Baraza Jipya la Mawaziri Kivuli wa CHADEMA kujaza nafasi ya ZITTO KABWE na kuwaondoa Mawaziri Mizigo

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau,

Mara baada ya kutangaza kumvua nafasi zote Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Waziri kivuli wa fedha, ZITTO KABWE, Mwanasheria wa CHADEMA, TUNDU LISSU alitangaza kuwa Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE angetaangaza Baraza jipya la Mawaziri ndani ya kipindi cha bunge lililomalizika. Lissu alisema kuwa uteuzi huo wa baraza jipya la Mawaziri Kivuli utalenga kuwaondoa Mawaziri Mizigo ambao wameshindwa kutimiza majukumu yao.

Mytake: Kama CHADEMA mpaka sasa wameshindwa kujaza nafasi ya ZITTO na wameshindwa kuwaondoa mawaziri mizigo, wanapata wapi uhalali wa kuiandama serikali juu ya baraza hili la Mawaziri ambalo limetangazwa hivi karibuni?
 
CHADEMA hawajashika dola lakin wanathubutu kufanya maamuzi magumu,

vipi kuhusu yule "mshkaji" wa magogoni anayetoa kibanzi na kuweka boriti kwenye jicho la watanzania?

tumuweke kundi gani? tapeli? au naye ni kiranja wa milembe anayewachagua vichaa wenzie kuongoza kundi kubwa la wasomi nchini mwetu.
 
jadili hoja ni kwa nni baraza halijajazwa?
 
Si wakati wa kujaza baraza la mawaziri kivuli maana kazi yao sio kila siku kama mawaziri wa serikali. Sasa ni wakati wa kujadili Katiba Mpya tusibiri wakati wa kikao kijacho cha Bunge Mbowe atatangaza.

Na huyo aliyeweka mambo ya Zitto tumechoka na upuuzi huo.
 
Mkuu, kama ndo hivyo, basi CHADEMA hawakutenda haki. maana bunge lililomalizika limefanyika bila ya kuwa na waziri kivuli wa fedha. pia limefanyika bila kuwa na naibu kiongozi wa upinzani bungeni. pia limefanyika huku Mawaziri Vivuli Mizigo wakiendelea kuharibu
 
Mahakama inatuchelewesha.

ukimuondoa tundu lissu kidogo na mnyika, nitajie mbunge mwengine wa chadema (bila chuki!) walau anayeweza kufikia nusu ya uwezo 'kichwani' wa zito?!
mbowe mwenyewe pia ni mzigo tu, tena mzito!!
 
Dah! hakika ukweli unadhihiri sasa. umeuliza swali ambalo nina hakika hakuna msukule utakaoweza kulijibu
 
ukimuondoa tundu lissu kidogo na mnyika, nitajie mbunge mwengine wa chadema (bila chuki!) walau anayeweza kufikia nusu ya uwezo 'kichwani' wa zito?!
mbowe mwenyewe pia ni mzigo tu, tena mzito!!

Wenyewe watakuambia ni LEMA.
 
Chadema hawana jipya kwenye jamii ya watanzania pengine iwe kwenye jamii nyingine ila siyo kwa watanzania.
 
Mkuu, yaani chadema wanachekesha sana, wanaangalia vibanzi kwenye macho ya wenzao huku wao wana maboriti
 
Back
Top Bottom