Baraza la Mawaziri kivuli nalo lipanguliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Mawaziri kivuli nalo lipanguliwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duble Chris, Apr 30, 2012.

 1. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Baada ya Rais JK kuunda baraza jipya (kumodify) la mawaziri nashauri Mbowe aunde baraza jipya la Mawaziri Kivuli ambalo litaendana na aina ya Mawaziri watako teuliwa - kiuwezo

  Pia nashauri achanganye na wabunge wa vyama vingine vya siasa (vya upinzani) ili kutimiza ahadi yake aliyo itoa siku anatangaza baraza lililopo sasa.
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Muandika uzi unafahamu neno KAMBI RASMI kisheria?
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kama kanuni inasema mawaziri vivuli watatokana na kambi rasmi haitawezekana maana CUF walilikoroga walipolazimisha neno 'rasmi' liongezwe, kama hivyo inabidi kanuni itenguliwe tena.
   
 4. February

  February Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wadau serikali kivuli duniani kote hupaswa kuonesha kiwango cha juu cha uwezo kuliko serikali. Hii ni moja ya changamoto kubwa ninaiona katika mwenendo wa mpambano kati ya baraza la jk na baraza kivuli.

  Ukweli baraza la JK ni dhaifu lakini kiwango cha shadow cabinet kuonesha uwezo mbadala bado ni changamoto iliyo wazi. Naomba tujaribu kupitia wizara moja hadi nyingine tupime kama msemaji wa kambi ya upinzani anaonesha uwezo kiasi gani ukilinganisha na waziri husika, naibu wake na hata mwenyekiti wa kamati ukizingatia kuwa kamati zote za kisekta zinaongozwa na wabunge wa ccm. Kwa mfano linganisha wizara ya fedha, nenda nishati na madini, kilimo, miundombinu, mifugo, makazi, miundombinu, uchukuzi, tamisemi, elimu, afya. Nk.

  Je, pamoja na udhaifu wa vilaza walioshika uwaziri katika wizara hizi nikweli kuwa mawaziri vivuli wanaonekana kufunika? Huwa naona aibu sana kuona wenyeviti wa kamati wanakuwa visible kuliko wasemaji wa upinzani. Hii ni aibu. Kwasababu mwenyekiti wa kamati ana mipaka ya mapambano kwakuwa serikali ni ya chama chake lakini msemaji wa upinzani hafungwi na mpaka wowote kwani lengo lake hasa kuhakikisha serikali iliyopo inaondoka na serikali ya chama chake inaongoza. Hii ni changamoto.

  Mimi najitahidi kufuatilia bunge lakini ukinipa mtihani wa hata kutaja mawaziri vivuli kumi na wizara wanazongoza napata shida kidogo, inanichukua muda na wakati mwingine nachanganya. Hii ni kwasababu mawaziri vivuli hawakati madaraka yao vilivyo. Kuna haja ya training ya kutosha kwa shadow cabinet na kusuka upya kama itaonekana ina tija.
   
 5. February

  February Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naomba tupime wizara hadi wizara.
   
 6. r

  rsmiruko Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona wewe na mtoa mada hamfuatilii speech za mawaziri vivuli. Mfano tu, fikiria speech za akina Mnyika, Mdee, Zitto, Lema na wenzao. Cheki pia kamati za kisekta zinazoongozwa na wapinzani, eg zitto, cheyo na mrema
   
 7. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mawaziri vivuli wanafanya kazi yao vizuri sana. Ila speaker mara nyingi anakuwa kikwazo, ana hila nyingi yani utazani ni mtu aliyetokea kuzimu, akashushwa tu pale bungeni.
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mawaziri vivuli wamefanya kazi vizuri, kama wewe ni mfatiliaji utagundua wizara nyingi zimechukua mipango ya Mawaziri vivuli katika shughuli zao.

  Mawaziri vivuli hawawezi kufunika sababu hawana serikali, so wanabakia kukosoa na kutoa mipango mbadala. Mipango hiyo mbadala ikitekelezwa, credit zinakwenda wizara husika ama serikali.

  Ila cha msingi si kushindana kati ya vivuli na vihalisia, muhimu serikali iwatumikie wananchi vizuri na kusimamia rasilimali zetu ipasavyo.
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani yupo Likizo
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  tunacho sema hapa ni kuwa baada ya JK kuunda baraza jipya la mawaziri basi Mbowe aangalie vichwa vitakavyo ingia barazani ili aviundie mawaziri kivuli wanao fanana nao au kuwazidi kama ilivyo kwenye wizara ya sheria na katiba

  tunajaribu kuzuia kupwaya kwa kambi ya upinzani kwa hoja wawapo bungeni, tukumbuke kuwa hawa jamaa watakuja na nguvu kubwa sana kuzima hoja za upinzani
   
Loading...