Barabara za Same hazifai. David Matayo na Anna Kilango Mpo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara za Same hazifai. David Matayo na Anna Kilango Mpo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kinepi_nepi, May 8, 2012.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ubovu wa barabara za wilaya ya Same mkoa wa kilimanjaro, jimbo linaloongozwa na wabunge wawili upande wa Magharibi David matayo na Upande wa Mashariki Anna Kilango, ni hatari na hazifai kwa matumizi ya wanadamu. Barabara hizi hasa za Milimani kuliko na wakzi wengi (wapiga kura) ni mbaya na hazipitiki kabisa kipindi cha mvua.

  Wakazi wa Gavao, Saweni, Bwambo na mamba Miamba wamewalalamikia wabunge wao kwa kuwadanganya na kuwahadaa kipindi cha kampeni. Wakati wa kampeni kwa nyakati tafauti wabunge hawa walipandisha matingatinga ishara ya kuongeza na kusawazisha hizi barabara kumbe ilikuwa danganya toto kura zipigwe.

  Masikitiko makubwa sana sehemu za milimani kuna vitua vya afya vichache sana visivyo na uwezo wa kutoa matibabu mazuri hivyo kutumiwa kama sehemu ya kuhamishia wagonjwa kupelekwa Same mjini au KCMC. Mvua ikinyesha usafiri unakuwa hakuna hivyo wazazi kuteseka na wagonjwa kufa kwa kukosa rufaa kwani gari la wagonjwa ambalo ni la Kanisa hushindwa kwenda sababu ya ubovu wa barabara na utelezi.

  Barabara hizi zilichimbwa kwa nguvu za wananchi wenyewe miaka ya 1970, 1980, 1990 kwa wananchi kutengeneza njia ili matingatinga yaweze kupanda na kuchimba kuanzia juu. wananchi wakatimiza wajibu wao kwa kujitolea wanasiasa wakawakaanga kwa lugha za uongo na kura.

  Katika Tarafa ya Mamba Miamba wajawazito inawapasa kutembea kwa miguu Kutoka Miamba mpaka Bwambo ilipo Hospitali ya Kanisa ambayo ndiyo pekee inasaidia wagonjwa kwenye ukanda huu.

  Pamoja na kuwa na Mlima shengena wenye madini na mandhari nzuri kwa ajili ya watalii, miinuko mizuri na hali ya hewa safi kwa ajili ya ujenzi wa hoteli na sehemu za kufanyia mapumziko nzuri, viongozi wa Same wamekosa ubunifu na kulifanya Jimbo lionekane kama halifai kuishi mwanadamu.

  Elimu imeshuka na shule za msingi na sekondari kuwa ni daraja la kuzalisha wasio na uwezo na kushindwa kuandaa kizazi kipya.

  Matatizo Mengi yanasababishwa na kuwa na viongozi wasioishi maeneo husika hivyo kutoathirika na huduma duni na mbovu za shule, barabara , hospitali na huduma muhimu za jamii.

  Mbunge David Matayo Naomba uende Saweni-Gavao, Na nenda Kijomo Kirangare, Nenda Suji na kwingineko uniambie kwa nini huwezi kwenda kuwasalimia wapiga kura wako wa milimani. Umewaahadaa na ubovu wa barabara amabayo wewe mwenyewe unaiogopa kuipitia.

  Anna Kilango Barabara hii ya Saweni-Gavao-Bwambo mamba Miamba mnagawana katikati na Mwanao David wewe umehamia kabisa Dar hujui wala hutaki kuisikia, umewaacha wananchi kama wakiwa. Kiwanda cha Iliki imekuwa ni siasa mbovu sana kuwaachia wananchi magofu ukiwaahidi eti unajenga kiwanda cha iliki. Kwa nini kampeni zikiisha hamwendelezi yaliyowapa kura???

  Jimbo la Same limekuwa mkiwa viongozi wake wamelitelekeza, halina ubunifu, hakuna vyonzo vya ajira, wala hakuna kiongozi mwenye kuthubutu.

  Jimbo lenye rutuba kwa ajili ya viazi, matunda, kahawa, iliki, na uoto wa asili, madini, mbuga za wanyama, maeneo mazuri ya utalii, miinuko ya kuvutia na kijani kibichi mwaka mzima. Kwa nini wananchi wake bado ni masikini????

  Nina Picha nimeshindwa kuzi-upload.

  Ni mimi Mzee wa Nepi
   
 2. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anna malecela hata rudi tena, ameshapima upepoo amegundua kuwa hamtamchagua tena.....kwa hiyo tafuteni alternative, labda huyo Mathayo...
   
 3. s

  simon james JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matayo naye hatarudi tena kwahyo same wametelekezwa
   
 4. o

  oakwilini Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anna kilango amebaki kuwa kama vuvuzela,anapiga tu domo jimboni anapewa kura kisha anaenda zake Dodoma kwa mumewe anawaachia watu shida zao.Ameahidi lami,kiwanda cha tangawizi,ajira kwa vijana,maji safi ya bomba lakini hadi leo hakuna kilichotekelezeka.Amechangisha zaidi ya mil 300 kwa ajili xa kiwanda matokeo yake amekwenda kuchnngesha vinu vya kusaga tangawizi(vitatu) kila kimoja kina thamani ya mil 8.Pia kilango amejenga majengo hizo mashine kwa kiwango duni lakin cha ajabu jk anatajwa kwenda kuzindua mradi huo uliojaa harufu ya ufisadi na siasa za danganya toto.Namwambia Kilango kwamba zama za ujinga zimeisha asubiri gharika 2015.
   
 5. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wabunge hawa ni janga la wilaya ya Same. Tunataka watoke waje wachapakazi maendeleo ni haki yetu.
   
 6. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  funga kazi ni barabara ya chome.
   
 7. l

  laigwenan JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  poleni wana same hii ndo Tanzania Bwana,msimwonee aibu mtu mwongo 2015 itumieni kura yenu vizuri kulipa kisasi kwa kujaribu upande mwingine tuone kama itafaa
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  haya maeneo ni same mashariki ama magharibi?
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Watengeneze barabara za kazi gani while hawaishi maeneo hayo??

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 10. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2014
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dr Mathayo David kafukuzwa uwaziri, sijui atakwenda Suji kuwasalimu aliowatenga?????
   
 11. K

  Kilahiro Senior Member

  #11
  May 25, 2014
  Joined: Aug 5, 2013
  Messages: 171
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Barabara zanini na kanga na kufia zinamaliza mchezo
   
 12. k

  kirikuu10 JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2014
  Joined: May 4, 2014
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si uliwasikia siku walipo kuwa jimbo la T.LIssu walivyo kuwa wanjidai kuponda utadhani majimbo yao yana neema ,ccm kwa unafiki nafikiri wanaongoza dunia nzima.
   
 13. k

  kireri jr JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2014
  Joined: May 10, 2014
  Messages: 228
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  si waliitaka CCM acha waone joto
   
 14. o

  ommymbwambo Senior Member

  #14
  May 27, 2014
  Joined: Mar 25, 2014
  Messages: 193
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ila hata barabara ya bomani kwenda ofisini kwa mkuu wa wilaya nayo vumbi mpaka leo.wekeni lami hii barabara
   
 15. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2014
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Ccm oyeee
   
Loading...