Barasa Chabi avunja ukimya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barasa Chabi avunja ukimya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 7, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,053
  Trophy Points: 280
  SHIRIKA la Umeme (Tanesco), ambalo limekwama kutekeleza mpango wake wa kupitisha nyaya za umeme zenye msongo mkubwa juu ya eneo liliko Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, limesema linafanyia kazi vitisho vilivyotolewa na waumini wa kanisa hilo.

  Kiongozi wa kanisa hilo, Askofu Zacharia Kakobe ametangaza eneo hilo lililo Mwenge jijini Dar es salaam kuwa ni hatari kwa mfanyakazi yeyote wa Tanesco na kwa sasa waumini wanalilinda wakiwa wamevalia fulani zilizo na maandishi wa kulikejeli shirika hilo la serikali.

  Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, meneja msaidizi wa mawasiliano wa Tanesco, Barasa Chabi alisema kuwa shirika hilo linafanyia kazi vitisho hivyo vya kanisa hilo na kwamba mpango wa kupitisha umeme eneo uko palepale kama lilivyopangwa.

  "Unajua sisi kama Tanesco hatutaki kuvutana na kanisa la Kakobe ndio maana tulitoa msimamo wetu juu ya suala hilo. Nadhani hakuna kitu kitakachobadilika, mipango ya kupitisha umeme iko palepale," alisema Chabi.

  Aliongeza kuwa tayari Tanesco ilishatoa maelezo yake juu ya mradi huo wa kupitisha umeme na kutoa elimu kwamba umeme huo hautakuwa na madhara yoyote kwa watu au kanisa hilo zaidi ya kuharakisha maendeleo kulingana na kukua kwa mahitaji ya huduma ya umeme katika jamii.

  Waamini wa FGBF wakiongozwa na askofu wao wameeleza bayana kuwa watazuia utekelezwaji wa mradi huo kwa kuwa ni hatari kwao na kwamba utavuruga mfumo wa sauti wakati wa ibada ambazo kwa kawaida hurekodiwa kwa ajili ya kurushwa kwenye televisheni.

  Kakobe pia ameeleza kuwa kanisa lake lina mpango wa kujenga studio ya televisheni kwenye eneo hilo.
  Waumini hao wanalinda eneo hilo kwa saa 24.
  Tanesco inataka kupitisha nyaya za umeme wa msongo mkubwa kutoka kituo cha Ubungo kuelekea Kijitonyama ambako kinajengwa kituo kidogo cha umeme kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo kwa wakazi wa Mikocheni, Oysterbay na maeneo mengine ya jirani.

  source: Mwananchi
   
 2. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  TANESCO endeleeni na kazi yenu hizo kelele za Kakobe na waumini wake ni nyimbo tu na hekaya za Abunuwasi.Kwani cha kushangaza kule anakoishi Kakobe Kijitonyama wanalalamika naye akiwa mmojawapo kuwa umeme ni kidogo sasa wamesogezewa Sub station karibu yeye anataka kuzuia njia ya kupitisha umeme.Kwani Kakobe yuko juu ya sheria??Si aburuzwe mahakamani tuu kwa kuzuia shirika la umma kutekeleza wajibu wake?Ila ujanja anao tumia yeye hajitokezi bali anawasukuma waumini wake wasio na uelewa wa sheria kuandamana na kuwazuia TANESCO.
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huu msimamo ndo mzuri, kakobe alie tu, alikuwa wapi siku zote kujenga hiyo studio na tv yake?mambo mengine sio ya kufumbia macho kwani anataka kuleta kisingizio cha udini hapo, penye ukweli lazima uzungumzwe tu!
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kanisa gani linatetea uvunjaji sheria?
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,053
  Trophy Points: 280
  kanisa la kakobe
   
Loading...