Barabara za Dar Es Salaam Mashimo ni too much kha!

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
13,385
9,752
Wadau wa JF ikiwemo Raisi na Mkuu wa Mkoa..

Hivi Mashimo barabarani ni Aina ya Siasa au ni Makusudically tu.. Karibu kila barabara nayopita jijini Dar Es Salaam ni Mashimo mwanzo mwisho.. last two week mida ya usiku niliona wadau wakiyafunika mashimo pale maeneo ya Mnazi mmoja Barabara ya Uhuru wakapandisha hadi juu juu hivi kulikuwa na Shimo la ajabu lefu kuelekea chini.. ila after one week hali ni ile ile mashimo tena... Hivi kuna utaratibu gani naweza fahamishwa wale wafukia mashimo barabarani kiasi gani wanalipwa maana ni work done zero job. i mean ni upumbavu kuwalea watu aina hii... i hope Meya anahusika au nikifahamishwa tu kuwa pengine mdau tu alijitolea maana Gov imeelemewa somehow kwa ajili ya reli na Umeme...

Na kama mimi ni mdau binafsi naruhusiwa kufunika mashimo kwa cement kali maana hizo rami sijui hata zinapopatikana. Bitumen ila nakumbuka kuna miaka furani wacomoro walikuwa wakija Dar wananunua lami kujengea kwao ila walianza kulalamika kuuziwa rami feki maana kwa uzoefu wangu na barabara za tz rami yenu inayojengea ni fake...

Barabara ya Uhuru ni aibu sana... ni bora ibadilishwe jina iitwe mkweche road.

Shauri moyo pale mashimo yake tuite Makonda Raod pengine itatizamwa

Kibarabara cha kuelekea Ferry chembamba na kimemeguka meguka ovyo nayo inapakana na ikulu aibu sana...

Nilipita tokea machinga complex nikakatiza kulia kuelekea mataa ya chang'ombe baada ya kona tu sikuamini mishimo yake kha!

Kuna Njemba na vigari vyao vichovu huwa sometimes wakiona mashimo hufika eneo la tukio kisha kuchonga zaidi shimo kwa square and then husepa forever wtf!

Ningependa kuwafahamu wanaozihudumia barabara za DSM maana yatosha unakuta barabara inakashimo kadogo kanaongezeka hadi linageuka Handaki..
 
Kwa jina maarufu zinaitwa barabara za KIANGAZI , ni barabara za udongo zilizolambishwa lami uchwara juu yake .
 
Penye population kubwa ndio inatakiwa kuwa kipaumbele cha serekali Sasa sijui Vipi !?
 
Mwenye mamlaka yake yupo busy kuaigiza samani kwanza na kutafuta mababa wa DNA, hizo barabara huenda hazituhusu.
 
Mkuu ziko barabara zinazoitwa RINGROAD utawasikia hizi barabara tutaziboresha kwa kiwango cha lami ili zisaidie jiji letu la DSM

Tokea Victoria ,kuelekea Hospital ya Dr KAIRUKI pita mbele ,kisha kona kushoto balaaaa,pale nadhani wavuvi hawajagundua lazima kuna MAKAMBALE wakavue.

Nenda barabara ya Kilwa eneo la Kongowe ni hatari barabara imechimbika ,inapigwa viraka fake.vinachimbuka.

Nawapenda na nawapongeza vijana wanaookoa na kuomba maji ya kunywa WAUNGWANA huwa tunawaunga mkono kwa kuwapa tulichonacho.

Maana gari za wanaotufikiria ubora Wa Huduma tunazostahili HAWAISHI TUNAKOISHI HAWAPITI TUNAKOPITA.

jiji linataka UKARABATI MKUBWA. uongozi kama Wa tume ya MH KEENJA unahitajika.

MACHINGA ni kila kona, viongozi ubunifu ni 0
 
Back
Top Bottom