Barabara za lami za dar kuwa vumbi ifikapo 2020 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara za lami za dar kuwa vumbi ifikapo 2020

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Semilong, May 23, 2010.

 1. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Jiji la dar limeanza ukarabati wake wa barabara za lami. Kama barabara ya lami ina shimo dogo, hilo shimo dogo linapanuliwa zaidi na kusawazishwa na kuwekwa kifusi badala ya kuwekwa lami. Operesheni hii inaenda kwa kasi sana.

  Kwa wale wanaoishi jiji la dar mnaweza mkajiona hali hii kwenye maeneo ya ocean road (sea view) nje ya fk law chambers, wengine mnaweza kujionea babara ya tandale inaetokea sinza maeneo ya kwa mtogole mpaka sinza, wengine mnaweza mkajionea maeneo mbalimbali ya temeke.

  Kama operesheni hii ikifikia njia ya kwenda mwananyamala hospital basi ile barabara yote itakuwa vumbi maana mashimo ni mengi sana.

  Kama operesheni hii ikikamilika jiji la dar litakuwa halina barabara ya lami ifikapo 2020.

  Mungu tumekukosea nini, kwanini unatuadhibu kiasi hichi. Yaani kila kitu kibaya kinatokea kwetu tu, kwanini umetupa viongozi wabaya kiasi hichi. mungu kama kweli upo ua viongozi wote wabaya na utupe wazuri
   
 2. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mungu alitupa nchi, iliyojaa kila alichoona chafaa na chapendeza machoni pake. Akaiwekea na watu wa kuitiisha. Kujiuliza ni wapi tuliomkosea Mungu, ni kama kuhoji ni kwanini Mungu akatupa nchi hii. Ni wajibu wetu kuitunza na kuitiisha. Tujiulize wenyewe ni wapi tuliokosea tangu taifa hili lilipoasisiwa. Tumekuwa wepesi wa kudanganywa, na kila baada ya kufanya maamuzi yenye kutuumiza wenyewe, tunamgeukia Mungu na kumuuliza ni wapi tulipomkosea badala ya kumshukuru kwa mema aliyotukirimia.
   
Loading...