Baraza la "Hikma" Kuhusu Amri za Baba!

Baraza la "Hikma" Kuhusu Amri za Baba!

Bazazi

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2008
Posts
2,806
Reaction score
3,502
BARAZA LA 'HIKMA' KUHUSU AMRI ZA BABA

Nikateuliwa mwenyekiti wa baraza kusikiliza mashauri kadhaa ya kifamilia. Baraza lilikuwa na wajumbe wengi tu. Nikavimba mwenyewe kwenye kiti cha uamuzi.

Nikaomba kusikiliza shauri la kwanza. Watoto wawili, mmoja mvulana mwingine msichana wakasimama kuzungumza.

Kwa kifupi malalamiko yao ni kwamba baba yao anawanyanyasa sana pamoja na mama yao.

Walisema tukio la hivi karibuni ni kuwa nyumbani kwao kulikuwa na ujenzi unaendelea. Hivyo, baba yao alikodi gari la mchanga. Aliwaita wenye gari, akawaelekeza mahali pa kuweka mchanga.

Gari la mchanga lilipofika, waliona ile sehemu ambayo baba aliagiza mchanga uwekwe gari halifiki. Ikabidi waumwage mchanga sehemu nyingine.

Baba aliporejea usiku na kukuta mchanga umewekwa mahali ambako siko, alimwita mkewe: "We' mwanamke kwa nini mchanga umewekwa hapa?"

Mke akajibu: "Nilisikia wanasema pale gari lisingefika, hivyo wakaona urahisi ni kuushusha hapo."

Baba: "Kama gari halifiki, kwa mini usingewaambia waubebe kwa mifuko na ndoo ili kuupeleka pale nilipoagiza?"

Mke alipotaka kujibu, mume wake alimkatisha, akasema: "Si nimeagiza wewe umeshindwa kusimamia agizo? Sasa wewe na watoto wako mtahamisha huo mchanga kwa mikono usiku huu mpaka uishe."

Wale watoto wakiwa wanalia, walisema kuwa baba yao ni mkorofi sana, anawatesa. Walisema siku hiyo hawakulala, walikesha wakibeba mchanga lori zima, kuutoa uliposhushwa na kuuweka alipokuwa ameelekeza baba yao.

ZAMU YA MASWALI

Wajumbe waliwauliza maswali wale watoto ya kutafuta ukweli wao, mwisho nikatakiwa nitoe hukumu.

Kabla ya kutoa hukumu nikawauliza wale watoto: "Siku hiyo baba yenu alikuwa amelewa pombe?" Wakajibu: "Huwa hanywi pombe kabisa."

Nikawauliza tena: "Ni mara ngapi hufanya uamuzi wa aina hiyo, watu wanaadhibiwa kwa makosa ya wengine?"

Watoto wakajibu: "Mara nyingi sana. Hiyo ndiyo kawaida yake. Juzi dada wa kazi alichelewa kupika alikuwa anajisikia vibaya. Mama alikuwa kazini. Sisi tulikuwa shule. Tuliporudi nyumbani baba akasema nyumba nzima hamna kupika wala kula siku mbili, eti kwa nini dada wa kazi acheleweshe chakula?"

Nikawauliza wale wale watoto: "Mna uhakika baba yenu havuti bangi kweli?" Wakajibu: "Baba ni mchamungu. Hanywi pombe, havuti sigara sembuse bangi."

NIKATOA HUKUMU

Niliwaambia: "Poleni sana watoto. Mna bahati mbaya sana. Baba yenu alizaliwa akiwa amelewa. Inawezekana pombe au bangi au vyote kwa pamoja."

Nikafafanua: "Dunia ina watu wa aina hiyo. Wanazaliwa wakiwa walevi. Utawaona kwa vitendo vyao, wanavyozungumza na wanavyoamua. Unakuta mtu mzima kabisa lakini anazungumza pombe tupu au bangi tupu. Sasa mtu huyo akirogwa anywe pombe au avute bangi utamkoma."

Nikasikia baadhi ya wanaume wanaguna, "aah, oooh, eeeh, iiiiih" mimi niligonga meza ili nisikilize shauri la pili.

SHAURI LA PILI

Mama wa makamo akasimama. Akatoa malalamiko yake kwamba mtoto wake alifeli shuleni. Baba aliporejea nyumbani na kuona matokeo akawa mkali. Akatembeza kichapo nyumba nzima.

"Mimi nilipigwa mpaka macho yakavia damu. Mwili wote ulivia damu. Yule mtoto aliyefeli mpaka leo kakimbia nyumba, ameona baba yake atamuua. Watoto wengine walipigwa kwa kufeli ndugu yao," alisema yule mama.

Nikasema: "Uzuri mama wakati nasoma hukumu ya wale watoto wawili ulikuwemo. Kimsingi mume wako naye alizaliwa amelewa. Ama ni pombe au bangi."

