Atasubiri apigiwe kelele zingine ndipo aamue kuwashtaki wachache kwa kesi ambaya anajua watashinda. SWALI; Hivi hao mawaziri wakiondolewa kwa ajili ya WIZI, je,watafaa kuendelea kuwa wabunge?
Hiyo habari umeipata wapi au ni mawazo yako?
Inasikititisha sana kuona watanzania wanakosa mang'amuzi juu ya jambo hili! Wengi wametega masikio yao ili kusikia tu uteuzi wa baraza jipya la mawaziri. Ingekuwa katika nchi nyingine kabla ya jambo lolote, ajenda kuu hapo ingekuwa wahujumu uchumi kupelekwa mahakamani; tena kwa maandamano ya hali ya juu na hata fujo! Hili ndilo jambo la kwanza ambalo lingesubiliwa kwa hamu na kila mtu. Lakini kwa Tanzania ni kinyume chake! Kinachosubiriwa kwa hamu ni uteuzi wa mawaziri wapya! Baada ya uteuzi tuendelee kudumisha amani na utulivu! Haya nayo ni mazingaombwe mengine! Bado tuna safari ndefu!
Heshima kwa wote. Ujanja wa JK. J.K anampango wa kubadilisha baraza la mawaziri na siyo kuwawajibisha mawaziri waliyofuja mali za umma. Ujanja anaotaka kuutumia J.K si kuwawajibisha ila atabadili baraza zima na kuwaacha wale waliyo husika ili ionekane kuwa hawajawajibishwa bali ni timua timua ya wengi. Kwa hiyo msahau kuhusu wao kupelekwa mahakamani. Kwani akiwawajibisha mawaziri hao pekee atalazimika kupambana na upepo wa kuwapeleka mahakamani.
Tulikuwa na imani sana na mkulu wetu alipochukua nchi lakini bahati mbaya imekuwa kinyume
peke yako, usinisemee mimi na ukoo wangu.
si kuwafuga bali anashiriki wizi pia ni mwizi mwandamiziHata yeye hatumtaki analea na kufuga wezi