimu kako hako ka mchina kana nyimbo za wasanii sijui umezotoa wapi kama sio wizi, wabunge wetu ambao ni watunga sheria wana nyimbo za wasanii kwenye simu zao hupo hapo mkuu! cha muhimu ni kuunda mfumo mzuri utakao wanufaisha hawa wasanii wetu tunapenda sana kuwachangia lakini tunawachangiaje ikiwa masanii anatoa single na yeye mwenyewe ndo anaisambaza kwa washikaji zake.
   
Loading...