Mama akasema: "Ndiyo maana kila akikasirika huwa ananuka pombe! Ndiyo maana akifoka tu huwa anaanza kunuka pombe! Ndiyo maana nikimdai matumizi tu anaanza kunuka pombe halafu ananijibu kipombepombe. Leo sasa nimeelewa."

HOJA YA MJUMBE

Mjumbe mmoja akasimama, akanirudi. Alisema: "Mwenyekiti unataka kutuharibia maadili ya familia. Mwanaume lazima aamue kiume. Mtoto anafeli, unatoa mkong'oto nyumba nzima. Huo ndiyo uanaume. Watajuaje wewe ni baba bila kuonesha utemi?

"Yule baba wa wale watoto ndiyo anafaa kuitwa baba. Nyumba nzima mnakesha mnabeba mchanga ili tuheshimiane. Wanaume lazima tuwe wababe ili tuheshimiwe kwenye nyumba zetu."

Yule mjumbe aliendelea: "Wanaume tunatakiwa tuwe na uamuzi kama wa Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte. Mtu akituhumiwa au akihisiwa anatumia au anauza dawa za kulevya anauawa. Duterte amewaagiza polisi waue tu. Huo ndiyo uanaume."

Nikamjibu mjumbe: "Falsafa ya uanaume kwenye familia au uongozi haipo hivyo unavyosema. Uanaume kwenye familia na uongozo unataka utiifu, nidhamu, urafiki na unyenyekevu. Kinyume chake ni ulevi tu.

"Baba kwenye nyumba, mke na watoto wake aliwatafuta mwenyewe ili washirikiane kujenga familia moja. Alijiona yeye si mkamilifu bila familia. Baba ndani ya familia ni mtumishi. Mke na watoto ni mabosi wa baba ndiyo maana hujihimu ili kuwapa huduma stahiki.

"Kiongozi pia ni hivyohivyo. Wananchi ni mabosi wake. Wao ndiyo wamempa ajira ya kuwatumikia kwa kuwaongoza. Polisi siyo mabosi wa kiongozi, bali ni wafanyakazi wa kiongozi kwa niaba ya wananchi ambao ndiyo mabosi wakuu. Hivyo, kiongozi hupaswa kuwatumia polisi ili kuwatumikia vizuri wananchi. Siyo kuwatumia polisi kuwaonesha cha moto wananchi.

"Duterte anakosea kujigeuza bosi wa wananchi na kuwatumia polisi kuwaonesha cha moto wananchi na hata kuwaua. Mfanyakazi kujigeuza bosi kwa mabosi wake, hiyo ni dalili ya ulevi. Hata wale akina baba wenye kunyanyasa wake zao na watoto wao, hao ni walevi. Walizaliwa wamelewa. Hivyo ni walevi kabla ya pombe. Yaani wao wenyewe ni pombe kichwani."

KIKAO KIKAVURUGIKA

Baada ya kusema hivyo, wajumbe wengi ambao walikuwa wanaume walikuja juu. Walisema uanaume lazima uheshimiwe.

"Lazima uamuzi wa kiume uheshimiwe. Uanaume ni nguvu. Mtoto mmoja akifeli, nyumba nzima bakora. Simu moja ikiibiwa Tandika, wakazi wote na wapitanjia wanakamatwa. Wanapewa mkong'oto mpaka walipe. Msokoto wa bangi ukionekana kwenye pantoni, abiria wote wanakamatwa, wanabondwa ikiwezekana wote wauvute," walipaza sauti wanaume.

Nikajaribu kuwatuliza, wakazidi kuja juu. Walisema: "Uamuzi wa kiume ndiyo unaongoza dunia. Mtaani akikutwa mtu anavuta bangi, mtaa mzima wanakamatwa, wanapelekwa mahabusu. Tukiona shamba la bangi Dar es Salaam, watu wote wa Dar wanabebwa msobemsobe kwenda kufyeka."

Nikasema: "Ninyi wajumbe mmekuaje? Ina maana mpaka wazee, viongozi wa dini, raia wema kabisa, wagonjwa na walemavu wasio na hatia nao wabebe msalaba kwa makosa ya wengine?"

Wakajibu: "Huo ndiyo uanaume!!!"

Sijakaa vizuri nikapigwa mtama, nikaondolewa kwenye kiti. Nikasikia sauti inasema: "Kuanzia leo wewe siyo mwenyekiti."

Nikawa nimepinduliwa na 'hikma' zangu.

Ndimi
Luqman MALOTO
08/04/2018
FB
 
Hii stori INA muhusu Bwana mmoja, we jishebudue tu km una vyeti vya bibi zako wte wawili
 
Kanda ya ziwa wanaume hawapatanishwi kabla hawajapigana, subiri wapigane kisha wapatanishe.
 
Mwandishi umepoteza Muda wako mwingi Sana. Andika vitu vya maendeleo bana
 
I second this
 
Back
Top Bottom