Baraza La Madiwani: Wilaya Ya Kishapu Kuna Njaa

madiwani wanaounda halmashauri ya wilaya ya kishapu wamejadili kwa dharura hali ya njaa inayoikabili wilaya hiyo.

hawa nao wamenunuliwa? mhe polepole na chama chako mjitathmini.

source: itv habari
Wamenunuliwa na wanasiasa hao
 
Ewe Mheshimiwa Rais mwenye enzi yote, wewe uliyetukuka na usiyejaribiwa, wewe usiyependa ujinga...mbona Watanzania na vyombo vya habari vya Tanzania ni kama hawajasikia amri zako kali???

Katika Taarifa ya habari saa 2 usiku huu, wakati wewe ukiwa unapasua anga ndani ya Bombardier yako uliyeinunua kwa pesa taslimu kuelekea Addis Ababa kuudhihirishia ulimwengu kuwa wewe si wa kispotispoti na kwamba Kiingereza unakijua, eti ITV wao kwa kuwa wamejua haupo wameamua kuripoti kuwa kule kwenu Kishapu eti kuna njaa, mifugo inakufa na huenda watu nao wakaanza kufa, hivi huu si uchochezi wa wazi wazi baba???

Na tena hizi taarifa eti zimejadiliwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani ambalo karibu wajumbe wote ni madiwani watokanao na Chama chako kilichotukuka, hivi huu kama si ukorofi ni nini??? Tena Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye anatokana pia na chama chako eti anasema katika kata yake peke yake wamekufa ng'ombe zaidi ya 420, sasa huu kama si ujuha ni nini...kwanini wasile nyama za hao ng'ombe wanaokufa??? Yani watu amekufa ng'ombe wa kwanza wakamfukia tu, akafa wa pili wanaangalia tu, hadi ng'ombe wa 420, huku si wanataka tu kukujaribu wewe baba usiyejaribiwa???

Na hivi Mtukufu Rais, kama wewe uliye Rais hujawahi kuiona njaa na wala huijui njaa, na wala hujawahi kuona watu wakifa kwa njaa, au mifugo ikifa kwa ukame, kwanini watu wanakuwa na mdomo mrefu kiasi hiki kila siku wanang'ang'ana kudai kuwa wao wanashinda njaa na eti kuna ukame mvua hazinyeshi??? Hivi wanataka wewe ukawapikie chakula??? Na hivi wewe Mtukufu Rais si majuzi tu ulikuwepo Shinyanga baba, na hivi huko si ndo kwenu, na hivi huko si ndiko ulikopata zile kura mil. 2 ulizomzidi Lowassa, na hivi si uliona jinsi mvua zinavonyesha huko na kijani kutamalaki, sasa iweje leo, wiki 2 tu baada ya wewe kutoka huko, eti kijitokeze kimtu na kusema kuna ukame na njaa wakati wewe Baba Mtakatifu bado hujaoteshwa, na wewe uliona kwa macho yako mvua zikinyesha???

Hivi Mtukufu Rais, hawa Watanzania nani kawaroga??? Wewe hukuleta tetemeko, hujaleta ukame, hujaleta njaa na wala hujaua ng'ombe, sasa kwanini wana mdomo kiasi hiki???

Hahahaha aaaaaaaaah, TWAFAAAA!
 
Atafungia vyombo vya habari vingapi atafukuza wangapi mengine inabidi awe anakausha tu
 
Mbuzi kakata kamba! Minong'ono hiyoo imeanza, itafuata kelele na baadae Nduru! Mficha maradhi kilio humfichua lakini pia wahenga walisema "mficha uchi hazai"?! Tutulie muda utaongea!
 
Wanaotakiwa wafe ndipo mwenyeheri ajue kuwa kuna njaa ni watu ambao hawatakuja wawe na njaa, wanatakiwa wafe wakuu wa mikoa, Wilaya, mawaziri nk, lakini hao wanaotangazwa haki ya nani hao ITV hawana bahati.
 
Nisiwachoshe wakuu.
Taarifa ya habari ya saa 2 ITV madiwani halmashauri ya kishapu walalamika njaa katika eneo lao. Mbaya zaidi ni pale mwenyekiti wa halmashauri aliposema yeye binafsi ng'ombe wake 20 wamekufa kutokana na ukame na katika eneo lake wamepoteza idadi ya mifugo 400. Sasa najiuliza hawa jamaa hawakumsikia mkuu wa kaya aliposema yeye ndio mwenye mamlaka ya kutangaza njaa?Au pale aliposema kuwa yeye ndio anaejua Tanzania nzima wapi kuna njaa na wapi hakuna.

Au hawa watu wameamua kumjaribu mkuu wa kaya?
 
Kishapu siyo WASHAP wala Whatup! Hawapigi Pushapu....Kiwilaya chao ni Kishapu kwa kuripoti maafa. Tafazai, kitengo cha maafa, temebeleeni Kishapu Chap Chap.... Nendeni kule wala msisubiri kutumia whatsup...
 
Back
Top Bottom